JE NI DHAMBI KUHUBIRI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII?

BWANA YESU asifiwe ndugu zangu.

NISAIDIENI HII.


KUNA MTUMISHI AMENIAMBIA.

-Wewe Peter Hujaitwa na MUNGU maana aliyeitwa na MUNGU hawezi kuhubiri Facebook.
-aliyeitwa na MUNGU hawezi kuwaambia watu maneno magumu kama wapingakristo na wafuga majini.
-Elimu za chuo cha Biblia kinakusumbua tu.
-Hutumii hekima kwenye mafundisho yako.
-Naujua ukweli kuhusu wewe na kinachokusumbua hivyo nitafute nikusaidie.


NIMEMJIBU YAFUATAYO na naomba Watumishi mnisaidie lolote ambalo nimekosea.

- Kuhusu MUNGU Kuniita Wewe Wala Isikusumbue Ndugu Yangu, Kwanza Hukuwepo Siku MUNGU Ananiita Na Pili Sijawahi Kumwambia Mtu Kwamba Nimeitwa Na BWANA Maana Hilo Sio Muhimu Sana Kwa Huyo Mtu Bali Injili Ndio Muhimu Zaidi Kwake. 

-Harafu Ndugu Umesema Unaujua Ukweli Wote Kuhusu Mimi Hivyo Nikutafute. Mi Naona Ukweli Wangu Wote Uanike Tu Hapa Tena Mbele Ya Marafiki Wote Ili Na Wao Wajue Jinsi Nilivyo Maana Ndio Vizuri Zaidi. Kuhusu Mimi Wala Usifanye Siri Hata Moja Ndugu Yangu. Ubarikiwe Na BWANA YESU Aliye Hai.


-sijawahi Kusoma Chuo Cha Biblia Popote Pale Duniani. Hata Hivyo Wanaosoma Vyuo Vya Biblia Sio Dhambi. Ningekuwa Simjui MUNGU Wala Nisingefanya Kazi Yake. Wewe Unaemjua Mbona Hata Huhubiri Habari Zake? Kosa Langu Ni Nini? Sijawahi Kububiri Dhehebu Lolote Zaidi Ya Kumhubiri BWANA YESU Anayeokoa. Tatizo Lako Wewe Ni Nini? Je Tuache Kuhubiri Injili Kwa Sababu Kuna Wanaopinga? Ukayafa Ni Mbaya Sana. Na U-baryesu Peleka Huko Huko.


-Wewe mwenyewe hujawahi kuhubiri popote na hata kwenye Profile yako kuna kubadilisha tu picha, sasa wengine wakihubiri unawaponda wakati wewe hata hujawahi kuhubiri. Mimi naomba MUNGU wa mbinguni aamue kati yangu mimi na wewe. Wala usinitishe kwa habari zako za mara hukuitwa mara mimi najua mengi sana kuhusu wewe, nimekuambia weka hapa yote kunihusu mimi wala usifanye siri maana najua sina kosa wala hatia yeyote.“Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako
duniani.” 1 Yohana 4:3


-Kazi ya karama ya neno la hekima na inavyofanya kazi:
kukupa jibu la swali unaloulizwa lakini hasa swali lenye hila, mtego, ushindani au mashtaka ndani yake.
Luka 21:12-15 inasema ''lakini, kabla hayo yote hayajatokea watawakamata na
kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi........ basi kusudieni
mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza, mtakavyojibu, kwa sababu mimi
nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana
nayo wala kuipinga''.


-Pole sana rafiki, kwa hiyo kwa akili yako hiyo Mhubiri sahihi hawezi kuhubiri fecebook? aliyekuambia ni muongo kuliko waongo wote. Neno la MUNGU litahubiriwa popote Katika Marko 16:15-16 BWANA YESU anatoa maagizo haya kwa kila mtumishi wake '' Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.''
Wewe leo unasema kwamba aliyeitwa na MUNGU hawezi kuhubiri facebook? Wewe huwezi kuhubiri acha tu na kama unadhani fecebook ni mahali pa kubadilisha tu profile picture pole.


-' Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; [Mathayo 7:24] '', mtu yeyote akilisikia neno la MUNGU hata iwe facebook anatakiwa akiamua kumfuata BWANA YESU hakika anaokolewa.


-Umesema kwamba nawambia watu kwa maneno makali, ni kweli kabisa maana kama unaona roho nyingine inaingia kuwazuia watu wasielewe neno la MUNGU au kuwaondoa kwenye kumwamini MUNGU lazima ionywe na ikemewe, Tito 2: 15 Biblia inasema ''' Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote. ''


-Umesema kwamba nakosea ninapowaita watu kwamba ni wapingakristo. nAKUSHANGAA SANA NDUGU KWANI Biblia yenyewe umewataja wapingakristo na sifa zao ni hizi 1 Yohana 2:18-20 '''Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa
sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
Walitoka kwetu, lakini
hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja
nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.
Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. ''',
 

Kwa hiyo tusiwataje? si kweli hao tutawataja ili wajijue na wageuke na kuacha uovu na sio hao tu tutakaowataja hata wachawi, waongo, wazizi na waasherati tutawaja na kuwaonya ili wamrudie BWANA YESU, Hatuhubiri upendo tu hapa mtandaoni. MUNGU anawahitaji watu wote ili wamrudie kwa kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wao.
Ubarikiwe sana uliyesoma ujumbe huu.


Naomba unishauri kwa sehemu ambayo inapungua.
Mtumishi huyu namheshimu sana.
Hata hivyo amesema atakuja tena na majibu sahihi kunihusu.
Mimi nasubiri na nitaleta tena hapa majibu niliyomjibu.
Kama mtumishi mwenzangu unakutana na changamoto kama hizi basi tusaidiane tufanyeje maana sio kila jambo mpaka kuliombea ndio linaondoka, hata msimamo tu unatosha.
Uliyejifunza kitu hapa kwenye ujumbe huu ubarikiwe pia na wewe ambaye imani yako imeongezeka ubarikiwe sana na hata wewe ambaye unaogopa watu kuwahubiria kitu fulani basi jifunze kitu na tuwasaidie watu.
Mbarikiwe sana wote
Ni mimi ndugu yako
Peter Michael Mabula.
Miasha ya ushindi.
Mabula1986@gmail.com.
0714252292.

Comments