FRORA MBASHA: DVD MPYA YA NIPE NGUVU YA KUSHIDA SASA IKO MADUKANI


Mungu amekuwa mwema kwangu tangia nilipomkubari kuwa mwokozi wangu na
nguzo yangu. Nimeona Mungu akinishindia na magumu ninayopitia na
niliyoyapitia katika maisha yangu. Nimeona Mungu huyu unayemwabudu kila
siku akinivusha na kunitia moyo pale ninapoona akili yangukufikiri jinsi
ya kutatua yale yaliyombele yangu. Mungu huyu ni waajabu kwangu,
kaniwezesha katika uaandaji wa albamu hii mpya ya "NIPE NGUVU YA
KUSHINDA". Nazidi kumshangaa Mungu huruma zake na fadhili zake kwangu.



Flora Mbasha

Ninaamini hata wewe unaweza kufarijika na kuinua imani yako kwa
kusikiliza ujumbe ulio ndani ya DVD hii. Mungu wangu anataka kuongea na
wewe kwa kupitia uimbaji wangu. Ni maneno ya Mungu ambayo ameweka ndani
yangu kwaajili ya kuponya na kuinua imani yako kwa njia ya uimbaji.
Kwangu ni vigumu mno kukufikia na kukuhubiria habari njema, lakini kwa
kupitia DVD hii utaweza kuungana nami na kupata Neno la Mungu.

Flora Mbasha Nipe Nguvu ya Kushinda

Ndugu mpendwa wangu, ninatambua unatamani sana kushinda magumu yaliyoko
mbele yako na haya unayopambana nayo, na umekuwa ukijiuliza nitafanya
nini? Lakini natamani kukutia moyo na kukuomba uzidi kuwa magoti mwa
Mungu wetu kila kuitwapo leo. Acha kusikiliza maneno ya watu
wanaokusemea mabaya ila msikilize Mungu wako naye atakutia nguvu.

Nyimbo zilizomo humu zitakusaidia sana katika maisha yako haya. Mungu akubariki sana.



Flora Mbasha Nipe Nguvu ya Kushinda

SIKILIZA WIMBO WA NIPE NGUVU YA KUSHINDA

Comments