MKESHA WA KULIOMBEA TAIFA KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA TAREHE 31 DEC 2014.


ASKOFU Godfrey Mallassy wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC), amesema wasingependa kuona machafuko ambayo yatasababisha kutoweka kwa amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa. Pia alisema kipindi cha kuelekea kuchagua katiba mpya na uchaguzi mkuu pia kuna kila sababu ya kila mwananchi kuhakikisha anailinda amani ya nchi iliyodumu kwa muda mrefu. Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa mkesha mkubwa wa kitaifa, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alisema maandalizi yote yamekamilika hivyo aliwaomba watanzania kufika kwa wingi kwa ajili ya dua hilo ambalo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka.
 
Mwenyekiti wa Mkesha Mkuu wa Kuliombea Taifa (Dua maalumu), Askofu Godfrey Mallassy (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkesha huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Desemba 31 mwaka huu. Kulia ni Askofu William Mwamalanga wa Kanisa la Kiinjili la Kipentecoste Tanzania.

 Alisema hakuna taifa lolote duniani ambalo linapenda kupoteza amani yake kwani amani ni mfano wa yai ambalo kama likianguka na kupasuka haliwezi kurudi tena. Pia alitumia fursa hiyo hiyo kuwaasa waandishi wa habari kuandika habari za usawa na kuacha kuandika habari za kupotosha jamii kwani kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha nchi. "Tunaenda kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 na kuchagaua katiba mpya hivyo basi ni vyema kuandika habari za ukweli na si za uchochezi kwani kwenda kinyume na maadili ya kazi zenu mnaweza kuupotosha umma ukizingatia kuwa ninyi ni muhimili wa nne wa nchi usio rasmi. "alisema. 
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYuJcDCPI3u3tD9st2-GGjD4cfuc7xXWxdphTDK0UZmlFoAXuQ1DFdWEYfK9U_vpDocFzmYGsIxMFBJTc76GtnfnFJVJQJaqss1hnp13ncSbhEl3L46fmHNgsgbx06LqYyo-oiQuJS1Ho/s640/2.JPG
Mwenyekiti wa Mkesha Mkuu wa Kuliombea Taifa (Dua Maalumu), Askofu Godfrey Mallassy. Kutoka kulia ni Askofu Nickson Kallinga, Mchungaji Derrick Luhende, Askofu William Mwamalanga, Makamu Mwenyekiti wa mkesha huo, Askofu Keneth Dismas, Mchungaji Debora Mallasy (Mjumbe), Mama Mchungaji Olivia Mallongo (Mjumbe) na Debora Elisha (Mjumbe).

 Akizungumzia mkesha huo alisema mkesha huo utafanyika katika mikoa mingine 16,ambayo ni Dodoma, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Iringa, Kagera, Ruvuma, Mbeya na Singida. Alitaja mikoa mingine kuwa ni Morogoro na Simiyu na lengo la mkesha huo ni kumshukuru mungu kwa awamu ya nne ya uongozi wa taifa na kuliombea taifa letu na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya na uchaguzi mkuu 2015. "Taifa lolote linatakiwa kuombewa kutokana na kupata maendeleo yaliyo kamili hivyo basi sisi wanadamu pekee hatuwezi kupata amani kwa siasa na Jeshi ila mwenyezi mungu pekee," alisema.
 
 Mchungaji Debora Mallasy (kushoto), akiwauliza swali wanahabari. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa mkesha huo,Askofu Keneth Dismas 
 
Maombi yakifanyika ndani ya Ukumbi wa Habari Maelezo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.
 
 Maombi yakifanyika baada ya mkutano huo. 
 
Wanahabari wakiwachukua taarifa hiyo.

Comments