Myles Munroe na mke wake kuzikwa leo.




Mshindi wa tuzo ya Injili ya Grammy mwimbaji CeCe Winans atatumbuiza  katika tukio la mazishi yaliyotambuliwa na serikali ya Bahamas kwa wapendwa mchungaji mashuhuri Myles Munroe na mke wake, Ruth, ambao walifariki katika ajali mbaya ya ndege  pamoja na watu wengine saba katika Bahamas Novemba 9.

Kevin Harris, msemaji wa Bahamas Faith Ministries iliyoanzishwa na Munroe, alithibitishia gazeti Christian Post Jumatatu kwamba Winans atashiriki katika mazishi ya wanandoa hao Alhamisi, Desemba 4.
Harris alieleza kuwa mazishi yatakuwa yakiserikali kwa kuwa inatambua mchango wa Munroe kwa taifa na kisiwa hicho.
Kulingana na Serikali ya Bahamas ,  mazishi yanayotambuliwa na  serikali  ni kutoka kwa wabunge, (Seneti), kuwahudumia makatibu wakuu na viongozi wengine wa ngazi za juu wa umma au raia. 
msaada kutoka serikali utakuja katika mfumo wa matangazo ya moja kupitia redio pamoja na mahudhurio ya wawakilishi wa serikali. mazishi yatakuwa wazi kwa umma.
Harris alieleza kuwa mazishi yatakuwa kesho Alhamisi  yakitanguliwa na ratiba ya shughuli ya Jumatano, Desemba 3, wakati miili ya Munroe na mke wake itabaki katika mapumziko katika Bahamas Faith Ministries Diplomat Center 10:00-5:00
Kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa sita mchana wanachama wa familia Munroe na viongozi waandamizi wa serikali watatoa heshima zao katika hafla binafsi wakati umma kwa ujumla wataruhusiwa kusaini kitabu cha rambirambi kuanzia saa sita mchana mpaka 05:00
kumbukumbu ya kitaifa itaanza saa moja baadaye katika Thomas A. Robinson Uwanja Oaks Field Sporting Complex katika Nassau, Bahamas na itaendelea mpaka 11:00

Comments