HAZINA YA MOYO

Na Godfrey Miyonjo.


“Mtu mwema katika HAZINA NJEMA YA MOYO WAKE hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake” LUKA 6:45.

BWANA YESU asifiwe,

Hazina ya moyo ni vitu ambavyo mtu amevihifadhi ndani ya moyo wake, vitu hivyo vyaweza kuwa vyema au viovu.
Kila Neno alisemalo au tendo alitendalo mwanadamu linatokana na hazina yake ya moyo ilivyo.

Kuna watu ama kwa kujua au kwa kutokujua wamejiwekea hazina mbovu ndani ya mioyo yao, na kwa hazina zao mbovu walizojiwekea hutoa yaliyo maovu.

Yaani kwakuwa ndani ya mioyo yao wamejaza uzizni, hata wanazini kila iitwapo leo, wamejaza matusi, hata wanatukana kila leo, wamejaza mawazo mabaya ya kutaka kuonesha maungo yao ya siri, hata wanavaa nusu uchi, N.K.

Ninayasema haya kwasbabu imeandikwa “Mtu mwema katika akiba njema hutoa yaliyo mema, na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya” MATHAYO 12:35.

Watu wengi huwa tayali hata kufa kwa kutetea uovu, kwasababu uovu umejaa ndani ya mioyo yao, 

Nao hufanya hivyo kwasababu ndivyo yasemavyo maandiko.
Yaani : “Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko na mpumbavu katika upumbavu wake” MITHALI 17:12.

Mpumbavu (aliye na hazina mbovu ya moyo) huwa ni vigumu sana kumwondoa katika upumbavu wake.

Lakina Yesu pekeyake ndiye aliye na uwezo wa kuondoa hazina zote mbovu zilizo ndani ya mioyo ya wanadamu. 

Yesu katika mwaliko wake wa mbinguni atawakribisha wale tu walio na hazina njema ndani ya mioyo yao.

Ndiyo maana alipokuwa akifundisha alitoa mfano huu:
“Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona aliificha na kwa furaha yake akaenda akauza alivyonavyo vyote akalinunua shamba lile” MATHAYO 13:44.

Ili mtu aurithi ufalme wa mbinguni lazima auze kwanza hazina yake yote ya moyo ile iliyo mbovu (atubu) kisha anunue shamba (ufalme wa mbinguni) kwa kumwamini YESU kama BWANA na Mwokozi wa maisha yeke.

Mtu yeyote akiamua kuuza vyote alivyonavyo na kuamua kulinunua hili shamba (ufalme wa mbinguni) hakika atakuwa na hazina njema ndani ya moyo wake, na atakuwa na sehemu katika ufalme wa mbinguni.

Kamwe hatatamani tena kuvaa hovyo (mavazi yasiyompa Mungu utukufu), hatatamani tena ulevi, uzinzi, ujambazi, utukanaji, N.K.
YESU anataka kila mmoja auze hazina mbovu (zisizo na thamani kwa Mungu) alizonazo leo, ili amiliki shamba lililo na hazina njema iliyositirika (iliyojificha).
Ewe ndugu unayesoma huu ujumbe Ninasemaaaaaaaaaa…………………………………………………….!
UZA HAZINA MBOVU ZA MOYO WAKO ULIZONAZO, ILI UWE NA UHAKIHA WA KUMLAKI BWANA YESU MAWINGUNI.
Asomaye na afahamu
By Ev.Godfrey Miyonjo.

Comments