FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI


Na Godfrey Miyonjo.
“Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” MATHAYO 16:19.
BWANA YESU asifiwe.
Inajulikana duniani kote kuwa funguo ni kifaa kinachotumika kufungulia vitu mbalimbali vilivyofungwa.
Kila ufunguo huwa una mahala pake maalumu pa kufungulia, ikiwa ni gari, kufuri, pingo, N.K.
Katika ilimwengu war oho yapo mambo ambayo hufungwa na kufunguliwa kama ilivyo katika ulimwengu wa damu na nyama.
BWANA YESU analijua hilo ndiyomaana ametupa funguo za ufalme wa mbinguni ili tuweze kufunga na kufungua mambo mbalimbali katika ulimwengu wa roho.
Isidhaniwe kuwa FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI zina umbo rasmi kama zilivyo funguo mbalimbali katika ulimwengu wa mwili.
Imeandikwa “mambo ya rohoni yatambulikana kwa jinsi ya rohoni”
Usije ukapoteza muda kwa kutafuta funguo za makufuri mabovu, magari chakavu au yale yaliyo mazima na kwenda nazo ibadani/kwenye maombi/maombezi, eti ukafanye tendo la imani ili ufungue mambo yako yaliyofungwa katika ulimwengu wa roho.
Huu ni uchanga wa kiroho na ni ushamba pia, kwakuwa katika ulimwengu wa roho hakuna kitu kama hiki.
Na mtu yeyote afanyaye mambo ya jinsi hii hana tofauti na Yule atengenezaye sanamu na kuiabudu.

BWANA YESU aliposema “Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” hakumaanisha kuwa eti tutakavyotaka kutumia hayo mamlaka tuwe tunatafuta funguo za magari, mapingo, makufuri, N.K ili kufungua mambo yetu.
BWANA YESU aliyasema hayo akitupatia mamlaka katika ulimwengu wa roho kufunga na kufungua mambo mbalimbali kupitia ndimi zetu (maneno ya vinywa vyetu).
Kwa maana imeandikwa “Mauti na uzima huwa katika uweza wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake” MITHALI 18:21
Imeandikwa “Kwakuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki (utafunguliwa); na kwa maneno yako utahukumiwa (utafungwa)” MATHAYO 12:37.
Mahala pengine Bibkia inasema umefungwa kwa maneno ya kinywa chako.
Hapo ndipo kila mwenye mwili anapaswa kujua kuwa hizo FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI tulizopewa na BWANA YESU utendaji wake huwa katika kutamka, yaani tunapotamka juu ya kufungua jambo flani katika ulimwengu wa roho hufunguka, na tunapotamka kufunga jambo flani hufungika katika ulimwengu wa roho.
Utendaji kazi wa hizo FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI huambatana na matamshi/maneneno yetu (kwa wale tuliomwamini YESU).
Wewe ambaye bado haujamwamini YESU FUNGUO hizi hazikuhusu, hivyo ingekuwa heri kama ungeamua kumwamini leo ili nawe upate funguo.
Hivyo ingekuwa heri kama kila mmoja wetu aliyemwamini YESU kutambua kuwa yeye anazo fungu, na anao uwezo wa kufunga na kufungua mambo mbalimbali katika ulimwengu wa roho.
Baada ya kulijua hilo kila mmoja wetu na aingie kwenye maombi yeye mwenyewe kufungua mambo yake yote anayohisi kuwa yamefungwa, na afunge yale yote mabaya yaliyofunguliwa kwake.
MFANO WAwEZA OMBEA
Afya yako
Elimu yako
Ndoa yako
Kazi za mikono yako
Uchumba wako
Huduma yako
N.K.

Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaa…………………………………!
CHUKUA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI, ILI UFUNGE NA KUFUNGUA MAMBO MBALIMBALI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
MUNGU akubariki sana.
By Godfrey Miyonjo.

Comments