HOFU YA MUNGU

Na Godfrey Miyonjo.
“Ibrahim akasema , kwa sababu naliona, Yamkini hapana HOFU YA MUNGU mahala hapa, nao wataniua kwasababu ya mke wangu” MWANZO 20:11.
BWANA YESU asifiwe.
Ninamtukuza Mungu kwa upendeleo alionipa hata nikaiona siku ya leo, kwa maana sikufanya jambo jema ambalo lingenifanya nifike siku ya leo.
Atukuzwe Mungu anayetuwazia mema kila iitwapo leo, leo kwa Neema na rehema zake imempendeza tushirikiane katika kujifunza Neno lake ambalo ndilo uzima wetu.
Watu wengi hudhani kuwa, kuwa na HOFU YA MUNGU ni kuhubiri, kuimba kwaya, kushuhudia nyumba kwa nyumba, kutoa sadaka, kukemea mapepo, kuhudhuria ibadani, N.K, kitu ambacho siyo kweli.
Kutokana na dhana walizonazo watu wengi katika vichwa vyao huwapelekea kufanya vitu ambavyo kimsingi havina faida yoyote kwao.
Unakuta mtu anahubiri, anafunga, anaomba, anaimba kwaya, anatoa sadaka, N.K, lakini ndani ya moyo wake anashuhudiwa kabisa kuwa yeye ni mpagani/haishi sawasawa na Neno la Mungu.
Kutokana na kutokuwa na HOFU YA MUNGU na kujiepusha na uovu mtu huyo anafanya kazi ya bure (kazi isiyo na faida),
Imeandikwa “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali name, Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu” MATHAYO 15:8-9.
Hofu ya Mungu ni hali ya utii na unyenyekevu aliyonayo mtu ndani ya moyo wake.
Hali hiyo humpelekea mtu kuishi sawasawa na Maagizo ya Mungu/Neno la Mungu.
Yaani HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuyajua yale yampasayo kutenda na yasiyompasa kutenda.
HOFU YA MUNGU humfanya mtu kuishi MAISHA HALISI, Yaani kutokuishi maisha ya maigizo.
Mtu aliye na HOFU YA MUNGU kila jambo analolifanya ni halisi kwake, ikiwa ni kutumika mbele za Mungu ni kiuhalisia, anapofanya ibada mbele za Mungu ni ibada halisi. YOHANA 4:23-24.
Hafanyi jambo kwa kufuata mkumbo tu, kama wasio na HOFU YA MUNGU wafanyavyo,
Kwa maana Wasio na HOFU YA MUNGU hufutata mkumbo, huwa hawaishi MAISHA HALISI, huwa anaigiza daima, humkiri Mungu kwa midomo tu, ila ndani ya mioyo yao huwa hawana mapatano kabisa na Mungu/Wamefarakana na Mungu.
Mtu asiye na HOFU YA MUNGU hufanya jambo kutokana na hofu ya wanadamu, hali au mazingira.
Hata kama anafanya ibada, anaimba, anatoa sadaka, anahubiri, N.K ni kutokana na mazingira tu, Yaani anafanya ili aonekane na watu kuwa nay eye anafanya.
Ndani ya moyo wake huwa na mambo haya: “nisipofanya hivi flani atanionaje?” “nisipofanya hivi nitatengwa na jamii”, “nisipofanya hivi nitafukuzwa kazi”, “nisipofanya hivi watoto wangu watakufa na njaa” “nisipofanya hivi sitaoa/sitaolewa”, N.K.
Mtu hajiulizi kuwa Mungu atanionaje, anajiuliza juu ya watu na mazingira.
Mungu huchukizwa sana na watu wa jinsi hii, wasio na HOFU YA MUNGU badala yake wanakuwa na hofu ya wanadamu, ndiyo maana anasema:
“Mimi, naam, mimi ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayeffanywa kuwa kama majani?” ISAYA 51:12.
Yaani imezoeleka mitaani kuona wachawi wakiogopwa kuliko Mungu,
Imezoeleka kuona kiongozi wa dini/siasa anaogopwa kuliko Mungu.
Mtu yupo tayari kunyenyekea chini ya mkono wa mwnadamu kuliko knyenyekeza chini ya mkono wa Mungu.
Yupo tayari kutekeleza maagizo ya mwanadamu (kiongozi wa dini/siasa, mganga) kuliko maagizo ya Mungu.
Hayo yote huwa hivi kwasababu watu wengi wamekataa ndani ya mioyo yao kuwa na Mungu, watu hawataki kufungua mioyo yao ili wapate kujifunza habari za UFALME WA MBINGUNI.
Wamekataa kuwa na ufahamu ndani ya mioyo yao, wameamua kujilisha vitu visivyofaa,
Imeandikwa: “Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu” MITHALI 15:14.
Je! Wewe nawe u miongoni mwao?
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaa……………………………………………!
Ni heri uamue kutubu leo, kwa maana siku ile ya ajabu na ya kutisha imekaribia sana, kumbuka kuwa imeandikwa:

“Naye aliye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa Atakimbia uchi siku ile asema BWANA” AMOSI 2:16.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu)

Comments