KANUNI ZAMATAYARISHO YA VIJINA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA!

Na  Mchungaji Peter Mitimingi ambaye pia ni mkurugezi wa huduma ya The Voice Hope Ministry (VHM)

Utangulizi:

1. Ndoa ni Kama Shamba.


Hakuna shamba ambalo huwa linaanza kulimwa pasipo kufanyiwa maandalizi. Ndoa ni jambo zito na gumu ambalo linahitaji sana maandalizi ya kina kabla ya mtu hajaingia.


2. Ndoa sio ya Kufanyia Majaribio.

Ndoa sio kitu cha kufanyia majaribio kama utaweza au utashindwa. Ndoa ni agano ambalo ukisha saini kuingia huwezi kutoka mpaka kifo kitakapo watengenisha.


3. Wachumba ni Kama Samaki Aliye Huru Baharini

Ni kama samaki baharini anakuwa na uhuru tu pale ambapo anakuwa hajanasa na kuingia kwenye nyavu. Akisha nasa na kuingia kwenye nyavu inakuwa ni vigumu sana kutoka kwenye nyavu na kurudi tena kwenye maji baharini.


4. Ukishaingia kwenye Ndoa Unakuwa Umeingia kwenye Nyavu

Kijana ambaye hajaoa wala kuolewa ni kama Yule samaki ambaye yupo majini baharini kabla hajaingia kwenye nyavu. Kabla hujaoa au kuolewa anao uhuru wa kuamua na kuchagua aina ya mtu ambaye ungependa kuwa mwenzi wako wa maisha yenu yote. Kuna mtu aliwahi kusema msemo wa kingereza ambao unafanana na maelezo niliyokuwa nayaelezea hapo juu kwamba “the best time to fire a person is before you hire” yaani muda muafaka wa kumfukuza mtu kazi ni kabla hujampa hiyo kazi yenyew

Comments