IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYETOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO. NA INAVYOTENDA KAZI


Bwana Yesu asifiwe.!
Ni furaha yangu katika Roho Mtakatifu kupenda kuujenga mwili wa Kristo katika mafundisho.
Mungu anapoweka kitu ndani yako ni kwa ajili ya kulijenga kanisa lake. Sifundishi ili watu wajue nafahamu kufundusha la asha! Bali nafundisha ili watu wamjue Kristo kupitia MAFUNDISHO nayopewa na Roho Mtakatifu.

Na Emmanuel Kamalamo.
Mara nyingi wakristo wengi wameshindwa kujua WITO WA HUDUMA zao. Na baadhi kuingia katika huduma ambazo hawakuitwa katika wito huo na hatimaye kuona kazi ya Mungu ni ngumu.
AINA ZA HUDUMA.
Kuna aina tano za Huduma zinazotenda kazi katika mwili wa Kristo.
1.MITUME
2.MANABI
3.WAINJILISTI
4.WACHUNGAJI
5.WAALIMU. (Waefeso 4:9-12)
Majukumu ya Huduma hizi ni kuwakamilisha WATAKATIFU (WALIOOKOKA) ili na wao washiriki kudanya kazi ya Mungu kwa karama na vipawa anavyokirumiwa na Roho Mtakatifu.

JE HUDUMA USOMEWA KATIKA VYUO AU KUPEWA
NDANI YA KANISA?

Jibu ni hapana. Huduma haisomewi wala haipewi na mtu ndani ya kanisa. Bali Mungu ndiye uumpa mtu Huduma. Nabii Yeremia alipewa Huduma ya KINABII kabla hajaumbwa wala kuwekwa tumboni, maandiko yanasema..."KABLA SIJAKUUMBA KATIKA TUMBO NALIKUJUA, NA KABLA HUJATOKA TUMBONI,NALIKUTAKASA; NIMEKUWEKA KUWA NABII WA MATAIFA" ( Yeremia 1:5)
Kabla Yeremia hajaumbwa alikuwepo katika mawazo ya Mungu na kazi atakayopewa, lasivyo Mungu asingesema..."KABLA SIJAKUUMBA KATIKA TUMBO" maana yake Yeremia alikuwepo na Mungu alimjua. Na alipoingizwa tumboni alitakaswa. Nini maana ya "KUTAKASWA" Kutakaswa maana yake...."KUTENGWA KWA AJILI YA KUSUDI MAALUMU"
Wapo pia waliopewa Huduma tangu tumboni kama vile YOHANA MBATIZAJI (Luka 1:15) ,SAMSONI (Waamuzi 13:5), SAMWELI ( 1 Samweli 1:11)

Ndiyo maana waliopewa HUDUMA tangu tumboni wanapoitwa wanakataa, Mungu huwa anafunga KUFANIKIWA KWA KAZI ZA MIKONO YAO lengo waje kwenye HUDUMA. Na wanapotii nakuingia kwenye Huduma eidha UTUME,NABII,UINJILISTI,UCHUNGAJIA AU UALIMU ndipo Mungu uwabariki.
VYUO SI SAHIHI?
La asha! Ni sahihi. Vyuo vina waalimu ambao Mungu uwatumia hao kuwaandaa watumishi walipewa huduma ndani yao na jinsi ya kuitumia huduma na si kukupa huduma, anayetoa Huduma ni Mungu....."ALIPOPAA JUU BALITEKA MATEKA, ALIWAPA WANADAMU VIPAWA.....NAYE ALITOA WENGINE KUWA MITUME; NA WENGINE KUWA MANABII; NA WENGINE KUWA WAINJILISTI; NA WENGINE KUWA WACHUNGAJI; NA WAALIMU" (Waefeso 4:8,11)
Wanafunzi wa Yesu walifundishwa na Yesu Kristo mwenywe.. Paulo alipoitwa alikaa chini ya Anania na wanafunzi wengini pia na Mitume.(Mdo 9:17,27) Paulo kukaa kwa mitume alikuwa anapewa msingi ulio imara katika Kristo.
Inaendelea.

Comments