MUNGU HUGUSWA SANA NA SADAKA YA SHUKRANI.

Mtumishi
Na Mtumishi wa Mungu Gasper Madumla. Akifundisha katika moja ya mikutano ya ndani,kigamboni.
Bwana Yesu asifiwe…
Mtumishi Baldiwin
MC Mwl.Baldwin Kachenje akisherehesha katika ibada ya mkesha wa kushukuru,katika kampuni ya Jambo freight ltd.
Watu wengi hawajaijua siri ya namna hii,maana wengi hudhani ya kwamba mguso wa Mungu upo kwenye ibada ya maombi peke yake. Kumbe Bwana Mungu wetu huguswa sana na ibada ya shukrani kwanza. Shukrani ni tendo kubwa sana lenye kila jibu la hitaji lako.Tazama waamini wa leo wana mahitaji mengi tena mbali mbali,mfano wapo watu wenye kuhitaji kuoa au kuolewa,wapo watu wenye mahitaji ya kujenga,wapo watu wenye mahitaji ya kumiliki biashara zao,wapo watu wenye mahitaji ya kukua kiroho,tena na zaidi wapo watu wenye mahitaji ya kupokea uponyaji wao,N.K
Majibu ya mahitaji haya yote yapo ndani ya ibada ya shukrani.Maana shukrani ni maombi tosha,huitaji kingine wewe anza kushukuru kwa moyo wako wote,naye Bwana atakupigania hiyo vita,maana vita si yetu bali ni ya Bwana.

Sikia;
Hata kibali halisi kitokacho kwa Mungu Baba,kipo ndani ya moyo wa mwamini uliojaa shukrani.

Watu wengi tunapitia katika magumu mbali mbali ya maisha,na si kana kwamba Mungu ametuacha bali sisi ndio tumemuacha Bwana Mungu kwa kushindwa kuwa na moyo wa shukrani,yaani tunatendewa mengi ila tunarudisha machache na wakati mwingine haturudishi kabisa. Endapo tukirejea mbele zake Bwana kwa shukrani tu,basi amini kufunguliwa katika kila aina ya vifungo.
John lisu
Mtumishi wa Mungu John Lisu akimuabudu Mungu katika mkesha wa kushukuru,Jambo Freight.ltd
Jambo hili ninalokuambia siku ya leo si kana kwamba nimelitunga hivi,au si kana kwamba ninasema kwa akili zangu binafsi,jambo hili ni Roho wa Bwana ndie asemaye nawe sasa,ukiamini kile nikuambiacho hapa,basi tegemea kuvuka katika kila eneo la maisha yako ndani ya mwaka huu na hata mwakani.
Sasa sikia;
Chukulia jambo hili katika mtizamo wa kawaida kabisa,yaani mtizamo wa kibinadamu juu shukrani,kwamba mtu mmoja anapokushukuru kwa jambo lolote uliomtendea,wewe utajisikiaje muda huo unaposhukuriwa? Je utajisika vibaya? Au moyo wako utafurahi ?
Ni dhahili kabisa na ni ukweli kwamba utafurahi. Sasa ikiwa wewe mwanadamu wa kawaida kabisa unapenda shukrani,basi Mungu ni zaidi.

Baba na mama Mzuanda.
Watumishi wa Bwana,Dr.& Mwl.Joe Mzuanda & mama Mzuanda wakiwamfanyia Bwana ibada ya kushukuru katika mkesha wa kushukuru mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Wapendwa,yapo mambo ya kufundishwa darasani kila siku lakini sio kuhusu shukrani!
Mfano,wewe ukipewa pesa labda elfu kumi tu,Je utafundishwa namna ya kushukuru? La hasha!

Bali utajikuta unanza tu kusema, ” asante…asante kwa pesa…” Ndivyo itupasavyo kumshukuru Bwana Mungu kwa mengi atutendeayo yasiyoweza kuelezeka,kwa mfano tu kumshukuru kwa pumzi ya bure,kwa afya ya bure,kwa ulinzi wa bure,kwa neema na rehema za bure,tena kwa kumaliza na kuingia mwaka mpya kwa bure,N.K
  • Katika kushukuru,kunamfanya Yule aliyeshukuriwa kutoa zaidi.
Kwa mfano mtu  mmoja anaweza akawa amekupa kitu kidogo tu,ila wewe ukimrudia mtu huyo kwa moyo wa shukrani basi ujue utamfanya mtu huyo aguswe zaidi na hata kuamua kukuongezea na mengine ambayo hata hukuyaomba kwake. Mungu naye ni zaidi,Wewe unapolejea kwake kwa moyo wa shukrani basi ujue unamgusa sana hata kukuachilia na vitu vingine ambavyo yamkini hukumuomba.
Zawadi-Mtumishi Madumla.
Wana familia ya jambo freight ltd,wakimtolea Mungu zawadi ya shukrani kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 ( Mtumishi Gasper Madumla akiwa kushoto wa kwanza)
Labda nikuoneshe kidogo katika Biblia ;
Imeandikwa;

” Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.’’ Luka 17:12-19

Sikiliza ndugu,
Biblia inasema kwamba mmoja kati ya wale kumi walioponywa,yeye akamrudia Bwana kwa shukrani.Mtu huyu aliyerudi alimsababisha Bwana Yesu Kristo kuachilia WOKOVU ndani yake. Tazama maneno ya Bwana Yesu hapo,anasema;

Waberoya-Sinza
Waberoya wakimtolea Bwana Mungu shukrani,na kuwapongeza watumishi mbali mbali wanaohudumu JFL,pamoja na Beroya,wakiongozwa na mtumishi mama Mzuanda.
‘’Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.’’ Luka 17:12-19
Wale wengine kenda walipokea uponyaji tu,lakini imani yao haikuwaokoa mbali na dhambi.. Huyu imani yake ikampa kuokoka,yaani Bwana Yesu akampa maisha mapya,jambo ambalo asingelipata yamkini kama asingerudi kushukuru.
Kushukuru kwa huyu mmoja kulimgusa Bwana Mungu hata akaachilia wokovu na maisha mapya ambayo wenzake kenda walikosa.

Jiulize na hujioji kwamba ni mara ngapi unajizuilia miujiza yako kwa kushindwa kushukuru?
Watumishi
Watumishi wa Bwana wakienda sawa katika mkesha wa kushukuru ( Mtumishi Gasper kushoto,Mtumishi Isaac,na mwinjilisti Musa Gwau )
Kumbe! Milango ya miujiza yako ipo wazi,ila tatizo lipo kwako kwamba humegoma kushukuru kwa hayo yote aliyokupa Bwana. Na inawezekana shida yako wala haitokani na vifungo vya mapepo,bali inawezekana umekwama katika sehemu moja tu ya shukrani.
  • Ibada ya kweli ya shukrani huanzia moyoni na kuishia katika matendo.
    Yeye anaye mshukuru Bwana Mungu kwa moyo wake wote,basi ujue ni dhahili ataonesha shukrani yake katika matendo pia yaani ataonesha kwa kumtolea Mungu kitu cha thamani.
    Haiwezekani mtu anayemshukuru Mungu kwa moyo wake wote,ashindwe kuonesha matendo ya kutoa sadaka iliyo njema machoni pa Bwana wake.
Mama Mzuanda
Mkurugenzi wa Jambo Freight ltd,mtumishi mama Mzuanda akisema neno kwa niaba ya kanisa la Waberoya Kimara.
Haiwezekani hiyo! Ni lazima mtu huyo atadhihilisha kwa matendo pia.
Kanisa la leo,lina shida katika eneo hili la shukrani inayoanzia moyoni,ndio maana utaona mtu anamtolea Bwana Mungu wake kitu kibovu katika vyema alivyonavyo.

Mwamini wa namna hii,hajashukuru bado kwa moyo mkunjufu na kamwe hawezi kumgusa Mungu. Mfano mwamini anamtolea Tshs 500.00(Shilingi za kitanzania mia tano tu ) Bwana Mungu wake katika ibada ya mwaka mzima,tena ni ibada ya kushukuru,hali mtu huyo akila vitu vya thamani zaidi ya hiyo Tshs 500 aliyoitolea kama sadaka ya kumshukuru Mungu kwa mwaka mzima.
Na tena cha ajabu mtu huyo utakuta simu yake hujaa vocha kila siku yaani kuanzia Januari hadi Disemba anailisha simu,na hapo hapo bado anamtolea Bwana Mungu wake mia tano !! Jamani!
Sasa utamgusaje Bwana Mungu aachilie mibaraka yako ikiwa utamtolea kwa unyonge wa namna hiyo?
Wengine hutoa buku moja iliyochoka! ( Tshs Elfu moja ya kitanzania ) kati ya pesa nyingi walizonazo. Sababu mlo wa mtu mmoja kwa siku ni zaidi ya elfu moja,hapo hapo mtu huyo utakuta akivaa vitu vya thamni ya zaidi ya hiyo elfu moja,hapo hapo bado hajailisha simu yake ya kiganjani,alafu ndio umtolee Mungu Elfu moja ya kitanzania!!!

Nataka niseme na wewe sasa hivi;
Siri yako ya kuvuka katika kila eneo ni kuwa na moyo wa shukrani kwanza. Hata kama unaona kile ukiombacho hujapata kwa muda huo,wewe endelea kukaza kushukuru mbele za Bwana,maana neno linasema; ‘’ shukuruni kwa kila jambo…’’ 1 Wathesalonike 5 :18
Bwana Mungu akiguswa katika shukrani,basi ujue mbingu,bahari na nchi zitatikiswa kwa ajili yako,ili zikatoe mibaraka yote. Imeandikwa;
” Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu;
nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi.
Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.” Hagai 2:6-8

Sula la kuzitikisa mbingu sio suala rahisi rahisi,ni mpaka ufanye kitu cha ziada ndipo mbingu zitikiswe kwa ajili yako,Na mwenye kuzitikisa si wewe,bali ni Mungu,wewe kazi yako ni kutenda kwa moyo wa shukrani. Ipo kazi ya ziada ya kufanya mbele za Bwana Mungu,kazi hiyo ni kuwa na moyo wa shukrani kwanza kabla ya yoyote yale.
Mch.Julie
Mch.Julie wa huduma ya Waberoya,na Jambo Freight.ltd akitoa neno katika ibada ya kushukuru. ” Mungu hupendezwa kwa shukrani”
  • Mguso wa Mungu wetu ni kuwa na moyo wa shukrani,kutoa kilicho chema zaidi.
Hii ni siri kubwa sana kwako,Mungu anakuhitaji umshukuru kwa moyo kwa ajili ya neema na rehema zake kwako,pia moyo huo wa shukrani yako uambatane na matendo ya utoaji.Matendo ya utoaji pia yanaambatana na kuwasaidia makundi mbali mbali ya wahitaji tulio nao katika jamii inayotuzunguka mfano leo wapo yatima,wapo wajane,wapo wahitaji wa kila namna.
Ninajua yamkini umejaribu njia nyingi za kujinasua katika hilo tatizo lako,lakini bado hujapata majibu sahihi,siku ya leo ninakushauri kipendwa kabisa nikikuambia jaribu njia hii ya kumfanyia Bwana ibada ya shukrani pale unapoabudu.
Ibada hiyo itoke ndani ya kilindi chako cha moyo,umshukuru Bwana Mungu kwa kukulinda mpaka leo wewe na watoto wako,wewe na familia yako,wewe na ndugu zako,kisha umtolee Bwana Mungu kitu chema machoni pake.Alafu sasa utaniambia kama Bwana Mungu hajakufanyia miujiza yako. Kama unaamini hayo nikuambiayo,utayapata majibu yako.
Kwa huduma ya maombi na maombezi,nipigine namba yangu hii;
0655-11 11 49.

UBARIKIWE.

Comments