UMUHIMU WA KUJARI WOKOVU NA USHIRIKA NA KRISTO.

Bwana Yesu asifiwe!

Namshukuru kwa nafasi hii tena kunipa somo hili ili tuzidi kujengana kiroho na mwili wa Kristo upate kujengwa.

Na Emmanuel Kamalamo.
Najua kila mmoja anajua nini maana ya WOKOVU. Lakini Roho Mtakatifu anaweza akasema na wewe kwa kona nyingine na ukapokea kitu cha kikusaidia, maana Neno la Mungu ni jipya kila siku.
NINI MAANA YA WOKOVU?
>WOKOVU-Ni matokeo ya MSAMAHAA WA DHAMBI anaoupata mtu baada ya kutubu dhambi. Na WOKOVU huo huleta badiliko la maisha kwa mtu na kuishi maisha mapya ambayo tunaita..."MAISHA MATAKATIFU".
Ukisoma Injili ya Luka 1:77 maandiko yanasema..."Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao". Ok, kama WOKOVU nikutangaziwa MSAMAHA WA DHAMBI, nani anatangaziwa? Ni mimi na wewe. Kwa mantiki hiyo huwezi kusamehewa dhambi kama haujatubu dhambi na kuziacha.
Huwezi kuacha dhambi na kuishi maisha matakatifu kama huna USHIRIKA NA YESU KRISTO aliye asili ya UTAKATIFU.Neno linasema.."Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika na mwanaye" (1 Wakorintho 1:9)
Lengo la Mungu kukuita na akuingize katika "USHIRIKA" na Yesu ni kutaka ule muungano wako na Yesu ukusaidie kuishi maisha MATAKATIFU, Na kuingia kuishi maisha matakatifu ni WITO unapewa, (wale waliotakaswa katika Kristo Yes, walioitwa wawe watakatifu" 1Wakor 1:2) kinachobaki ni kuitika wito huo, Mungu akulazimishi uwe MTAKATIFU bali anakutengenezea mazingira ya kukusaidia uwe mtakatifu, na mazingira hayo ni kuungana na Kristo.
Ndiyo maana baadhi ya watu kwa kukosa "USHIRIKA NA YESU" wanaishi nje ya WOKOVU. Maana yake hawajasamehewa dhambi zao kwa sababu wanaendelea na maisha ya dhambi na kanisani wakwenda...ooh! Sikia nikwambie, ili upone juu ya HUKUMU YA JEHANAMU hakikiksha unajali wokovu, kama uamini kasome Biblia yako uwe na uhakika utaambiwa.."SISI JE! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII?" (Waebrania 2:3)
KAMA HUJAOKOKAOKOKA LEO
BAADA YA KUFA NI HUKUMU
(Waebrania 9:27)

MUNGU WANGU AKUBARIKI
By Emmanuel Kamalamo.

Comments