somo:MJI WA MAUTI

SNP Dr Godson
                           Utangulizi

Mji wa mauti unaitwa mji wa mauti kwa sababu kazi yake kubwa ni kusababisha mauti. Na majina mengine unaitwa mji wa damu au mji wa kuzaa mapoza, na umeandaliwa na shetani mwenyewe, mji huu umefanyika kuwa ni karakana ya kutengeneza matatizo.  Ndani ya huu mji kuna mauti, kukosa kazi, kuzaa mapoza, kuna magonjwa, kuna umaskini, kukataliwa.
 
2WAFALME 2:19 “watu wa mjini wakamwambia Elisha, angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapoza”. Unaweza ukawa unafanya biashara Fulani na unaweza ukawa unapata faida lakini kumbe ndani ya biashara hiyo kuna mauti. Kwa mfano: biashara ya bodaboda, watu wanasema “asante mchina ametusaidia”  lakini angalia jinsi ambavyo watu wengi wanakufa kutokana na hizo bodaboda.

LUKA 19: 41-43 “ Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia akisema laity ungalijua yata wewe katika siku hii yapasayo amani, lakini sasa yamefichwa machoni pako………….” Hapa Bwana Yesu aliuona ule mji na akawa anaona mauti ndani ya huo mji lakini watu wengine walijua ni amani walizidi kushangilia na kufurahi  (mstari wa  37)  lakini mafarisayo waliona wivu na walijua kuwa wao na mji wao wako salama hata hawamwitaji Yesu. Hivyo walianza kuwanyamazisha wanafunzi wa Yesu. Bwana Yesu aliwajibu kuwa wajaponyamaza wanafunzi hawa, mawe yatainuka na kushangilia hivyo hivyo. Huu mji wa yerusalemu Bwana Yesu aliuona uharibifu uliokuwa mbele yake na ndivyo ulivyo mji wa uharibifu umejaa damu japokuwa mtu huwezi ukauona kwa macho.

NAHUMU 3:1-4  “Ole wake mji wa damu, umejaa mambo ya uongo na unyang’anyi, mateka hayaondoki…….. kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa Yule kahaba mzuri, Yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake. Kwenye vijiji utakuta kuna mtu mmoja ambaya ni mchawi na kila mtu anajua kabisa kuwa huyo mtu ni mchawi lakini wanamwogopa kijiji kizima wanamwogopa kwa ajili ya mambo yake ya uchawi. Hivyo kupitia yeye mji mzima umejaa damu kwa ajili ya kuwaua watu lakini hiyo miji yote ni lazima iharibiwe kwa Jina la Yesu.
Katika mahubiri yaho mchungaji alizidi kusisitiza kuwa ni muhimu kufahamu kuwa kuna maisha ambayo watu wanayaishi ni maisha magumu yamejaa taabu ambazo hata kama rais wan chi angeamua kukussaidia asingeweza. Kwa mfano kama mtu umechukuliwa msukule, rais wan chi hawezi kukutoa msukuleni, yeye atakachoweza kufanya atahakikisha kuleta huduma za jamii mfano kujenga shule, kuleta umeme, kuleta maji, lakini rais wa nchi hawezi kukusaidia wewe ukiwa unakandamizwa na wachawi, ni mpaka pale ambapo watu wote watakapoamua kumtegemea Yesu ndipo watakapoweza kuwekwa huru mbali na mji wa mauti. Hivyo ni muhimu kufahamu kuwa miji ya mauti inaweza kupanga vifo kwa ajili ya watu, lakini kwa wale ambao ni wana wa ufufuo mji wa mauti hauna nguvu juu yao. HII NI SAA YA UFUFUO NA UZIMA.


             
Mch Kiongozi Dr Godson akimfungua mtu leo baada ya huyo dada kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.

Comments