MJI WA UHARIBIFU

Mchungaji Adriano Makazi akimwabudu na Kumshukuru Bwana
katika ibada - Bonde la Maono - Ufufuo na Uzima Morogoro.

Utangulizi: Somo la leo linaitwa Mji wa Uharibifu”. Ni vizuri kufahamu kuwa ipo miji ya uharibifu ambapo wachawi, waganga wa kienyeji, washirikina, wasoma-nyota, wapigaramli na washirika wao wote hukaa humo. Leo tutaenda kuibomoa miji  hii  kwa Jina la Yesu.

ISAYA 19:18…[Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.]…Tunapoongelea Misri tunaizungumzia Afrika. Maana ya miji  mitano katika Misri ni  kuwa itakuwepo miji mitano Barani Afrika. Biblia inasema kuwa katika hiyo  miji mitano, mmoja utakuwa ni mji  wa uharibifu. Kwa nini uwepo mji wa aina hii?  Kwa  sababu shetani hapendi kuona mambo mema yakifanyika, na katikati ya mema shetani hupenyeza uharibifu. Kumbuka hata katika mitume 12 wa Yesu Kristo, shetani alijipenyeza na kumuingia mmoja wao aitwae Yuda Iskariote ili kuleta uharibifu.

Katika Biblia Misri ilibarikiwa na kuwa kama kimbilio la watu kwenda nyakati za shida na njaa.  Tunamuona Ibrahimu alikimbilia Misri njaa ilipozidi,  na hata mwanae Isaka alifanya vivyo hivyo. Watoto wa Isaka vivyo hivyo, njaa ilipowapata,walikimbilia Misri  na kumkuta Yusufu ndugu yao akiwa amefanywa Waziri Mkuu wa Misri. Kwa hiyo basi, mataifa yanaonekana yakija Afrika kupata chakula.  Misri  imebarikiwa hivyo kwa kitendo cha kuwapokea Wayahudi (Israel).  Yesu Kristo akiwa kabla ya kusulubiwa Golgotha,  alipokelewa msalaba wake na Simoni wa Kirene (ambaye ni kutoka Afrika) kudhihirisha kuwa Afrika ndiko ambapo moto wa Injili utatokea nyakati hizi za mwisho na kufanya mataifa yote duniani kuwa falme za mwanakondoo.

Platform wa Bonde la Maono Morogoro wakimsifu na kuwimbia Bwana wakati wa ibada

Sehemu nyingine mji huu unaitwa’Mji wa Ghasia” (ISAYA 22:2…[Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha;  Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga,  Wala hawakufa vitani.])… Unapoona ghasia zinatokea bungeni au katika mita yetu ujue zinatokea kule. Sehemu nyingine uniatwa mji wa machafuko (ISAYA 24:10…[Mji wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote.])… Yanapotokea machafuko  ya ndoa,  machafuko makazini,  ujjue yote huanmzai hapo.  Na zipo nyumba katika  huumji,  na wachawi hutumia aina hizi za nyumba zishikilie watu. Unaweza kumuona mtu katika mwili lakini kumbe anakuwepo mara mbili.  Kila mji unaouona unakuwa na uongozi wake (wakuu wa kuutawala mji) ambao huzuia vinavyoingia ndani ya mji,kama ambavyo Dnieli alizuia na Mfalme wa Anga la Uajemi ili majibu yake yasimjie Danieli.

Mungu anapenda sisi tuombe ili  kupata majibu  ya kile tunachomuomba kama  katika MATHAYO 7:7. Hata hivyo wapo mashetani wakaao katika miji ya uharibifu ambao huzuia majibu ya maombi yetu.  Tangia siku ya  kwanza ulipoanza kuomba  hitaji  lako, Bwana ameshakujibu lakini wenyeji  wa miji  ya uharibifu huyazuia hayo majibu ili yakufikie ukiwa tayari mzee wa miaka 80. Yakija katika muda huo,  majibu ya aina hii yanakosa maana.  Leo kila mmoja adhamirie kuibomoa hii miji kwa Jina la Yesu ili tupate majibu yetu kwa wakati wa Bwana.

Kimsingi wachawi huwa hawana sababu ya maana ya kumsababishia mtu matatizo. Watu wa aina hii huweka ‘vikao vya uharibifu’ na kupanga namna ya kukuangamiza. Hawa hujifungia ndani ili kutengeneza mango wa maangamizi.  Mara nyingi watu wa aina hii  huwa ndugu wa karibu au wa ofisi makazini. Ndiyo maana Biblia husema Adui wa mtu ni  wale wa nyumbani mwake.

2 WAFALME 6:8…[Basi, mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema, Kituo changu kitakuwapo mahali Fulani]…  Ujue hata wewe kuna mtu/watu wanafanya vita na biashara yako.  Kuna watu wanapanga ajali kwa ajili  yako ingawa hujui. Si vizuri kwenda kwa mazoea. Haujui adui wakoamepanga aina gani ya vita dhidi yako. Kuna watu  wanapanga kituo cha watu wengine kwa maisha yao.

MAOMBI
Kila aliyepenga shauri juu ya ndoa yangu, au juu ya watoto wangu, Bwana auoyooshe mkono wake kinyume nao,  ili mashauri yao yawarudie wao  wenyewe kwa Jina la Yesu. Amen 


2 WAFALME 6:9..[Yule mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite mahali fulani;   kwa sababu ndiko wanakoshukia Washami.]… Shetani amejipanga lakini hata Yesu Kristo naye amejipanga kwa ajili yako. Kuna wakati  wa kujihadhari. Si vyema kwenda bila hadhari.

MAOMBI:
Naagiza mtego wa ajili waliokutegea uwanase wenyewe kwa Jina la Yesu. Mungu na akuokoe na mtego wa wawindaji kwa Jina la Yesu kwa sababu Yesu Kristo ameshinda vita na kuzimu.  Amen


2 WAFALME 6:10...[Mfalme wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu, na kuhadharishwa;  akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si mara mbili. 11 Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?]… Unapoambiwa jambo hukimbilii tu. Kwa niniMfalme wa Shamu afadhaike? Ni kwa sababu  kituo alichopanga uharibiifu hakikutokea,  zaidi ya  mara tatu. Alipanga magonjwa,  akaugua mwanae wa kwanza akafa. Alipanga ajali, badala yake ajali ikatokea nyumbani kwake mwenyewe. Na iwe hivyo hivyo kwa Yule ndugu yako aliyepanga mabaya kwako, yamrudie yeye na familiayake na wafadhaike  kwa Jina la Yesu. Tunaye Roho Mtakatifu wa kutujulisha mambo yote ya sirini yaliyopndwa juu yetu kwa Jina la Yesu.

Platforms wakiongoza Majeshi ya Bwana katika Sifa na Kubadu Bonde la Maono -Morogoro

Mungu amemficha mwanadamu ili asiyaone baadhi ya mambo yaliyopangwa maishani mwake. Laiti mtu angejua mambo /matukio ambayo yalikuwa yatokee kwake kila siku maishani mwake na ambayo  Bwana anamuepusha, angepiga magoti na kumshukuru Mungu kusema 'asante’.  Tazama Bwana amekuwezesha kwa miezi yote ya mwaka kuishi vizuri,  na kukuepusha na mabaya yaliyopangwa kukupata kipindi hicho. Mwezi wa Desemba ni mwezi wa kumpa Bwana shukurani kwa ukarimu ambao  Bwana ameufanya katika maisha yako. Lazima uwe na moyo wa shukrani. Muombe Mungu  ili mwaka 2015 uwe ni "mwaka wa kutiisha, kumiliki na kutawala" kwa Jina la Yesu.

Majeshi ya Bwana Bonde la Maono Morogoro wakifuatilia  kwa makini somo "Mji wa Uharibifu"

Huu ni wakati wa kumpa sifa Bwana kwa matendo makuu aliyofanya maishani  mwetu. Daudi alisema ni ‘heri kuwa nyumbani  mwa Bwana kuliko miaka  elfu moja kwenye karamu za  waovu’. Mungu  aliweka siku moja tu  ya saa 12 kwa ajili ya kumwabudu.  Ni vizuri kuja nyumbani kwake, na kusogeza mioyo ya shukrani kwake.

Comments