MAKANISA SABA.Ufunuo 2&3 * sehemu ya mwisho *

Bwana Yesu asifiwe…
Ninakukaribisha katika uchambuzi wa makanisa saba ikiwa leo ni siku ya tano ya uchambuzi huu. Ukweli ni kwamba ninachambua kwa ufupi kwa kila kanisa,maana nikisema nikuandikie yote,basi ni dhahili fundisho hili la makanisa yale saba litakuwa ni fundisho lefu kuliko mafundisho yote niliyopata kuandika. Lakini pia zipo jumbe nyingi sana katika kila moja ya barua kwa kanisa kama ilivyoandikwa katika Ufunuo 2&3.
Siku ya leo tutamaliza ufafanuzi wote kwa kuyaangalia kwa kifupi juu ya makanisa matatu ya yaliyobakia,ambayo ni; ◇Kanisa la Laodikia. ◇Kanisa la Efeso. ◇Kanisa la Smirna.
Camera360_2014_10_1_112833_jpg
Kanisa la Laodikia.
[V] KANISA LA LAODIKIA. ~ Laodikia ilikuwa kama kilomita sabini kusini mashariki mwa Filadelfia. ~ Inasemekana mji uligunduliwa na mfalme Antiochus II Theos(261-246 BCE).Mfalme huyu akauita jina la mji huu Laodoce jina la mke wake. ~ Mji huu ulikuwa ni tajiri. ~ Mji huu ulikuwa maarufu kwa ustawi wake na ulikuwa na shule maarufu ya UTABIBU. ~ Mahali hapa palisifika na kuwa na manyoya mazuri,lakini pia kulikuwa na dawa ya macho maarufu ulimwenguni. ~ Kanisa hili halipo hai hivi sasa,na limebakia magofu tu.
▪ Barua kwa kanisa la Laodikia imeandikwa katika Ufunuo 3:14-22 Na hapa tunasoma mstari mmoja tu;
 “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. ” Ufunuo 3:18
Bwana Yesu anatuonesha utoshelevu wake,anamwambia Laodikia atafute utajiri wa kweli ndani yake Bwana Yesu pia Laodikia wapate kuona sawa sawa,maana walidhani wana dawa nzuri ya macho ingawa walikuwa bado ni vipofu-Yesu pekee ndie dawa ya kufungua waliofungwa na kwa walioonewa na ibilisi. ( Ufunuo 3:20)Laodikia,amepewa nafasi ya kufungua mlango ili Bwana aingie,Laodikia wa leo ni wewe,tazama-Bwana anabisha ukisikia na kufungua yeye ataingia ndani ya moyo wako. Bwana Yesu anakutazamia uokoke,aingie ndani yako uwe kiumbe kipya.
Camera360_2014_10_2_031134_jpg
Efeso hiyo.
[VII] KANISA LA EFESO. ~Efeso ulikuwa ni mji mkubwa na tajiri sana katika ulimwengu wa zamani ~Kulikuwa na bandari juu ya Asia ndogo,hivyo Efeso ulikuwa ni makao ya biashara na usafiri. ~Hapa ndipo palipokuwa na hekalu kubwa la Artemi pia Artemi alijulikana kama Diana. Artemi alikuwa mungu wa uzazi,hivyo aliabudiwa sana. ~ Mji ukawa maarufu hata kwa biashara,(Matendo 19:23-24) & Matendo 19:34.
 
~ Leo,kanisa hili limebaki magofu,pia ndipo pana eneo kubwa sana kuliko maeneo ya makanisa yote sita. ~ Pana eneo la michozo la kizamani.
Camera360_2014_10_2_035348_jpg
@ Mtumishi Gasper Madumla,akieleza jambo katika kanisa la Efeso.
▪ Zipo sifa kama tatu hivi,zinazopatikana Efeso,nazo ni; ◇Palikuwa na miungu mingi iliyokuwa ikiabudiwa.mfano palikuwa na mungu wa uzazi Diana au Artemi. mungu huyu alikuwa na matiti mengi. ◇Paulo alifika mahali hapa na kuhudumu takribani muda wa miaka miwili. ◇ Baada ya kifo cha Bwana Yesu,mama yake Yesu alikimbizwa Efeso na kufichwa huko na mwanaye Yohana.(Yoh.19:25-27) kabla ya kurudishwa Yerusalemu tena.
Bwana Yesu analisifu kanisa hili kwamba katikati ya miungu na mchanganyiko wa mafundisho ya uongo,lenyewe bado lilikuwa na subira kwa Bwana(Ufunuo 2:3) ~Subira ni jambo la msingi sana katika maisha ya mkristo. Wengi siku ya leo wamekosa subira maana hata kuomba kwao wanataraji kujibiwa papo hapo. Mpendwa kuwa na subira kwa Bwana,Yeye MUNGU ni mwaminifu hawai wala hachelewi.
[VII] KANISA LA SMIRNA. ~Hili ndilo kanisa la pekee lililobaki hai mpaka leo. Makanisa sita hayaendelei na ibada zao,lakini kanisa hili linaendelea na ibada zake.Hivyo ni kanisa moja la kipekee kabisa tofauti na yale saba. ~Smirna sasa ni Izmir,ulikuwa ni kilomita hamsini kaskazini mwa Efeso.
~Lakini pia Smirna ulijulikana kwa ibada za kipagani,ingawa barua ya kanisa hili imewaja na faraja. Hivi sasa,watu waendao kujifunza habari za mkanisa,hupitia kufanya ibada mahali hapa. ~Kanisa hili lipo chini ya Warumi.
 
Jambo moja kubwa na la msingi ambalo Bwana Yesu anawaambia watu wa kanisa la Smirna ni; ◇ Wasiogope majaribu,bali wawe waaminifu hata kufa.
” Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa 3na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima. “Ufunuo 2:10
Bwana Yesu leo anasema na wewe maneno hayo hayo,kwamba majaribu hayana budi kuja kwako,lakini usiogope kupitishwa majaribuni maana ndipo mahali pekee pa kupanda ngazi kiroho . Lakini uwe MWAMINIFU HATA KUFA,yaani pale inapobidi kufa kwa uaminifu basi ni bora kufa kuliko kumkosa Bwana Yesu mwenye mbingu. Hapa,panatutaka hata kupoteza mali na pesa kwa ajili ya uzuri wa Bwana MUNGU.
Na Mtumishi Gasper Madumla
▪ Kwa huduma ya maombi na maombezi usisite kunipigia kwa namba yangu hii; 0655-111149.
@ Mtumishi Gasper Madumla.
MWISHO.
UBARIKIWE.

Comments