VIWANGO VYA KUFIKA MBINGUNI

Bwana Yesu asifiwe,leo napenda nikushirikishe hili somo linalohusu jinsi ya kufikia viwango vya mbinguni ambavyo vimewekwa na Mungu Baba mwenyewe kupitia Yesu Kristo (Isaya 40:8).
Hivi ni viwango ambavyo vimewekwa ili vitusaidie sisi tuishi maisha mema yanayompendeza Mungu hapa duniani na viwango hivi vitusaidie sisi wanadamu ili tuweze kuingia mbinguni na viwango hivi kamwe havibadiliki.

VIWANGO VINAVYOTUWEZESHA KUFIKA MBINGUNI
1.KUMPOKEA YESU KRISTO
Yesu ndiye njia na kweli ya kutufikisha kwa Baba yake.
Yesu ndiye Mkombozi wa ulimwengu huu na mtu mwenye mapenzi ya dhati kabisa ya kwenda mbinguni ni lazima kwanza ampokee Yesu Kristo kama Bwana na Mkombozi wa maisha yake (Yohana 14:6).
Wapo watu wengi sana wanafarijiana kuwa unaweza kuishi maisha mema na hakuna ulazima wa kumpokea Huyu Yesu na mbinguni utaenda tu kwa kuwa Mungu anaangalia duniani uliishi maisha ya namna gani huku ni kupotoshana.Mungu aliamua mwenyewe kuweka kiwango hiki cha kumpokea Mtoto wake Yesu Kristo kwanza katika kizazi hiki huku maisha ya utakatifu yanafuatia.Ninaweza kusema hivi kuwa kuishi maisha yasiyokuwa na dhambi huku hujampokea Yesu Kristo katika maisha yako huko ni kutofikia kiwango cha kukuwezesha kuingia mbinguni.
Tunaweza tukawa tunawajua watu wengi sana ambao wametangulia mbele ya haki kwenye kiti cha hukumu ambao hapa duniani kwa kweli waliishi maisha mema na yanayompendeza kila mtu na hawakuona haja ya kumpokea Huyu Yesu kwanza walijua maisha yao mema ndiyo yatakayowaingiza mbinguni kwa kweli ninaweza kusema wanasubiri kutupwa ziwa la moto maana walikataa hiki kiwango kimojawapo cha kumpokea Yesu Kristo awe Mwokozi wao ili awaonyeshe njia ya kwenda mbinguni kwa Baba yake.
Haijalishi mtu ameishi maisha mema kiasi gani katika nyakati hizi huku haoni haja ya kuwa na Yesu moyoni mwake basi atarajie tu kutoiona mbingu ambayo watu walioamua kumpokea Yesu wameahidiwa.
Ni muda wa kuwaambia watu ukweli kuwa bila kuwa na kiwango hiki cha kumpokea Yesu mtu hawezi kufika mbinguni maana neno la Mungu halibadiliki kamwe.

2.KUZALIWA KWA MAJI MENGI NA KWA ROHO
Hiki ni kiwango chengine cha kufika mbinguni maana Yesu mwenyewe amesema katika neno lake kuwa mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu (Yohana 3:5).
Kuzaliwa kwa maji maana yake ni kubatizwa kwa maji mengi na inafanyika kwa mtu ambaye amekwisha kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.Hiki ni kiwango pia ambacho Mungu mwenyewe amekiweka ili tuweze kufika kwake mbinguni.

3.MATUNDA TISA YA ROHO MTAKATIFU
Viwango vya Mungu kamwe havibadiliki na Yesu Kristo mwenyewe atamuhukumu kila mtu kutokana na neno lake aliloliweka kwetu (Ufunuo 19:11-13).
Matunda tisa ya Roho Mtakatifu ni mmojawapo ya viwango ambavyo vinatuwezesha kufika mbinguni.



Unaweza ukawa unajiuliza matunda hayo tisa ya Roho Mtakatifu ni yapi hayo.
Tukisoma Wagalatia 5:22-23 tunakutana na matunda hayo ambayo ni UPENDO,FURAHA,AMANI,UVUMILIVU,UTU WEMA,FADHILI,UAMINIFU,UPOLE NA KIASI.
Inatakiwa uwe nayo yote lisipungue hata moja katika maisha yako kila itwapo leo kama una nia ya kwenda mbinguni.

Ninachoweza kusema viwango vya kufika mbinguni vipo vingi katika neno la Mungu hivi ni baadhi tu.
Damu ya Yesu ikanene mema kwako katika siku yako ya leo huku ukitafakari baadhi ya viwango hivi ambavyo vinamuwezesha mtu kufika mbinguni.Amen

Comments