Katika nyakati hizi za mwisho unahitaji utembee katika nguvu ya ufufuo kwasababu maajenti wengi wa shetani na roho zidanganyazo zinafanya kazi kwa bidii sana kuyaangusha na kuyapeleka makanisa,huduma na maisha ya watu wengi kwenye ziwa la moto ( 1 Petro 5:8).

Wakristo wengi wanashindwa kumpendeza Mungu,kwasababu hawatembei katika nguvu ya ufufuo na hawamuombi Mungu awape hiyo nguvu ya ufufuo,nguvu ya kufufua vitu vilivyokufa katika jamii zao,nguvu itakayofufua uamsho wa Injili utokee tena katika maisha yao.
Nguvu ya ufufuo itakayofufua tena fikra na mitazamo ya watu kuhusu Yesu Kristo na nguvu na mamlaka yake aliyo nayo na jinsi inavyofanya kazi.
Nguvu ya ufufuo inayopatikana kwa Huyu Mwanaume Yesu ya kuwafufua tena wapendwa waliorudi nyuma tena kwa kuuona Wokovu ni mgumu (1 Yohana 3:8b).
Badala yake
tunatumia mwingi sana kuomba tupate magari,majumba mazuri,mavazi ya
thamani,vyakula vya gharama,tunashindwa kabisa kuomba tupate nguvu ya
ufufuo itakayofufua tabia zetu njema,mawazo mazuri,matendo
yatayompendeza Mungu.
Kama hutembei katika nguvu ya ufufuo ya kutaka kuona watu wengi wanakuja kwa Yesu,basi unaweza kudanganywa na elimu nyingi za uongo zinazopatikana katika ulimwengu huu
Kutembea katika nguvu ya ufufuo ya Yesu Kristo utaweza kuzijua Injili feki ambazo muda wote zinahubiri tu kuhusu mafanikio bila ya kujali dhambi za watu wanazozitenda kila siku (Mathayo 6:33).
Ukiwa na nguvu ya ufufuo inayopatikana kwa Yesu itakuwezesha kumrudisha mtu aliyekuwa anaelekea njia ya upotevuni na kumrudisha kwa Bwana Yesu ( Mathayo 28:19-20).
Tamani kuwa na nguvu ya ufufuo katika Kristo Yesu katika maisha yako ya kuwaona watu wanakuzunguka wakimpokea Yesu Kristo
Waombee kila siku waache njia zao mbaya kabla hii neema ya bure haijaisha.
Mwambie Mungu akuwezeshe kutembea katika nguvu ya ufufuo katika Kristo Yesu.
MUNGU akubariki sana.
By Godwin Mlay.

Comments