WOKOVU NI ZAWADI BORA YA WANADAMU KUTOKA KWA MUNGU.


BWANA YESU atukuzwe.
Karibu nikujuze mipango ya MUNGU  juu wa wanadamu.
Wokovu ni zawadi bora kutoka kwa MUNGU kwa ajili yetu wanadamu.
 ''Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. -Waefeso 2:8-9''
Ukiupata wokovu unaingia kwenye familia ya MUNGU.
Wokovu ni kumpokea YESU KRISTO.
Walio na wokovu Biblia inasema neno hili juu yao.  " Naye Alituokoa Katika Nguvu Za Giza, Akatuhamisha Na Kutuingiza Katika Ufalme Wa Mwana Wa Pendo Lake. Ambaye Katika Yeye(YESU) Tuna Ukombozi, Yaani, Msamaha Wa Dhambi- Wakolosai 1:13-14. 
-Ni Furaha Kuu Kuwa Ndani Ya YESU KRISTO.
-Sio wote wamempokea BWANA YESU ila 
ni faida kuu kumpokea BWANA YESU maana,

- Kumpokea YESU Ni Kuvuka Kutoka Mautini Na Kuingia Uzimani. 
 ''Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia.Yohana 3:36''
YESU Akikuokoa ndugu yangu, Hata Ukiondoka Duniani kama una  Wokovu Wa BWANA YESU Utakua Unaishi Paradiso(pema Peponi) Hata Kama Walio Duniani Watakuwa Wanakuita Marehemu. 
-YESU KRISTO Ni Muhimu Kuliko Vyote Unanavyovifahamu.

''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. -1 Yohana 1:9''
 Baada Ya Kifo Ni Hukumu. Neno Hilo Watu Wengi Hawapendi Kulisikia Ila Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli lakini YESU KRISTO Anaokoa, Na Kama Ukimpokea  Unaokoka, Warumi 8:1-2 inasema '' Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika KRISTO YESU imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. ''
Ukiwa umempokea YESU KRISTO kama BWANA na MWOKOZI wako MUNGU anakuambia usiogope.
Hii ni ahadi kwa wateule wa MUNGU, Kwamba tusiogope.
''Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe, usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia naam, mkono wa kuume wa haki yangu.Tazama wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika, watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. {Isaya 41:10-11} 
Ndugu yangu, JEHOVAH MUNGU ana ushindi wako, ana ushindi wako wa kuyashinda ya dunia na ana ushindi wako wa kuwashinda kila mawakala wa shetani ambao wanataka kukutoa kwenye Wokovu wako. omba tu naye atajibu maana yeye huliangalia neno lake ili alitimiz.
 ''Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. -Yohana 3:16''
MUNGU akubariki sana kwa kujifunza ujumbe wa leo. Na lengo la MUNGU ni kukuokoa mara tu baada ya wewe kuijua kweli yake.
Kama unataka kuokoka omba kwa sauti yako maombi haya kisha baada ya hapo jiunge na kanisa la kiroho wanaoifundisha kweli ya KRISTO. OMBA HIVI.

 Eee BABA Wa Mbinguni, Ninakuja Kwako Katika Jina La YESU KRISTO. Neno Lako Linasema " Yeyote Ajaye Kwangu Sitamtupa Nje Kamwe-Yohana 6:37." Basi Ninajua Kwamba BWANA Hutanitupa Nje, Bali Utanipokea. Ninashukuru Kwa Hili. Ulisema Katika Neno Lako Kwamba " Ukimkiri YESU Kwa Kinywa Chako Ya Kuwa Ni BWANA, Na Kuamini Moyoni Mwako Ya Kuwa MUNGU Alimfufua Katika Wafu, UTAOKOKA, Kwa Kuwa Kila Atakayeliitia Jina La BWANA ATAOKOKA-Warumi 10:9,13". Ninaamini Kwa Moyo Wangu Ya Kuwa YESU KRISTO Ni Mwana Wa MUNGU. Nisamehe BWANA Dhambi Zangu Zote, futa jina langu kwenye kitabu cha hukumu na  Liandike Jina Langu Kwenye Kitabu Chako Cha Uzima. Ninaliitia Jina La YESU Na Ninajua BABA Wa Mbinguni Unaniokoa Sasa. Neno Lako Linasema " Kwa Moyo Mtu Huamini Hata Kupata Haki, Na Kwa Kinywa Hukiri Hata Kupata Wokovu-Warumi 10:10" Nimeamini Kwa Moyo Wangu Na Ninamkiri BWANA YESU Sasa Na Kwa Sababu Hii Nimeokolewa. Nafunga Ukurasa Wa Dhambi Na Nafungua Ukurasa Wa Mema Tu ROHO MTAKATIFU Nisaidie. Asante BWANA YESU Kwa Kuniokoa. Kwa Jina La YESU KRISTO Nimeomba. AMEN.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.Endelea kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments