HUU NI MWAKA 2015 ANGALIA TAFSIRI YA NAMBA 15 KIBIBLIA

Na Mchungaji Peter Mitimingi wa The Voice of Hope Ministry(VHM)

Namba 15 kibiblia ni namba ya PUMZIKO na MWELEKEO MPYA. It is a number of REST and NEW DIRECTION
1. Namba 15 kibiblia inawakilisha PUMZIKO (rest) ambayo huja mara baada ya siku ya ukombozi ambayo huwakilisha na namba 14.

2. Siku ya 15 ya mwezi wa kwanza wa Kiebrania (Nisa) ni siku maalum ya mikate isiyotiwa chachu.
(Mambo ya Walawi 23:6,34).

3. Ni siku ya kupumzika kwa watoto wa Israel.
4. Mfalme Hezekia aliongezewa miaka 15 ya kuishi tena ikiwa ni mwelekeo mpya wa maisha yake baada ya kupona kifo. (2Wafalme 20:1-6).
5. Ilikuwa ni Mwaka wa 15 wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, ambapo huduma ya Yohana Mbaatizaji ilipoanza rasmi. (Luka 3:1-3).
6. Kuna ahadi 15 kwa Wakristo ambazo zimetajwa katika kitabu cha Injili ya Mathayo.
i. Ahadi ya ufalme wa mbinguni (Mathayo 5:3)
ii. Tutajazwa na haki yake (5:6)
iii. Tutamwona Mungu (5:8)
iv. Tutaitwa wana wa Mungu (5:9)
v. Yesu ameahidi kutukiri mbele ya baba Mungu (10:32)
vi. Tutapewa Pumziko (11:29)
vii. Mungu atatufanya kuwa sehemu ya familiya yake (12:50)
viii. Tutabadilishwa na kuwa kama watoto wake ili tuurithi uzima wa milele (18:3)
ix. Atatufanya kuwa wakuu katika ufalme wake (18:4)
x. Tutapata uwezo wa kumpokea Kristo (18:5)
xi. Tukikubaliana duniani Mungu atatufanyia kutoka mbinguni (18:19)
xii. Kristo atakuwa pamoja nasi (18:20)
xiii. Tutaokolewa (24:13)
xiv. Tunamtumikia Yesu kwa kuwatumikia wengine (25:40)
xv. Yesu siku zote hatatuacha atakaa nasi (28:19)

7. Hosea alimnunua mwanamke kahaba kwa vipande 15 vya fedha. Ilikuwa Mungu anaonyesha mwelekeo mpya kati yake Mungu na taifa la Israel lilikokuwa linafananishwa na yule mama kahaba. (Hosea 3:1-5)
8. Yakobo alimtumikia Laban miaka 14 kwajili ya binti zake ilikuwa ni mwaka wa 15 alipokuwa huru kutoka katika deni la binti za Labani (Mwanzo 31:41).
9. Wayahudi wa Shushani walikusanyika siku ya kumi na tano ya mwezi huo wakapumzika, wakaifanya kuwa siku ya karamu na furaha. (Esta 9:18)
10. Nawe nakuombea kuwa mwaka 2015 uwe mwaka wa kupumzika na kufanya karamu na kufurahi. Uwe mwaka wa utakaopata mwelekeo mpya wa maisha yake yenye baraka na mafanikio makubwa.

Comments