KUMKATAA YESU NI KUKATAA UZIMA WA MILELE.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu kwa lengo la kujifunza habari za ufalme wa MUNGU.
Yohana 3:19-21 ''Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU. '' 
BWANA YESU ndiye Nuru iliyokuja ulimwenguni ili kuwatoa wanadamu kwa shetani ambako ni gizani. Lakini wanadamu walio wengi wamependa giza kuliko Nuru na hiyo ndiyo hukumu itakayowapata kwamba Nuru imekuja kuwaokoka lakini wanadamu wakapenda giza kuliko Nuru.
Ndugu zangu hakuna kwingine kokote ambako mwanadamu anaweza kupitia ili aende uzima wa milele ila ni kwa YESU tu(Matendo 4:12, Yohana 14:6). Hakuna uzima wa milele popote ila kwa YESU KRISTO ndiposa tunasema kwamba KUMKATAA BWANA YESU NI KUKATAA UZIMA WA MILELE.
Ngoja nikuambie neno hili ndugu yangu    ''Wadhalimu Watarejea Kuzimu, Naam, Mataifa Yote Wanaomsahau MUNGU.-Zaburi 9:17'' 
-Ndugu Mataifa Ni Wewe Hivyo Kama Umemsahau MUNGU Na Haumhitaji Maishani Mwako Basi Una Hasara Kubwa Maana Waovu Wataenda Motoni.
- Siku Ya Mwisho Malaika Watakusanya Waovu Wote Na Kuwatupa Jehanamu(Mathayo 13:41-42, Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi, na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.).
- Ndugu Tunapohubiri Habari Za YESU Tunakuwa Tunahubiri Habari Njema Za Ufalme Wa MUNGU. 
-Kama Unaakili Ndugu Tubu Kwa YESU Leo Ili Jina Lako Liandikwe Kwenye Kitabu Cha Uzima(Mathayo 3:2, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. ).  
-Ndugu Wasiomcha MUNGU Wataenda Jehanamu(2 Petro 3:7, Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha MUNGU.
-Ndio Maana BWANA YESU Anakuambia Mkono Wako Au Mguu Ukikukosesha Na Kukufanyish Dhambi Ni Heri Kuukata, Maana Heri Kuingiza Uzima Wa Milele Huna Mkono Na Miguu Kuliko Kwenda Jehanamu Na Viungo Vyako Vyote(Mathayo 18:8-9, Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto. ). 
-Ndugu, Mikono au miguu au macho yanayotajwa hayana maana kwamba ni viungo vya mwili wako ila maana yake ni kwamba jambo lolote au tabia yeyote usikubali ikakukosesha uzima wa milele. Kuna watu ulevi imekuwa nndio mikono yao ambayo inatakiwa kukatwa maana wakiendelea na ulevi wataishia jehanamu. Kuna mtu mmoja aliniambia kwamba anaweza kuacha dhambi zote ila uzinzi hawezi kuacha maana amejaribu hakuweza, uzinzi umekuwa miguu ambao unatakiwa ukatwe ndipo apate nafasi ya kumpendeza MUNGU. Kuna watu hawawezi kuacha uongo, matusi, uasherati, uchawi, kuseng'ng'enya, wizi na kila aina ya dhambi na mambo hayo wakiendelea yao yatawapeleka kubaya sana. Ndugu yangu unayeteswa na dhambi na unadhani huwezi kuacha nakuompa okoka upya na waza mbingungi, waza uzuri wa uzima wa milele na sio dhambi hiyo. Tambua ukifa kwenye dhambi hiyo hutaenda mbinguni, ni hatari sana.

Ni Wakati Wa Kutubu Na Kurejea Kwa BWANA YESU(Matendo 3:19, Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; ). 

Ni Heri Kuwa Mwenye Haki Leo Ili Siku Ile Usiende Motoni(Mathayo 25:46,Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele. ). 
-MUNGU Kakupa Kuishi Leo Ili Tu Utubu. BWANA YESU Yuaja Na Kila Jicho Litamwona(Ufunuo 1:7, Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. ).
- BWANA Anawapenda Wampendao. 
-BWANA YESU yuaja na kama umeshupaza shingo basi hakika utaangamia,  Kwa walioshupaza shinda, Mwenye Kudhulumu Na Azidi Kudhulumu, Mwenye Kufanya Uzinzi Na Aendelee Na Uzinzi Wake, Muongo Na Mchawi Waendelee Na Ubaya Wao, Wenye kufanya dhambi na wazidi kufanya dhambi Na Mwenye Kujitakasa Na Azidi Kujitakasa Sana. BWANA YESU Yuaja Ili Kumlipa Kila Mwanadamu Sawasawa Na Matendo Yake Yalivyo. Huu Ni Wakati Wa Kutubu Na Kuacha Dhambi.BWANA YESU yuko tayari siku zote kuwapokea wale wanaotubu.
Ufunuo 22:11-12 '' Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments