UTULIVU WA ROHONI


“Je! Wote wafanyao maovu hawajui?........................................................... “ ZABURI 14:4.
BWANA YESU asifiwe wana wa Mungu,
Na Godfrey Miyonjo.
Wana wa Mungu tushirikiane katika somo hili na ninaamini kuna kitu kitakwenda kufanyika juu ya maisha ya kila mmoja atakayeshiriki.
Watu wa Mungu, Mungu wetu anauliza “Je! Wote wafanyao maovu hawajui? “
Jibu ni kwamba asilimia 90 kama siyo 100 ya wote watendao uovu wanajua kuwa uovu ni machukizo mbele za Mungu.
Kinachokosekana kwao ni KUKOSA UTULIVU WA ROHONI wakati wanafanya maamzi.
Mahala pengine Mungu anasema: “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa” HOSEA 4:6.
Tukijiuliza kwa nini watu wa Mungu waangamizwe kwa kukosa maarifa? Jibu linalokuja haraka ni kwamba: kwasababu walio wengi hawana UTULIVU WA ROHONI, hivyo siyo rahisi kwao kupata muda wa kuyatafakari maneno ya Mungu.
Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna jambo ambalo linaweza likatendeka kwa usahihi kwa mtu asiye na UTULIVU WA ROHONI.
Mtu asiye na UTULIVU WA ROHONI daima huwa anafanya bora liende tu kutokana na mazingira yalivyo.
Kwa mfano:
Kuna watu wanajutia uamuzi wao wa kuoa/kuolewa kwasababu walikurupuka wakati wa kufanya maamuzi, hivyo wameingi kwenye ndoa na watu wasiokuwa wa kwao.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI kuna watu hadi leo bado hawajampa YESU KRISTO maisha yao, kwa sababu hawajakaa chini na kutafakari nini hatma ya maisha yao.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wanatamani sikukuu yoyote ile itokee hata kama isiyowahusu ili walewe, wafanye uzinzi/uasherati, waibe na kufanya kila aina ya uovu pasipo kujua kuwa kile wanachokifanya kinakwenda kusababisha wao kuangamia kimwili na kiroho pia.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wameshikilia mafundisho ya uongo ya dini zao na mizimu yao pasipo hata kutafakari, ili kujua ukweli ulio ndani yake.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu walio wengi wanapita tu masomo yaliyoandaliwa na watumishi mbalimbali wa MUNGU pasipo kuyasoma, wakati mwingine hulike na kucommen “AMEN” pasipo hata kujua kilichoandikwa kinahusu nini.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wanaishi bila malengo kwa mwaka mzima, yaani tokea JANUARI hadi DESEMBA hajajiwekea malengo yoyote juu ya maisha yake ya kimwili na kiroho pia.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu watu wanashindwa kuyafikia malengo yao waliyojiwekea wenyewe.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wanazitumikia SANAMU na HIRIZI ambazo haziwezi kuwasaidia kwa lolote. Mfano Sanamu zina macho lakini hazioni, zina msikio lakina hazisikii, zina pua lakini hazinusi, zina mtomo lakini haziongei, N.K.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wengi wanawaogopa na kuwaheshimyu wanadamu (wachawi, wenye mamlaka/viongozi, waume/wake) kuliliko MUNGU.
Kwa kukosa UTULIVU WA ROHONI watu wanakuwepo katika majumba ya ibada lakini mawazo yao yanakuwa yapo mbali na ibada, wanawaza wake/waume zao, mali zao, biashara zao, N.K.
MPENDWA HAKIKISHA UNAPATA MUDA WA KUTULIA NA KUMTAFAKARI BWANA,
Kumbuka KWENYE UTULIVU WA ROHONI ndipo palipo na majibu,
Ikiwa kuna maombi uliomba inakupasa utulie ndipo upokee majibu, kumbuka DANIELI alisubiri kwa siku 21 (DANIELI 10:11-14)
Pia Wakati wana wa Israeli waliponyamaza kimya/wlipotulia ndipo BWANA alipowapigania (KUTOKA 14:11-14,19-30)
Kwenye utulivu ndipo Mungu atakupa mafunuo/atasema na wewe, fanya hima ukae kwenye uwepo wa BWANA.
MUNGU akubariki sana. 
By Godfrey Miyonjo.

Comments