ZIJUE SABABU ZA KUZALIWA YESU KRISTO NA UZIPOKEE NA ZILETE WOKOVU MAISHANI MWAKO.


Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa kwa kunipa siku ya leo, nami nitaifurahia na kuishangili.
Mungu awabariki nyote pia mnaotajia kupokea wokovu wa roho zenu katika Kristo Yesu Mwokozi wetu.
Najua kila mahari sasa kuna maandilizi ya ya sikukuu ya KUZALIWA YESU KRISTO.

Na hii inasherekewa na mtu yeyote awe na asiwe na dini.

Haya ni mambo muhimu tuyafahamu, na kama unayafahamu basi kuna baadhi awayafahahamu basi ni muhimu na wao waya fahamu na kuokolewa kupitia kuyafahamu sasa.

MAMBO MATATU MUHIMU KUYAFAHAMU.

1-ANAYEZALIWA NI NANI?

2-NA KWA AJILI YA NANI?


3-NA AFANYE NINI?


>Jambo la kwanza.
Anayezaliwa ni Immanuel.
Isaya 7:14 "Kwa hiyo Bwana mwenywe atawapa ishara .Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli"

NINI MAANA YA IMANUELI?
Mathayo 1:23 "Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani Mungu pamoja nasi.
Kwa mantiki hiyo, anayezaliwa ni Mungu ambaye upenda "USHIRIKA" na wanadamu kwa kusudi la KUSIFIWA NA KUABUDIWA. Neno la linasema..."Tazama, masikani ya Mungu ni pamoja na wanadamu..." Ufunuo 21:3.
Hivyo ujue anazaliwa ni Mungu na anakuja katika NAFSI ya Mwana lakini ni Mungu yule yule mmoja.
Ndipo mtumishi wa Mungu Nabii Isaya akatoa UNABII juu yake Yesu Kristo nakusema....."Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshahuri wa ajabu, Mungu mwenye NGUVU, Baba wa milele, Mfalme wa amani." Isaya 9:6.
Hivyo huyo mtoto alizaliwa na tunashelekea kuzaliwa kwake anasifa zifuatazo
1.MSHAHURI WA AJABU
2.MUNGU MWENYE NGUVU
3.BABA WA MILELE
4.MFALME WA AMANI.

Unapojiandaa kusherekea ujue unamsherekea Muumbaji (MUNGU) wako aliyekuumba wewe na mimi.
Paulo anathibisha maneno ya manabii akisema..."MUNGU ALIDHIHIRISHWA KATIKA MWILI" 1 Timotheo 3:16 Yaani Yesu alizaliwa katika MWILI...Yohana 1:14 "NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, AKAKAA KWETU" ok, "NENO"
ni nani? NENO ni Mungu ambaye ni YESU KRISTO aliyekuwako, aliyeko na atakaye kuwako. Yohana alimumuona YESU KRISTO amevaa vazi lililochovywa katika damu na jina lake aitwa, NENO LA MUNGU. Ufunuo 19:13.

Kwa hiyo tuweke HESHIMA katka kusherehekea si katika UNYAJI POMBE, UASHERATI, UZINZI na kila aina ya uovu maana si kusudi la sikukuu hiyo.
Tunaendelea.....
YESU AMEZALIWA HALELUYA HALELUYA.

By Emmanuel Kamalamo.
 

Comments