Hongera Tanganyika kwa kutimiza miaka 53 ya uhuru. Sherehe za leo zilikuwa za mwisho kwa Rais Jakaya Kikwete akiwa madarakani.



Leo ni mwaka wa 53 tangu upatikane uhuru wa Tanzania bara(Tanganyika) kutoka kwa muingereza, kama ilivyo ada ya miaka mingi, 9 Desemba huwa kuna sherehe za kuadhimisha siku hii

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama Rais Jakaya Kikwete wakati  akiwasili katika uwanja wa Uhuru ambapo sherehe za miaka 53 zikiathimishwa hapo ambapo yeye ndiye mwenyeji wa sherehe hizo ambazo kwake ni za mwisho katika uongozi wake.
Awali Rais alifika na kupanda jukwaa maalumu,ambapo uliimbwa wimbo wa taifa ukifuatiwa na upigaji wa mizinga 21, na baada ya hapo akafanya ukaguzi wa vikosi vya ulinzi na usalama.
Maadhimisho haya ya tanzania bara yanaathimishwa toka ilipojipatia uhuru toka kwa Muingereza Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya ya 53 ni muhimu kwa Watanzania, kutokana na kwamba nchi ipo katika kipindi cha uchaguzi, ambapo Watanzania siku ya Jumapili Desemba 14, watapiga kura, katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
Uchaguzi huo ni muhimu, kutokana na viongozi katika ngazi hiyo kuwa karibu kabisa na jamii.
Tanzania pia inaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake ikiwa katika harakati za uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika mwakani.


Waziri mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Ally Mohamed Shein. uwanja wa taifa.
RaisJakayaKikwete akiingia uwanjani, Pembeni ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamnyange.
Mweshimiwa Rais Akikagua gwaride maalum lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama.
Waziri mkuu mstaafu Fredirick Sumaye akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiq
JWTZ  gadi ya wanawake wakiwa kazini uwanja wa taifa leo.

Comments