KAMBA ZA KICHAWI

Na RP Adriano Makazi akifundisha somo  liitwalo
"Kamba za Kichawi" katika Bonde la Maono -Ufufuo na uzima  Morogoro.

Utangulizi: Wiki iliyopita tulizungumzia habari za vifo vyenye utata. Jambo  la kufufua wafu linawezekan hata leo kwa sababu katika  Biblia wapo  wengi  waliowahi kufa na kufufuliwa. Zaidi sana, Yesu alitupa mamlaka ya kufufua wafu.

Somo la leo linaitwa Kamba za Kichawi”. Zipo kamba zinazotesa maisha ya watu. Wachawi wanaweza kumfunga mtu  kupitia kamba: katika familia yako, kamba za kuzuia hatua za maendeleo yako, kamba za kuifunga ndoa n.k. Ndiyo  maana unaweza kuona mtu anafanya kazi kwa bidii lakini  mabadiliko hayaonekani. Kumbuka kuwa 'kila jambo baya' kwa mwanadamu huanzia kuzimu.  Unapozungumzia mchawi unamzungumzia shetani  mwenyewe kwa kuwa yeye shetani ndiyo mkuu wa wachawi na washirika wake.

Mungu aliye juu anao makuhani wake wanaomtumikia (watumishi wa Mungu, wachungaji,  maaskofu n.k), kama ambavyo makuhani wa shetani ambao ni wachawi,  wapiga ramli, waganga wa kienyeji, wasoma nyota wanavyomtumikia shetani. Kamba zikeshakatika, utaona aliyekuwa akienda akichechemea anakimbia.

Kamba za kichawi kimsingi ni mapepo. Wachawi  huyaita mashetani kwa namna ya kucheza ngomazao za kichawi kwenye madhabahu zao.  Wanapotoa kafara, ile damu  ikeshamwagika huagizwa mashetani ya kutekeleza mashtaka yao. Vikao vya kichawi huitishwa ili kumfanya mtu mmoja aharibikiwe.

Maandiko katika ZABURI 119:61-62 imeandikwa….[Kamba za wasio haki zimenifunga, Sikuisahau sheria yako.62 Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.]… Anayetamka mambo haya ni Daudi, mwana wa Yese, mtu  wa vita. Daudi anatukumbusha kuwa, hata kama kamba za wasio haki  zitatufunga, tusisahau ‘Sheria ya Bwana’.  Kuna mambo ambayo tunamhitaji Bwana peke yake, kwa sababu hata kama utaweka tumaini lako kwa rais, au mbunge, au kiongozi wako hawezi kukusaidia. Daudi hata baada ya kujua amefungwa kamba, alisema ‘msaada wangu u katika Bwana, aliyeziumba mbingu na nchi’. Endapo Daudi aliwahi kufungwa kamba, wewe je?

ZABURI 126:4…[Bwana ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki.]… Leo Bwana ataenda kusimama na kuzikata kamba za wasio haki. Kamba za wachawi,washirikina, wapiga ramli zikatike  kwa Jina la Yesu.  kawaida ya mtegaji anapokuwa anatega,  huwa anaficha mtego wake. Kwa uliyeokoka,  jifunze kunena kwa lugha nyakati zote ili kuitegua mitego ambayo inakuwa imefinchwa njiani.

Mtu anaweza kutegwa kwenye kitambaa. Unaletewa zawadi ya kitambaa na wewe unaondoka na kuanza kujifuta usoni kwa furaha. Kitendo  tu chakufuta jasho,  unajifunaga usoni mwako. Wakati  mwingiene, wachawi wanaweza kuikuletea zawadi ya nguo. Endapo utavaa nguo yenye manuizo ya ainaa hii, na ukatumia hiyo nguo bila kufanya maombi yoyote, unaingia katika huo mtego. Badala ya kuwa umevaa nguo unakuta wewe ndio umevaliwa‼! Kwa mut aliyeokoka, hawezi kuvaa nguo hata ya dukani kwabla ya kuiombea. Katika MARKO 16:17…[Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.]… Ukiwa umeamini, ishara zitafuatana na wewe. Hata kama wachawi watakutegeseha mtego wa kudhuru uhai wako, hawataweza kukudhuru. Shida ipo tu kwa wale wasiomwamIni Yesu.

ZABURI 140:5…[Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.]… Maana yake, njia unayopitia kila siku  kuelekea kazini au sheleni au biasharani  kwako, wenye kiburi  wamekuwekea wavu ili unaswe.

MAOMBI
Kila mtego na kamba na kila wavu kwenye njia yangu, leo naamuru kwa Jina la Yesu, enyi wenye kiburi mliotega mitego na tanzi kwenye njia yangu ya mafanikio,  leo naisafisha njia yangu, naondoa vikwazo na vizuizi kwenye njia yangu. Mashujaa wa kuzimu leo  nawaondosha kwwa Jina la Yesu. Amen


Katika  Biblia wapo watu waliofungwa kamba. Samsoni Mnadhiri wa Bwana, kwa mfano, alifungwa na waliomfunga hizo kamba ni  ndugu zake mwenyewe. Tunajuaje haya? WAAAMUZI 13:5…[kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake;   maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.]… Haijalishi wewe ni nani, hata kama ungekuwa ni  Mnadhiri wa Bwana, ujue unaweza kuwa umefungwa kamba.

WAAMUZI 15:9 …[Basi Wafilisti wakapanda wakapiga kambi yao katika Yuda, wakajieneza katika Lehi. 10 Watu wa Yuda wakasema, Mbona mmekuja kupigana nasi? Wakasema, Tumepanda ili kumfunga Samsoni, kumtenda yeye kama alivyotutenda sisi.]…. Ukumbuke kuwa, Mungu anatokea juu, lakini wanaopanda kwenda juu ni mashetani. Wafilisti  ‘wamepanda’ ili kumfunga Samsoni. Haya yalitokea kwa sababu Samsoni alichukua muda mrefu sana kufanya maamuzi  ya kumuoa aliyemchumbia, na matokeo yake baba mkwe wake akamuoza kwa mwanaume mwingine.

WAAMUZI 15:11-12 …[Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakatelemka hata ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao. 12 Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniangukia.]… Mungu hadhihakiwi, chochote apandacho mtu ndicho  atakachovuna.  Si vizuri kuwafunga ndugu zako kamba. Wachonganishi ni sawa na wachawi tu. Wapo wanaoitana majina mazuri makanisani kama vile ‘mpendwa’ lakini  nje ya hapo humsema mwezake vibaya.

YAKOBO 2:14-16...[Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? 15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?]… Yafaa umsaidie ndugu  yako,  umuonye na umwelekeze na wala  usimtie mikononi mwa Wafilisti kwa Jina la Yesu.

MAOMBI
Mabaya hayatakupata wewe kwa Jina la Yesu. Uwe mbali na mtego wa mwindaji  kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo, nimepita  mautini na nimeingia uzimani kwa Jina la Yesu. Amen


WAAMUZI 15:13…[Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini.]…Wale waliokufunga sana huwa wanafurahi  kuona kuwa hauzai, au hauponi, au haufanikiwi. Fedha zikeshaisha, hata wale uliodhani ni ndugu au marafiki zako  wanakugeuka ghafla na kukuacha peke yako. Wengi wa watu wameumizwa na wale walikouwa wanawaamini sana, na matokeo  yake, maumivu yanayotokea hapo ni makubwa sana na kusamehe inakuwa ngumu.

Wafilisti walisaidia kufunguka kwa Samsoni kwa jinsi walivyopiga kelele zao (WAAMUZI 15:14). Matatizo humsogeza mtu karibu na Bwana.  Daudi baada ya kumuua Goliath, vita dhidi yake na Sauli ilainza rasmi. Imeandikwa 1SAMWELI 18:6-9…[Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.]… Katika dunia ya leo, inaua akina Habili, na kuwaacha akina Kaini. Sauli vivyo hivyo,  alamuonea Daudi wivu tangu siku ile walipomsifu wale wanawake. Hata wewe,  yamkini kifungo chako kilianzia siku ile ulipofunga ndoa, ulipopata scholarship,  ulipopata kazi, ulipoinuliwa kazini n.k.  Kwa kadiri unavyomsema vibaya ndugu yako, ndicyo ambavyo  Bwnana anavyomuinua. Wale waliokutesa na kukusema mabaya, saa inakuja ambapo watakuija kwako kukuomba msaada kama ilivyotokea kwa nduug  zake Yusufu.

WACHAWI HUMFUNGA JE MTU?

LUKA 13:16…[Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?]… Mapepo yanaweza kumuingia mtu na kumfunga. Mtu aweza kuwa na magonjwa ya ajabu ajabu kumbe ni  kamba zimetumwa kwake ili kumfunga.

MATHAYO 17:14-18…[Nao walipoufikia mkutano, mtu mmoja akamjia, akampigia magoti, akisema, 15 Bwana, umrehemu mwanangu, kwa kuwa ana kifafa, na kuteswa vibaya; maana mara nyingi huanguka motoni, na mara nyingi majini. 16 Nikamleta kwa wanafunzi wako, wasiweze kumponya. 17 Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. 8 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.]…Mashetani wanaweza kusababisha udhaifu.

MATHAYO 9:29-33…[Hata hao walipokuwa wakitoka, tazama, walimletea mtu bubu mwenye pepo. 33 Na pepo alipotolewa, yule bubu alinena, makutano wakastajabu, wakasema, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.]… Kila hali unayopitia leo hii,  iwe nzuri au  mbaya,  kuna aliyesababisha hiyo hali. Hata kama hujui kuomba,  waweza kukishika kitabu cha ‘maombi ya Kushindana’ na kuomba na kwa kufanya hivyo, mambo huwa yanafanyika katika Ulimwengu wa Roho. Bidii ya mtu ndiyo itakayosababisha mtu  kutoka kwatika tatizo husika. Namna mtu binafsi  atakavyotia bidii, ndivyo ambavyo Mungu atamtoa katika hiyo hali. Biblia inasema ‘kila  amwendeaye Mungu huamini kuwa Mungu yupo, naye huwapa thawabu wote wamwitao’.

Comments