KRISMASI NA KUZALIWA KWA BWANA YESU KRISTO


 
BWANA YESU asifiwe.

Kama kuna tukio kubwa duniani basi ni kuja kwa ukombozi wa wanadamu wote. Mkombozi pekee ambaye anaweza kuwafanya wanadamu waende uzima wa milele ni BWANA YESU. Krismasi inatokana na neno la kiingeleza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani Misa au Ibada ya KRISTO. Wengine Christmas huita Noeli, ni sawa kabisa

Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka Lugha ya Kifaransa "noël". Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis " yaani (siku ya) kuzaliwa".
Warumi 14:5-6 ''Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa BWANA; naye alaye, hula kwa BWANA, kwa maana amshukuru MUNGU; tena asiyekula, hali kwa BWANA, naye pia amshukuru MUNGU.''

YESU Akikupenda Huwa Anakupenda Jumla Jumla. Alitupenda Zamani Ndio Maana Akajitoa Kufa Msalabani Ili Mimi Na Wewe Twende Uzima Wa Milele Bure, Cha Ajabu Kila Mtu Mara Baada Tu Ya Kumpokea YESU Huanza Kutengenezewa Makao Mbinguni, Hakuna Upendo Kama Huu. Wateule Wa MUNGU Tuliookoka Tunalindwa Na Damu Ya YESU. Huu Ni Upendo Mkuu Sana.



 Matukio yote yaliyomhusu BWANA YESU ni muhimu sana kwetu wanadamu. Katika Mathayo 26:6-13'' Naye YESU alipokuwapo Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma, mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia akaimimina kichwani pake alipoketi chakulani. Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakasema, Ni wa nini upotevu huu? Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini. YESU akatambua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi.
...............  Amin, nawaambieni, Kila patakapohubiriwa Injili hii katika ulimwengu wote, tendo hilo alilolitenda huyu litatajwa pia kwa kumbukumbu lake. ''
 
BWANA YESU alisema moja ya mambo ambayo yatakumbukwa wakati injili ikihubiriwa ni hili la kuoshwa miguu kwa nywele zilizopakwa mafuta ya thamani sana, hilo ni moja tu katika yale mengi ambayo tunayakumbuka. Tukio hilo litakumbukwa sana na kila itakakohubiriwa injili litasemwa, je tukio la kuzaliwa si zaidi? . Biblia haisemi kwamba YESU alizaliwa tarehe 25 December ila tukio la kuzaliwa kwake linabaki pale pale ndio maana liliandikwa. Katika Mathayo 28:20 BWANA YESU anasema kwamba atakuwa nasi siku zote Biblia inasema ‘’ na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. ‘’. Hapo BWANA YESU anasema kwamba atakuwa na sisi siku zote maana yake yupo pamoja na wateule wake jumatatu hadi jumapili ya kila wiki, tarehe 1 hadi taehe ya mwisho ya kila mwezi hata December 25 yupo pamoja nasi kama tu tukiitumia siku hiyo kwa kumtukuza yeye. Hakuna siku ya shetani hata moja  ila mwanadamu akiitumia siku yeyote kwa kumtumikia shetani hiyo itakuwa kwa uangamivu wake mwenyewe. Tunatakiwa Tuitumie Dec 25 kwa BWANA na sio kwa adui. Wapingakristo wengi hutaka kupinga kila jambo linalomhusu YESU KRISTO na husema kwamba hiyo siku ni ya shetani, wamempa shetani siku na wakati huo huo ipo siku Dec 25 itaangukia siku yao ya kuabudu, sasa sijui kama siku hiyo bado wataiita siku ya shetani. Mfano mwaka huu 2014 Sikukuu ya Krismasi itakuwa Alhamisi, Mwaka 2015 Krismasi itakuwa Siku ya ijumaa, Mwaka 2016 Krismasi itakuwa siku ya Jumamosi na Mwaka 2017 Sikukuu ya Krismasi itakuwa Jumapili. Mfano huu ambao nimeutaja unahusika na siku za kuabudu karibia dini na madhehebu yote hivyo siku yao ya ibada itakuwa pia ni siku ya Sikukuu ya Krismasi sana kwa leo wanasema hiyo ni siku ya shetani na siku ikiangukia siku yao takatifu ya ibada wataita sijui siku ya nini hata sijui.  Unaweza kujiuliza kwamba Hakuna popte kwenye Biblia panapoagiza kuadhimisha siku ya Uhuru wa nchi yetu wala hakuna agizo popote kwenye maandiko la kuadhimisha siku ya Wanawake duniani na hata sherehe za vijana wal;a wamama katika makanisa yetu haviko katika maagizo ya Biblia lakini sio dhambi hata kidogo kusherekea Ndugu zangu ukweli ni kwamba MUNGU hashughuliki na siku bali waabuduo halisi imewapasa kumwabudu BWANA MUNGU katika roho na kweli(Yohana 4:24). Hakuna dhambi kwenye siku mfano ona hapa MUNGU alisema kwamba anachukia sabato za waisraeli kwa sababu ya uovu wao, Tena MUNGU anachukia sikukuu za miandamo ya mwezi(Hosea 2:11, Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa. ). Hakuna dhambi kwenye siku ila dhambi iko kwenye matendo ya mtu katika siku yeyote. 

  Warumi 14:5-6 ‘’Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa BWANA; naye alaye, hula kwa BWANA, kwa maana amshukuru MUNGU; tena asiyekula, hali kwa BWANA, naye pia amshukuru MUNGU. ‘’. Hapo ndipo tunapata uhakika kwamba hakuna dhambi kwenye siku. Ni Jambo  zuri kuiadhimisha siku kwa BWANA. Dec 25 kila mwaka Wakristo kote duniani huiadhimisha siku hiyo kwa BWANA kwa kukumbuka kuja kwa ukombozi duniani. Kama kuna anayeitumia siku hiyo vibaya ni kwa uangamivu wake mwenyewe. Hakuna andiko linalokataza watu kumtukuza MUNGU tarehe 25 December. Hakuna ajuaye siku kamili ya Kuzaliwa BWANA YESU kama ambavyo hakuna anayejua siku kamili ya BWANA YESU kurudi mara ya pili lakini matukio yote mawili ni halisi katika Biblia. 

Kuna watu hujaribu kukadilia siku ya kuzaliwa kwa BWANA YESU lakini kwa kukosea, Hakuna Dhambi Kwenye Siku Ila Dhambi Iko Kwenye Matendo Ya Mtu Anayoyafanya Siku Yeyote Katika Juma. Biblia Haijasema Kwamba YESU Alizaliwa Tarehe 25 Decemba Ila Hakuna Dhambi Kwenye Kuadhimisha Siku Hiyo (Warumi 14:5-6), Mwezi Wa 6 Malaika Gabriel Alimtokea Mariam, Mwezi Huo Wa Sita Haujulikani Kama Ni Mwezi Wa 6 Wa Mwaka Au Kama Ni Mwezi Wa 6 Wa Mimba Ya Elizabeth Maana Malaika Huyo Huyo Miezi 6 Kabla Alimtokea Zakaria Mme Wa Elizabeth  Luka 1:19( Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za MUNGU; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. ) Na Luka 1:36 ( Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; ), Na Mara Baada Ya Mariamu Kutokewa Na Malaika Alienda Kwa Elizabeth Kukaa Miezi 3  Luka 1:56 (Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake. ) , Hapo Bado Hatuambiwi Kwamba Mariamu Alikuwa Mimba, Mimba Ya Mariam Inakuja Kugundulika Kipindi Yusufu Anataka Kumwacha  Na hatujui kwamba ulipita muda gani wala miezi mingapi tangu Malaika amtokee Mariam Mathayo 1:18-25 '' Kuzaliwa kwake YESU KRISTO kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa ROHO MTAKATIFU. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa BWANA alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa ROHO MTAKATIFU. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake YESU, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na BWANA kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, MUNGU pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa BWANA alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU. ''
Baada Ya Malaika kumtokea Mariam Hatuambiwi Lolote Hadi Mimba Ilipotimiza Miezi 9 Wakati Wa Kuzaliwa   Hivyo Mwezi Wa 6 Tunaoutaka Sisi Hapo Haupo. Jambo Jingine Christmas Maana Yake Ni Kusanyiko La KRISTO Lakini Wapingakristo Waliondoa Christ Na Kuweka X Ni Kwa Hila Tu. Ndio maana wamewashawishi watu wote kuandika X-mass wakimaanisha Christmas.
 

Tukio la Kuzaliwa kwa YESU KRISTO nimelifafanua na sasa nataka niseme kile ambacho ROHO MTAKATIFU alisema kupitia manabii zamani za kale kuhusu kuja kwa BWANA YESU.


= Yakobo katika Mwanzo 49:10 alisema yafuatayo ‘’ Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii. ‘’ na ni kweli jambo hilo lilitimizwa katika Luka 1:32-33 ‘’ Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana MUNGU atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. ‘’


= MUNGU kupitia Musa alisema yafuatayo kuhusu YESU KRISTO Kumb 18:18 ‘’ Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. ‘’ andiko hilo linatimizwa wakati ambao BWANA YESU alitokea Duniani Yohana 1:45-51 ‘’ Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, YESU, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Basi YESU akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? YESU akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa MUNGU, ndiwe Mfalme wa Israeli. YESUakajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa MUNGU wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu. ‘’ Pia Kumb 18:18 imesema kwamba  MUNGU ataweka neno lake ndani ya Mwanaye YESU KRISTO na hiyo ilitimizwa katika Yohana 12:49-50 ‘’Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali BABA aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema. Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama BABA alivyoniambia, ndivyo ninenavyo. ‘’ pia Yohana 17:8  inathibitisha, Biblia inasema ‘’Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. ‘’


= Katika Isaya Roho wa MUNGU alisema kwamba Isaya ‘’  Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;  na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. -Isaya 11:1-4  ‘’


= MUNGU alisema pia kupitia Yeremia kwamba ‘’   Tazama siku zinakuja, asema BWANA, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, BWANA ni haki yetu-Yeremia 23:5-6‘’


=ROHO MTAKATIFU pia alisema kwa njia ya ufunuo kwa anabii Danieli kwamba ‘’ Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake MASIHI aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu-Danieli 9:24-26‘’


=Pia ROHO MTAKATIFU alisema kupitia Nabii Mika kuhusu umilele wa YESU na hata eneo ambalo atazaliwa, Biblia inasema Mika 5:2-4 ‘’Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.  Kwa sababu hiyo atawatoa, hata wakati wa kuzaa kwake aliye na utungu; ndipo hayo mabaki ya nduguze watawarudia wana wa Israeli. Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, MUNGU wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hata miisho ya dunia. ‘’.


Tukio la kuja kwa BWANA YESU ni tukio la kuja kwa uzima kwetu. Hakuna uzima wa milele kwingine popote pale nje  na BWANA YESU(Yohana 14:6, Matendo 4:12)

Tunapokumbuka kuzaliwa kwa BWANA YESU tunakuwa tunakumbuka jambo kubwa sana la uzima wetu.

YESU alileta uzima wa milele kwa kila binadamu ambaye atampokea kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yake na akidumu katika yeye ni furaha ya milele.

YESU Akikupenda Huwa Anakupenda Jumla Jumla. Alitupenda Zamani Ndio Maana Akajitoa Kufa Msalabani Ili Mimi Na Wewe Twende Uzima Wa Milele Bure, Cha Ajabu Kila Mtu Mara Baada Tu Ya Kumpokea YESU Huanza Kutengenezewa Makao Mbinguni, Hakuna Upendo Kama Huu. Wateule Wa MUNGU Tunalindwa Na Damu Ya YESU. Huu Ni Upendo Mkuu Sana.
 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

Comments