HUDUMA YA MAOMBEZI NI HUDUMA YA BURE.

Na Godfrey Miyonjo.

“Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE TOENI BURE” MTHAYO 10:8.
BWANA YESU asifiwe sana,
Ndugu zangu nataka kila mmoja wetu atambue kuwa hakuna mahali popote katika bibliapanapotutaka tutoe malipo ya aina yoyote ile ili tuombewe.
Gharama yote ya uzima wetu alishatulipia BWANA YESU pale msalabani.
Kwa kupigwa kwake sisi tumepona ISAYA 53:5.
Gharama pekee kwetu sisi kwa sasa ni kutubu dhambi zetu tukimaanisha kuziacha, na kuamua kuishi maisha matakatifu, hakuna kingine.
Katika kipindi hiki cha mwisho kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana, watu waliojiingiza kwa siri wamekuwa wakilitumia vibaya jina la Yesu kwa maslahi yao binafsi.
Wamekuwa wakijitungia mambo ambayo hayapo kimaandiko,
Niliwahi kufundisha somo lenye kichwa cha somo kisemacho
“USIWE MWEPESI WA KUTOATOA SADAKA KWA KILA MADHABAHU, MADHABAHU ZINGINE NI MADHABAHU ZA SHETANI”.

Niliyasema hayo ili nikutahadharishe ndugu yangu kutokana na udanganyifu uliopo katika siku hizi za mwisho,
Kuna waongo huwadanganya watu watoe sadaka ya ukombozi, sijui sadaka ya kuvunja maagano/kuvunja mikataba, N.K,
Hii ni roho ya upotevu ambayo inatenda kazi sasa, na imekwisha kuwapoteza wengi,
Kwa maneno ya kinywa chake mwenyewe BWANA YESU aliwaagiza wanafunzi wake kuwa “MMEPATA BURE TOENI BURE”
Tupo mwishoni mwa mwaka, najua watumishi wa uongo wamesha jitungia sada za uongo nyiingi, sijui sadaka za kuuteka mwaka, sadaka kwa ajili ya afya yako na watoto wako, sadaka ya bajeti yako ya mwaka mzima, N.K,
Ndugu inawezekana ni kweli huwa unafanikiwa katika mambo yako baada ya kuyatekeleza hayo maagizo ya viongozi wa dini, lakini yakupasa ujiulize kuwa hayo uyafanyayo yapo kimaandiko?
Ukiona kuwa ni uzushi wao tu ni bora ukachukua hatua,
MWENYE MASIKIO YA KUSIKILIA NA ASIKIE.
MUNGU akubariki.
By Godfrey Miyonjo.

Comments