JE, KUNA MASHINDANO YA UREMBO/U-MISS KWENYE BIBLIA? JE, ESTHER ALISHIRIKI MASHINDANO YA UREMBO?

Na Mchungaji  G. Daniel ambaye pia ni mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili Tanzania.

Labda tuweke rekodi sawa hapa, kweli inazidi kupotoshwa hasa na wale ambao waliatazamiwa kuisimamia. Na maoni ni kwamba tunapoamua kutetea jambo sio lazima tuilzamishe Biblie iseme kile ambacho haisemi. Sio lazima tulazimishe vifunge visomeke jinsi ile tutakayo sisi.

Kuna mtu ameniuliza swali; Je, ni kweli Esther wa kwenye Biblia aligombea kwenye mashindano ya urembo (umiss)? Hapa nitajibu swali hilo, naomba uwe mvumilivu usome kila kitu hapa, na ukawe mwalimu wa wengine pia.

1. ESTHER NI NANI? Kwanza ifahamike kwa wengi, kwamba huyu anayeitwa Esther hapa alikuwa miongoni mwa Wayahudi waliokuwa uhamishoni Babeli katika Jimbo la Shushani Ngomeni. Jina hili Esther halikuwa jina lake halisi, ni jina la Kibabeli ISHTAR lenye maana ya mungu mke wa mashariki kule Shushani Ngomeni. Jina halisi la Esther ni la Kiebrania yaani HADASA lenye maana ya mti mzuri uliokuwa ukitoa marashi/harufu nzuri, ya kupendeza na kuvutia.
 
2. JE, NI MASHINDANO YA UREMBO? Mfalme Ahusuero aliachana na Mkewe aliyekuwa akiitwa Vashti baada ya kutokea mgogoro kati yao. Ndipo ikatangazwa mbiu ya kutafuta wanawake wanawali ambao siku ya siku wangepita mbele ya Mfalme ili apatikane mmoja miongoni mwao atakayekuwa MKE wa Mfalme. Haya hayakuwa mashindano ya Urembo, lilikuwa ni tukio ambalo Mfalme angelitumia kupata msichana ambaye angekuwa kuwa mke wake. ESTA 1-3

Kama kuna watu Wakristo ambao wanavutiwa na mashindano ya urembo kwa sababu ya mamilioni ya pesa wanazopewa washindi, kwa gharama ya kuonyesha maungo hadharani nk, basi wafanye hivyo kwa sababu ya mfumo wa dunia umewakamata na wakanaswa, lakini wasijaribu kuipotosha Biblia kuwa imeruhusu mashindano ya urembo.

Esther (Hadasa) hakuwa anagombea urembo (Miss Shushan Ngomeni) hapana, alikuwa anawania nafasi ya kuwa mke, ulikuwa ni utaratibu wa Kibabeli na sio wa Kiyahudi. Tunaposhindwa maisha ya kuishi sawasawa na Neno la Mungu tusitafute visingizio kwa kuilazimisha Biblia isomeke namna ambavyo haisomeki.
Kushindwa kwangu/kwetu na dhambi kusiwe sababu ya kudanganya watu kuwa Biblia imehalalisha kile tunachokifanya, UKWELI UTASIMAMA HATA KAMA HAKUNA ANAYEUTETEA!
MUNGU AKUBARIKI.
BY MCH. OVERCOMER DANIEL
MLIMA WA MAKIMBILIO
DAR ES SALAAM - TANZANIA

Comments