CHANGAMOTO ZA KUOA AU KUOLEWA KWA MARA YA PILI NA MTU MWINGINE (REMARRIAGE)

Na Mchungaji Peter Mitimingi,  Huduma ya VHM.

1. Muda Muafaka wa Kuoa au Kuolewa Tena Baada ya Kutengana na Mwezi wako wa Kwanza.
Inashauriwa kwanza kwa wanandoa walioachana au kutengana na hasa kwa migogoro kuchukua muda angalau kuanzia mwaka mmoja kabla ya kuanza kufikiria mambo ya kuoa au kuolewa tena. Hii itasaidia kuponya vidonda vya majeraha ya aliyepita pia itasaidia kutuliza akili na kufanya maamuzi yenye kina, hekima na busara. 


2. Usifanya Haraka Haraka Kuoa au Kuolewa Mara ya Pili
Kuharakisha kuoa au kuolewa kwa muda mfupi kutaongeza matatizo juu ya matatizo. Yale matatizo uliyoyakimbia kule yanaweza kujirudia mara tatu zaidi ya yale uliyo kuwanayo hapo kwanza na mwenzi wako wa nyuma. Pia inaweza kuwa hatari kwa watoto wako maana kutokana na vidonda vya majeraha ya nyuma ya mwenzi wako, atayaleta kwako wewe na watoto ambao hawana hatia wala mahusiano na majeraha na madonda hayo.

Changamoto za Watu Wawili Waliotengana na Wenzi wao Wanapokutana na Kuamua Kuoana
Ndoa ya watu wawili waliokuwa wametengana kila mmoja na mwenzi wake na kukutana na kuamua kuoana, huwa na matatizo na changamoto nyingi kuliko zile walizoziacha kwenye ndoa ya kwanza. 


Baadhi ya Sababu Zinazosababisha Ndoa hii Kuwa Ngumu zaidi Kuliko zile walizo ziacha kwa Wenzi wao

i. Kila mmoja tayari anayo majeraha na makovu ya madonda aliyoumizwa huko alikotoka.
Kama mtu huyu hakupitia kile kipindi cha kutibu na kupona majeraha kabla ya kuanza mahusiano mapya na mwenzi mpya, basi ni wazi kwamba madonda na majeraha ya mwenzi huyu yataendelea kumtesa huyu mwenzi mpya.


ii. Uvumilivu wa kuvumilia ndoa ya pili huwa ni mdogo sana kulinganisha na nguvu ya kuvumilia changamoto ya ndoa ya kwanza.
Nguvu nyingi ya uvumilivu inakuwa imeishia kwenye ndoa ya kwanza iliyoshindikana. Kwenye ndoa ya kwanza mtu anaweza kumvumilia mwenzi wake kwa muda mrefu sana na kutumaini kwamba kuna siku labda huenda mwenzi wake akabadilika na mambo kuwa mazuri. Uvumilivu huu unapofikia kikomo hapo ndipo matengano huweza kutokea na mtu huyu alienda kwenye ndoa nyingine kwenye mfuko wa akiba ya uvumilivu kunakuwa kumeishiwa kabisa kiasi kwamba anakuwa hana uvumilivu tena kama ule aliokuwa nao kwenye ndoa ya kwanza.


iii. Uzoefu wa Ndoa ya Kwanza Unakuwa Umemjengea Sugu ya Jeuri na Kiburi
Kila mmoja anapoingia kwenye ndoa ya mara ya pili, anakuwa na sugu kwamba usinisumbue ukinikorofisha tutaachana kama tulivyoachana na yule wa kwanza. Nikiachana na wewe haitakuwa mara ya kwanza hata kama jamii watasema weseme tu walishasema nimezoea.


iv. Mwenzi Aliyeachana naye Huchukuliwa kama Kioo na Fimbo kwa Mwenzi Mpya
Ndoa iliyopita huchukulia kama kioo cha kulinganisha mwenzi aliyepita na wa sasa na hasa yanapojitokeza matatizo kwa mwenzi mpya, ni rahisi sana kutolea mfano mwenzi aliyepita alivyofanya vizuri katika eneo fulani fulani kuliko huyu mpya na hii huwa ni kama msumari wa moto kwenye kidonda cha huyu mwenzi mpya anayepewa mazuri ambayo mwenzi aliyemuacha alikuwa akiyatenda. 


v. Kuendelea na Mawasiliano na Mahusiano na Mwenzi Aliyepita kunaweza kubomoa Ndoa hii Mpya.
Kuendelea kuwa na mahusiano na mwenzi aliyepita huwea kuleta wivu, chuki, mgongano na mafarakano kwa mwenzi mpya. Wakati mwingine kwasababu mmoja alipata watoto na mwenzi waliye tengana naye, kwasababu ya wale watoto wanabaki kuwaunganisha kwajili ya mahitaji mbalimbali mume na mke wa zamani wanajikuta wakiwasiliana na kupanga mipango kwajili ya watoto wao wanakuwa kama kiunganishi kwao. Hali hiyo huweza kuleta matatizo na migogoro mingine tena kwa ndoa hii mpya kwasababu ya huo mwingilianao. Kama hakutakuwa na uwazi na maelewanao katika kuhusiana na mzazi mwenza mliyetengana naye, basi huweza kupelekea maisha magumu ya ndoa hii mpya na hata kuifanya kuvunjika pia.

Huduma ya Ushauri zinapatikana kwa "appointment" maalumu na kuna changizo kidogo kwa huduma hii ambayo inatolewa na Mwalimu Mitimingi p
A pastor, Teacher and a Professional Counseling Psychologist

Comments