UWE NA BIDII UKATUBU


“Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii ukatubu” UFUNUO 3:19.

BWANA YESU ASIFIWE milele.

Wapendwa, upendo wa Mungu kwetu ndio unaopelekea Mungu kuwatuma watumishi wake kwetu kila iitwapo leo, ili watufundishe, watuonye, wakati mwingine hata watukaripie.

Mungu huyafanya hayo ili kila mmoja wetu afikirie toba, kila mmoja aamue kumgeukia Mungu, asiwepo mtumwa wa dhambi.
Pamoja na Mungu kutupenda na kutumia gharama kubwa ili kuhakikisha kila mmoja wetu anaijua kweli, siku hizi kumekuwa na watu wasioipenda kweli, watu nanaokataa mafundisho, watu wasiopenda hata kusikia habari za Mungu.
Na Godfrey Miyonjo.

Hili ni tatizo kubwa sana katika kizazi hiki, watu wamekuwa wakitetea madhehebu yao, dini zao pasipo hata kujipima katika Neno la Mungu kama wako sawa au la!

Watu wameyakumbatia mafundisho ya uongo wanayofundishwa katika dini zao, yapo mafundisho mengine huwa ni siri ya washirika tu wa dini au dhehebu husika.

Watu hula kiapo kuwa hata iweje, wasije asi dini au dhehebu husika.
Hata kama wataamua kuishi dhambini ni sawa ila hawaruhusiwi kubadili dini au dhehebu.

NDUGU, DINI NA DHEHEBU VITAKUFAIDIA NINI MBELE ZA MUNGU, IKIWA HUNA WOKOVU?

Acha kuganda juu ya siri za dini yako, mwamini Yesu akuokoe.
“Kisha itakuwa wakati ule, nitachunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya siri zao;…………………….” SEFANIA 1:12.

Dhambi yaweza ikawa siri mbele za wanadamu ila siyo mbele za Mungu.

Jichunguze ndugu, kama haupo sawa katika njia zako amua kuacha yote, jikane na ujitwike msalaba wako umfuate BWANA YESU.
Nawe usemaye umeokoka, na bado unatenda dhambi kwa siri siri tambua kuwa ghadhabu ya Mungu inakuja, tubu leo kabla siku ile haijafika.
MUNGU akubariki.
By Godfrey Miyonjo.

Comments