AINA ZA MAKANISA


Kanisa siyo jengo kama baadhi ya watu wanavyodhani. Kanisa ni kusanyiko la watu wamwaminio Yesu (Filemoni 1:2), hao wamwaminio Kristo hukutanika kwenye nyumba za Ibada ambazo huitwa Majengo ya Kanisa.
Yesu alivyoondoka aliacha Kanisa, lakini kutokana na sababu mbali mbali Kanisa liligawanyika katika madhehebu mbali mbali. Mwongozo wa Kanisa ni Neno la Mungu ambalo linapatikana ndani ya Biblia. Kwa kutumia kigezo cha jinsi Kanisa linavyoweka kipaumbele kwa Neno, tunaweza kupata Aina tatu za Makanisa, nayo ni kama ifuatavyo:


1. MAKANISA YA KIROHO


Haya ni makusanyiko ya Watu wa Mungu, ambao baadhi ya sifa zao ni hizi zifuatazo:
Wanategemea uongozi wa Roho Mtakatifu. (Rum 8:14)
Wanafuata Neno la Mungu. (2Tim 3:16)
Wanahimiza Utakatifu ndani ya kusanyiko. (1Pet 1:13-16)
Wanakemea dhambi na hawawalei watenda dhambi. (1Kor 5:11)
Huomba kupitia jina la Yesu tu, (Mdo 4:12)


2. MAKANISA YA KIMWILI

Haya ni makusanyiko ya watu waitwao Wakristo/Wakristu ambao sifa zao ni kinyume na sifa za kundi la kwanza, baadhi ya sifa zao ni kama na zifuatazo:
Hawafuati Neno la Mungu, hufuata maagizo ya wazee wao.
Dhambi kwao si tatizo, ilimradi ufanye kitubio.
Walevi hushauriwa siku ya jumamosi wasilewe sana ili kesho yake wasisumbue kwenye misa.
Hupiga magoti na kuabudu vinyago/sanamu.
Jina la Yesu kwao si muhimu, huomba wafu wanaodai ni watakatifu.
Hupinga uwezekano wa mtu kushinda dhambi,
Huridhia viongozi wao kuwa mashoga.
Hudhani mtu huwa Mkiristo kwa kuzaliwa na mzazi Mkristo.
Hudhani mtu aliyekufa dhambini na kutupwa motoni, ikipelekwa fedha kwa kiongozi wa dini anaweza kuomba na hukumu ya Mungu ikabatilishwa! N.k.


3. MAKANISA YANAYODHANIWA KUWA YA KIROHO

Hili ni kundi la waamini ambalo mtu asiyejua Neno, anaweza kudhani ni ya kiroho lakini kumbe siyo, nayo yana sifa zifuatazo:
Hutumia Biblia, lakini msingi wao si kutafuta ufalme wa Mbingu kwanza.
Viongozi huwafundisha wafuasi wao kuwategemea wao badala ya kumtegemea Yesu,
Huwafundisha wafuasi wao kuhusu mafanikio ya mwilini tu na hawana muda kufundisha toba ya kweli, hukumu ya Mungu wala Utakatifu.
Hupenda kutukuzwa na mara nyingi hujipa sifa na vyeo wasiokuwa navyo.
Wafuasi wao hawana badiliko lolote katika roho zao, tabia zao huwa sawa na za wasiomjua Mungu.

YESU ANARUDI!
By Emmanuel Bubelwa.
Mimi nimejifunza kitu, wewe je?

Comments