Kina mama wakiwa na watoto wao katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es
Salaam jana baada ya kujifungua katika mkesha wa Krismas. Picha na
Venance Nestory
Muuguzi mkuu wa zamu wa Hospitali ya Amana, jijini
Dar es Salaam, Teresia Akida alisema kati ya watoto 52 walizaoliwa
wakiume ni kiume ni 31 na wa kike 21.
Alisema mmoja wa wazazi wa watoto hao, Asha
Abdallah alijifungua watoto watatu wa kiume ambao bado hawajatimiza
miezi, hivyo wamehifadhiwa kwenye mashine za watoto njiti.
“Watoto wote wanaendelea vyema na hali afya zao ukiacha hao watatu ambao bado wapo katika uangalizi maalumu.
“Pia, kuna pacha wengine wawili wa kike na wa kiume ambao wamezaliwa na afya njema,” alisema.
Abdallah alisema anaendelea vizuri na afya yake isipokuwa watoto wanaendelea na matibabu.
“Licha ya kuwa na hali hii lakini wananyonya vizuri maziwa,” alisema.
Kwa upande wa Hospitali ya Temeke, watoto 19 walizaliwa, wakiwamo tisa wa kike tisa na 10 wa kiume.
Ofisa muuguzi wa hospitali hiyo, Grace Rusya alisema watoto hao wamezaliwa katika njia za kawaida na wakiwa na afya njema.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sophianias Ngonyani alisema kati wa watoto 30 waliozaliwa, wa kiume 17 na wakike 13.
Katika hatua nyingine; watoto 20 walizaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Mariam Mazengo
alisema watoto sita wamezaliwa kwa njia ya upasuaji na wengine 14
kawaida.Mazengo alisema watoto wanane kati ya 20 ni wa kike.
Mkoani Tanga, watoto 11 walizaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Bombo wakiwamo pacha wa kike na kiume waliozaliwa kwa njia ya upasuaji.
Muuguzi wa zamu wodi ya wazazi, Ashirina Mwanyoka
alisema watoto wa kiume ni saba na wa kike wanne. Alisema watoto wote na
mama zao wako salama kiafya.
Comments