DALILI 7 ZA NDOA INAYOELEKEA KUVUNJIKA...

Na Mchungaji Peter Mitimingi ambaye pia ni mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministry(VHM)

1. Wakati wanandoa wanapokuwa hawaongei tena kila mmoja kwa mwenzake. (Partners no longer talk to each other).

2. Wakati wanandoa hawaonyeshi tena matendo ya mapenzi kama vile Kukumbatiaana, kushikana mikono, kumbusu mwenzi wako, na kuonyesha kumjali mwenzi wako. (They no longer hold hands, kiss, or careless).


3. Wakati ambapo maisha ya tendo la ndoa yanakuwa ya kuchoshana na hayana radha. (Their sex life is boring).



4. Wakati ambapo kila mazungumzo yao huishia kwenye kugombana na kununiana. (Every discussion or disagreement escalates into a major fight).


5. Wakati kila mmoja anampuuzia mwenzake na kuona hana mvuto tena. (They take each other for granted and no longer take time to look attractive).


6. Wakati ambapo wanandoa hao huachia wanandugu, watoto na hata vitu kama kazi, biashara, kuchukua nafasi kubwa ya mapenzi ya wanandoa hao. (They let other people (relatives, children, or even things like jobs) come between them).


7. Wakati wanandoa hawafanyi tena mipango pamoja, kila mwanandoa kivyake vyake. (They no longer do things together any more).
Kama ukiona kuna dalili hizo katika ndoa yako basi anza kuchukua tahadhali.


Pia ushauri wa ndoa (Marital counseling) unapatikana kwa gharama nafuu wasiliana nami kwa 0713 18 39 39

Comments