KUZALIWA KWA YESU

Na Askofu Zakaria Kakobe.


SOMO:  KUZALIWA KWA YESU

Kwa kuwa leo ni siku nzuri ya Krisimasi, ni vizuri kuchukua muda kutafakari juu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa kwa ajabu na kwa kipekee mno.Tunajifunza mengi mno tunapotafakari juu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Tutaligawa somo letu leo katika vipengele sita.
( 1 ). Utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu                      
( 2 ). Jinsi Yesu alivyozaliwa
( 3 ). Jinsi Herode alivyoitafuta roho ya mtoto
( 4 ). Jinsi ya kushinda dhambi kama Yesu
( 5 ). Faida ya kuzaliwa mara ya pili
( 1 ). Utabiri wa kuzaliwa kwa Yesu.
Kuzaliwa kwa  Yesu  Kristo  kulitabiriwa na Nabii Isaya miaka zaidi ya 700 kabla ( Isaya 7:14; 9:6 ).Utabiri huu katika maandiko, ulitimizwa kama yalivyonena maandiko. Mahali hapa tunajifunza mambo yafuatayo:-
1.  Kila Neno la Mungu limehekikishwa ( Mithali 30:5-6 )
2.  Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno ya Mungu hayatapita kamwe, lazima yatatimizwa ( Luka 21:33 )
Neno hili la Mungu linazungumza kwamba wenye dhambi wote, hawataurithi ufalme wa Mungu bali watatupwa katika ziwa liwakalo moto na kiberiti. Neno hili ni kweli, utabiri huu ni kweli utatimizwa kwa wote wenye dhambi. Utabiri katika Neno la Mungu pia unasema Yesu ataruudi tena kuwachukua walio wale( Yohana
) 14:1-3 .neno hili hakika litatimi .
( 2 ). Jinsi yesu alivyo zaliwa
.       Yesu Kristo alizaliwa kutokana na mimba iliyopatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mimba hiyo-haikutungwa kutokana na mbegu ya mwanadamu iharibikayo bali ile isiyoharibika ya Roho Mtakatifu (Mathayo 1:18-20).Hakuna yeyote kabla na baada ya Yesu,aliyezaliwa kwa njia hii ya ajabu.Yesu aliyezaliwa kwa njia hii ndiye pekee aliyejaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote,bila kutenda dhambi katika maisha yake yote (Waebrania 4:15).
Sisi nasi tukitaka kushinda dhambi hatuna budi kuzaliwa kwa roho,yaani kuzaliwa mara ya pili .katika       (Mathayo 2:4-6;  Luka 2:6-7),tunaona kawa Yesu Kristo alizaliwa katika kijiji kidogo sana cha Bethlehemu na kulazwa katika hori ya kulia ng’ombe mahali hapa pia tunajifunza juu ya mpango wa Mungu kwetu.Huduma kubwa sana na mambo makubwa sana huanzia katika unyenyekevu na kukubali kushughulishwa na mambo manyonge (Yakobo 4:6,warumi 12:16). Kuzaliiwa kwake kuliambatana na kupewa tunu au zawadi, dhahabuna uvuumba na manema ne.Tunapewa zawadi kubwa sana tunapokuwa tumezaliwa mara ya pili kwa jinsi ambavyo tunavyokuwa na ushindi juu ya shetani na kupewa ufallme na ukuhani.
Katika (Mathayo 2:1-11) tunaona kwamba Mamajusi wa mashariki walikwenda kumsujudia Yesu. Neno ‘mama jusi”linatokana na neno la kiyunani “Magoi” au ‘Magi” ambalo linatupa nenola kingereza ‘magician’ au “wachawi” mamajisi walikuwa wachawi (Danieli 2:2). Wachawi hawa walitoka mbali mashariki kulikojaa upagani,kuja kumsujudia Yesu tangu katika utoto wake, kuonyesha jiinsi shetani asivyo na chochote mbele ya Yesu Kristo.
( 3 ). Jinsi herode alivyo  itafuta roho ya mtoto mathayo 2:13-21.
Herode alitafuta kuiua roho ya mtoto Yesu bali wazazi wake walimficha walipokimbilia Misri .Baada ya kuzaliwa mara ya pili,ni muuhimu sana kufichwa na wazazi yaani walimu wetu ili shetania asituuangamize katika utoto wetu.
(4)Jinsi ya kushinda dhambi kama yesu.
Hakuna namna nyingine ya kushinda dhambi ila kuzaliwa kama alivyozaliiwa Yesu. Ni lazima tuzaliwe mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika (Waebrania 4:15; Yohana 3:3;   1Petro 1:23). Ili tusherehekee vizuri kuzaliwa kwa Yesu leo ni muhimu kuona kwamba tumezaliwa mara ya pili.
(5). Jinsi ya kuzaliwa mara ya pili
1.Kuungama na kuacha dhambi (Mithali 28:13).
2.Kuamini katika damu ya Yesu isafiishayo dhambi (1Yohana 1:6-9).
3.Kumpokea  Yesu na kumkubali awe dereva wetu, Bwana wetu na Mwokozi wetu (Yohana1:12; Walawi 26:13; Warumi 10:9).
(6). Faida ya kuzaliwa mara ya pili
Leo ,ingawa tunasherekea Krismasi, Yesu hakuzaliwa leo alizaliwa miaka mingi iliyopita akaishi duniani na kupaa mbinguni. Sisi nasi tukizaliwa mara ya pili mwishoni mwa safari yetu duniani itakuwa kuwepo pale alipo Yesu yaani mbinguno (Yohana 14:3). Baada ya kuichukua sura yake Yesu kwa kuzaliwa mara ya pili na kuuvua utu wa kale ule wa asili, ndipo tutakapokuwa na uhakika wa kukaa na Yesu milele (1Wakoritho 15:45-49).Hatupaswi  kukosa faiida hii ya kuzaliwa mara ya pili, kukosa faida hii ni kusherekea krismasi bila faida yoyote.
SIFA YA KUTUWEZESHA  KUINGIA MBINGUNI
Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!
                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 
                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         
Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.
                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Fatilia Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        
Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org
Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries
Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

Comments