KUNA TIKETI MBILI(2) ZA KUINGIA MBINGUNI.

Na Mtumishi Alex Simion Makuli
 Bwana YESU asifiwe. 
Mbinguni hutaingia kwa sababu ya dhehebu lako zuri, mbinguni hataingia kwa ujanja ujanja, mbinguni tunaingia kwa tiketi 2 tu. 
 -Tiketi ya 1 ni "KUMWAMINI YESU"
-Na tiketi ya pili(2)ni "UTAKATIFU". 

YESU KRISTO ndio njia/tiketi namba 1 ya kuingia mbinguni. "YOH 3:16 KWA MAANA JINSI HII MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU HATA AKAMTOA MWANAE WA PEKEE, ILI KILA MTU AMWAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE".

 "YOH 3:5 YESU akajibu Amin amin nakuambia mtu asipozaliwa kwa maji na Roho hawezi kuingia ufalme wa MUNGU". 
Ndugu mpendwa mbali na KRISTO YESU hakuna mbingu, baadhi ya watu wanajifariji kwamba ooh dhehebu langu ni zuri sana, dhehebu halimpeleki mtu mbinguni, dhehebu bila YESU ni bure. 
YESU anasema "YOH 14:6 MIMI NDIMI NJIA NA KWELI NA UZIMA, MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI". YESU pekee ndiye njia/tiket ya kutufikisha mbingun mbali na hapo ni kupoteza muda. 

 "UTAKATIFU". Utakatifu ni tiketi namba mbili(2) ya kuingia mbinguni. Mkristo anapomwamini YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake kinachofuata ni kujifunza Neno la MUNGU ambalo litamsaidia kuishi maisha matakatifu.
 Ili upate nafasi mbinguni lazima uwe mtakatifu, maana hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia ktk uzima wa milele. Biblia inasema wenye dhambi wote sehemu yao ni ktk lile ziwa liwakalo moto na kiberiti yaani "Jehenamu" (UFUNUO 21:8). 
 Je duniani kuna watakatifu?. Ndio duniani kuna watakatifu. "ZABURI 16:3 WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI NDIO WALIO BORA, HAO NDIO NILIOPENDEZWA NAO". 
MUNGU mwenyewe anadhibitisha kuwa duniani kuna watakatifu. Lakin kuna baadhi ya watu wanasema kuwa duniani hakuna watakatifu na kwamba haiwezekani kuokoka duniani. duniani watu wanaokoka sawasawa na WARUMI 10:9 na watakatifu wapo sawa sawa na ZABURI 16:3
 Kuishi maisha matakatifu ni mhimu sana kwa mkristo ili aweze kukamilisha safari ya kuingia mbinguni, ukimwamini YESU halafu ukaendelea kuishi maisha ya dhambi haitakusaidia kitu na Jehanamu utaingia. Biblia inasema "EBR 12:14 TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE, NA HUO UTAKATIFU AMBAO HAPANA MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO". Mbingu ni ya Watakatifu tu. Pia Neno la MUNGU linasema "UFUNUO 22:14 HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, WAWE NA AMRI KUUENDEA HUO MTI WA UZIMA NA KUINGIA MJINI KWA MALANGO YAKE". Na UFUNUO 21:27 inasema "Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo bali wale walioandikwa ktk kitabu cha uzima cha Mwanakondoo". Ndugu mpendwa MUNGU anatupenda sana hataki hata mmoja apotee bali kila mmoja awe na uzima wa milele. Kama hujampoke YESU ni wakati sasa wa Kumpokea na Kuendelea kuishi maisha matakatifu. MUNGU akubariki sana.
MUNGU akubariki sana.
By Alex Simion Makuli.

Comments