
Zifaatazo ni habari picha katika matukio tofauti kwenye zaidi ya siku 2 za watu kufunguliwa, pia alifundisha kuhusu jinsi ambavyo wateule wanaweza kuwashinda wachawi, hili ni somo katika moja ya ibaada hizo huko Bujumbura Burundi.
MUNGU alimtumia mtumishi wake kuwaombea na kuwafungua mamia ya watu kwa jila kuu la YESU KRISTO.
![]() |
Mtume Peter Rashid Abubakar akiihubiri injili ya yesu. Hapa anaonekana akiwa na mtafisiri wake au mkalimani wake jijini Bujumbura. |


Senior Pastor/Mtume Peter Rashid Abubakar
alifanunua akisema: Wapo wafalme wengine wanahofu ya Mungu wengine
wachawi kama huyu Mfalme wa Babeli alisema leo tunaangamiza uchawi aina
4: 1. Penye kichwa cha njia: watu wengi hawafahamu kama hata njia zina
vichwa wengi wanajua njia ni njia tu kumbe ili mchawi akuroge hasimamima
kwenye njia tu ili mradi njia hapana hutafuta kichwa cha njia na kisha
anasimama kwenye kichwa hicho cha njia ndipo anaanza KUNUIZA UCHAWI WAKI
TENA KWA KUWATAJA WALE ALIOKUSUDIA KUWAROGA 2.Alitikisa MISHALE huko na
huko ikimaanisha pande nne za dunia ipo mishale ya kichawi ikirushwa
inamfikia yule aliyekusudiwa ndio wale unawasikia wakilalamika mara
nasikia vichomi visivyoisha mwilini mwangu hiyo ni mishale ya kichawi,
mwingine anatembea na MSHALE na ulikusudiwa ifikapo siku fulani na
tarehe fulani na mwaka fulani huo MSHALE utamuua ndio wale unaweza
kusikia kuwa FULANI AMEKUFA!! watu wanaanza kushangaa huku wakisema Mmh!
Mm nilikuwa naye tu na tuliagana kwa amani!! Amekufa!!!? Huo ni mshale
wa kichawi 3.

Aliziuliza TERAFI swali terafi ni nini? Terafi naweza
nikafafanua ni VITABU VINAVYOFUNDISHA ELIMU YA UCHAWI kama vile unaweza
kusikia KITABU CHA FARAKI;YAASINI;RUKYA;ALGHAZAR etc kiasi kwamba mchawi
aliyesomea uchawi huo hawezi kufanya uchawi wake hadi aviulize hivyo
VITABU ili vimpatie maelekezo mazuri asije akakosea ktk kazi zake! Sasa
basi alipozotazama hizo TERAFI 4. Ndipo alipoyaona MAINI yapo safi
yanafanya kazi vizuri ndipo kupitia uchawi huo akayaharibu maini yakawa
hayafanyi kazi! Ndio maana watu wengi sasa hivi waweza kuwasikia
wakisema jamani jamani mm maini yangu nimepimwa na Doctor wameniambia
maini yote yameharibika au ini moja limeharibika!! Kumbe huo ni uchawi
uliotumika. Senior Pastor Peter Rashid Abubakar aliombea watu wengi na
kufunguliwa kwa kukausha wafalme au viongozi wakubwa wa serkali
wanaotumia uchawi huo ktk jina la yesu, kisha alivunja vunja vichwa
vyote vya njia mahali wanaposimama wachawi ktk jina la yesu pia VITABU
vyote vya uchawi alivichoma vyote ktk ulimwengu wa roho kwa moto wa
Mungu.
![]() |
Siku Mtume Peter Rashid alipowasili Burundi. Hapa akiwa Air port na mke wake Pamela. |
Hakika wengi walifunguliwa.
Comments