MAADUI WAKIPANGA VITA YA KIMWILI WEWE PANGA VITA YA KIROHO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze mambo muhimu.
Tunawashinda shetani na watoto wake kwa damu ya YESU KRISTO, Biblia inasema '' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao-Ufunuo 12:11a''
Siku moja mwaka 2012 tulikuwa kwenye maombi kanisani kwetu PAG Chukwani Zanzibar, Namshukuru MUNGU kwa ajili ya siku hiyo maana wakati maombi yakiendelea nilikuwa nikiona live vitu vingi sana, Niliona mambo ambayo MUNGU angelitendea kanisa, ni baraka sana, niliona jinsi ambavyo, kuna mtoto mmoja ambaye kila siku alikuwa anahudhuria maombi hayo ya mkesha, niliona baraka za MUNGU za ajabu juu ya maisha yake. ghafla katika kuona huko nilisikia sauti ya kunitisha ikisema ''Tutalipiza tu na lazima tuanze na wewe'' yaani mimi, nilipotazama kwa kina sehemu ambamo inatokea sauti, maana kwangu usiku ule na giza lile nilikuwa naona kama mchana kwa neema ya MUNGU, niliona kama upepo wa kisulisuli na katikati ya upepo huo kulikuwa na kama kiumbe hai maana niliona mfano wa kiumbe hai, niliona jicho na kama ka mwili ka kiaina. Nilianza kuingiwa na hofu na hofu ilipozidi hata kule kuona kwa jinsi ya rohoni kukakata, tuliendelea na maombi lakini nusu naogopa nusu hofu. baada ya kumaliza maombi niliwaambia wenzangu kile ambacho niliona, Mchungaji alisema nisihofu maana majini kazi yao ni kutisha wateule wa BWANA lakini hayana lolote. baada ya kuondoka kanisani, kuelekea nyumbani  yaani kule nilikokuwa nimepanga chumba, Hofu ilikuwa ndani yangu, nilikemea sana lakini nikiwaza tu naogopa, nilipokaribia kufika nyumbani nilisikia kelele za bundi, na kweli kwenye nguzo ya umeme jirani kabisa na chumba changu niliona bundi wanne wakiwa wanazozana, nilijitia nguvu na kuchukua jiwe na kuwaponda wale bundi huku nikitamka '' Jiwe hili naligeuza moto wa kuunguza adui kama vile ambavyo Daudi alimuua Goliathi kwa jiwe dogo''. walikimbia na nikaingia ndani kulala, nililala lakini kwa tahadhari kubwa. Kesho yake nilikuwa sawa lakini nikikumbuka vitisho vya zile nguvu za giza naogoapa tena, baadae nilipata ufunuo muhimu sana ambao ni uhakika wa uzima, ni jawabu la kukaa salama.''BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani? Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba. - Zaburi27:1,5''
Nilipata jibu sahihi maana licha ya kuyajua maandiko mengi lakini wakati wa tatizi maandiko hata sikuyakumbuka, yaani yakikuwa kama yameyeyuka kichwani mwangu. Hofu ni mbaya  na uoga ni machukizo mbele ya MUNGU.
Ndugu yangu najua kabisa umewahi kupitia kwenye vitisho vingi kutoka kwa maadui, na yawezekana kabisa kwa sasa unapitia kwenye vitisho vingi sana kutoka kwa wachawi au watu au majini. Lakini napenda kukuambia kwamba msaada upo tena ni msaada wa uzima wa roho na mwili. Msaada ni YESU KRISTO pekee.
MUNGU anasema  ''Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya. -Mithali 1:33''
Jambo kubwa ni kumsikila na kumtii MUNGU, Kumtii MUNGU -jambo la kwanza ni kuokoka, 
-jambo la pili ni kuishi maisha matakatifu 
-na jambo la tatu ni kuomba kwake lolote ambalo linakutatiza au kukutisha.  
Mteule mmoja anasema ''Nalimtafuta BWANA akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote. -Zaburi 34:4''

 Ndugu yangu mtafute tu BWANA kwa maombi na utakaa salama.

''usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. -Isaya 41:10''
 -Maadui zako Wakipanga Vita Ya Kimwili Wewe Panga Ya Kiroho. 
-Wakitumia Kafara Ya Kuku Ili Laana Na Mikosi Vikupate Wewe Tumia Damu Ya YESU Na Jina La YESU KRISTO Ukifuta Laana Zao Na Amuru Laana Hiyo Iwarudie Wao. Utashangaa Badala Ya Wewe Kuwa Maskini Wao Ndo Umaskini Walioutamka Utawakamata. Wakikutamkia Magonjwa Mwite BWANA YESU Utashangaa Kwa Kuwaona Watu Wabaya Hao Wakipanga Foleni Hospitalini Kila Siku. Ni Heri Kumpata YESU KRISTO Maana Yeye Habadiliki Wala Habahatishi.

 ''Lakini BWANA Yu Pamoja Nami, Mfano Wa Shujaa Mwenye Kutisha; Kwa Hiyo Hao Wanaonionea Watajikwaa, Wala Hawatashinda; Watatahayarika Sana. Kwa Sababu Hawakutenda Kwa Akili, Wataona Aibu Ya Milele Ambayo Haitasaulika Kamwe-Yeremia 20:11.''

Sisi Wateule Tumekombolewa Kwa Damu Ya YESU, Hata Wachawi Wanune, Hata Majini Wakunje Uso Hawatatupata Kwa Jina La YESU KRISTO. Biblia Inasema Uhai Wetu Umefichwa Katika MUNGU Kupitia YESU KRISTO. Wakolosai 3:3b ''na uhai wenu umefichwa pamoja na KRISTO katika MUNGU.'' 
Tunaye YESU Tena Tumehakikisha Ni Kamanda Wetu Ndio Maana Tunashinda Vita. 
 ''Maana MUNGU hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. -2 Timotheo 1:7''

Kataa uoga na hofu, Mwamini MUNGU utakaa salama.

''Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA MUNGU wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.-Kumb 20:1''

Asante BWANA YESU Kwa Wema Wako Kwa Kuja Kutuokoa. 
 ''Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.-1 Yohana 5:4''
Tunamshinda shetani na watoto wake kwa MAOMBI na maombi sahihi ni maombi ya IMANI, Na Imani yetu kama iko bila matendo imekufa. Imani na utakatifu na maombi ya nguvu hakika ushindi ni lazima.
Ndugu kama uko nje na BWANA YESU huwezi kuomba harafu MUNGU akakusikia, ingia kwanza ndani ya YESU ndipo utapokelewa na MUNGU na maombi yako yatakuwa yanapokelewa siku zote. 
  Ukiwa Nje Na Wokovu Wa BWANA YESU Tambua Tu Kwamba Unauona Uzima Wa Milele Ila Hutaki Kuufuata.
 YESU KRISTO ni muhimu kuliko vyote.
KATAA MAGONJWA NA KILA MPANGO WA SHETANI JUU YA MAISHA YAKO KWA KUOMBA MAOMBI HAYA. Ninaamuru kwa jina la YESU KRISTO kwamba bakteria, virusi na viumbe vyote wa magonjwa hamna uwezo juu yangu kwa jina la YESU KRISTO. Hamna mamlaka juu ya Tanzania. Ninawatiisha viumbe wote wanaoonekana na wasioonekana wasababishao magonjwa kwa jina la YESU, hamtaingia ndani ya Tanzania kwa jina la YESU KRISTO. Kwa mamlaka niliyonayo ninawafunga virusi wote wa mafua ya ndege, virusi wa mafua ya nguruwe, ebola nje ya Tanzania kwa damu ya YESU KRISTO. Kemikali zote, bakteria, protozoa wote ninawatiisha kwa damu ya YESU KRISTO. Kwa mamlaka ya damu ya mwanakondoo, viumbe wote wa magonjwa ninaupiga ule uweza uliowekwa ndani yenu juu ya Tanzania, juu ya Afrika, juu ya maisha yangu, juu ya familia yangu; ninaamuru kuanzia sasa hamtaingia ndani ya nchi ya Tanzania kwa jina la YESU KRISTO.Ninavimiliki na kuvitiisha viumbe vyote vinavyokaa kwenye anga, bahari, na nchi. Mimi ni mtawala wenu, hamna mamlaka ya kunitawala haikuwa hivyo tangu zamani. Ninawaseta mrudi kuzimu mlikotoka kwa jina la YESU KRISTO. Ninaamuru kuanzia sasa hamtanidhuru kwa damu ya YESU KRISTO. Viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekana hamna uwezo wa kunitawala kwa jina la Yesu KRISTO. Ninabeba mamlaka kama mtawala, ninawateketeza na uwezo wenu wa kudhuru kwa damu ya mwanakondoo. Nimepewa amri juu ya pepo wachafu na viumbe vyote, ninaangamiza kila nguvu iliyo juu yenu ninyi viumbe wa kishetani na kichawi na waganga wa kienyeji, ninawakausha kwa damu ya YESU KRISTO. Niwaondolea ule uwezo wa kuidhuru Tanzania kwa mamlaka ya damu ya mwanakondoo. Ninaiachilia damu ya mwanakondoo kwenye mipaka yote ya Tanzania, damu inenayo mema, ninainyunyizia kwenye mipaka yote ya Taifa la Tanzania na juu ya watu wake wote. Iwalinde dhidi ya magonjwa yote kwa jina la YESU KRISTO. Kwa mamlaka ya Jina la YESU KRISTO ninatawala viumbe vvyote vilivyomo baharini, angani na kwenye nchi kwa damu ya YESU. Ninatawala uchumi wa nchi, utajiri wa nchi; ninautawala kwa jina la YESU KRISTO. Ninatawala kwa jina la YESU KRISTO, ninatawala na kuvitiisha viumbe vyote vya magonjwa kwa jina la YESU KRISTO. AMEN!

Make Money at : http://bit.ly/copy_wi

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments