MAMBO MAKUU NANE(8) ALIYOYASEMA BWANA YESU ILI KUITHIBITISHA BIBLIA.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu uchukue ujuzi wa kiroho kwa ajili ya kujua na kuwasaidia wengine.
Leo nazungumzia mambo 8 muhimu ambayo yalitamkwa na BWANA YESU mwenyewe ili kuithibitisha Biblia takatifu.

1.   YESU alisema Neno la MUNGU ni kweli: Yohana 17:17 '' Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. ''.
-Neno la MUNGU ni kweli.

2.   YESU alisema Agano la kale ni sahihi: Mathayo 12:40-41 '' Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. ''
-BWANA YESU alizungumza habari za Yona ambapo kuna kitabua katika agano la kale kinachoitwa kitabu cha Nabii Yona, na Yote aliyoyasema BWANA YESU yanapatikana katika kitabu cha Yona ambacho kipo agano la kale.

3.   YESU alisema itakuwa rahisi mbingu na Dunia vitoweke lakini hata Yodi moja ya Neno la MUNGU haiwezi kutanguka: Mathayo 5:18 '' Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. ''
-Torati ni sehemu ya Biblia, Torati ni maandiko matakatifu,Torati ni sheria za Musa ambazo zilizolewa kwa ajili ya Waisraeli. Kwa sasa hatuko chini ya Torati lakini hiyo haiondoi kwamba Torati ni maandiko matatifu yaliyomo ndani ya Biblia takatifu.(Warumi 3:19 '' Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya MUNGU ''). Tena Zaburi 119:89 inasema ''Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele.    ''

4.  YESU alisema hata kama mbingu na dunia zitapita lakini Neno la MUNGU halitapita kamwe: Mathayo 24:35 ''Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. ''
-Neno la MUNGU ndilo Neno la KRISTO, BWANA alisema Neno lake halitapita kamwe.

5.   BWANA YESU alisema Neno la MUNGU liliongozwa na ROHO MTAKATIFU kuandikwa: Marko 12:36 ''   Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, BWANA alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako. ''
-Maandiko hayo aliyoyasema BWANA YESU yapo katika Zaburi ambayo ni kitabu ndani ya  Biblia.
-Kumbe Daudi aliandika Neno la MUNGU kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.
-Ni maadiko mengi yanayothibitisha kwamba waandisho wa Biblia waliandikwa Neno la MUNGU kwa kuongozwa na ROHO wa MUNGU. Unaweza kusoma Yohana 16:13 au 2 Petro 1:21.

6.   YESU aliita Agano la kale kwamba ni Neno la MUNGU: Marko 7:13 ''huku mkilitangua neno la MUNGU kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.   ''
-YESU alikuwa akiwaambia wafalisayo na waandishi kwamba wanalitangua neno la MUNGU na kumbuka kwamba Neno la MUNGU lililokuwepo wakati huo ni Agano la kale.

7.  YESU alifundisha kila fungu la maneno ukilinganisha na tabia ya nyakati zile ni sahihi kama MUNGU alivyokusudia.: Marko 12:26-27 ''  Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Sura ya Kijiti, jinsi MUNGU alivyomwambia, akisema, Mimi ni MUNGU wa Ibrahimu, na MUNGU wa Isaka, na MUNGU wa Yakobo? Yeye si MUNGU wa wafu, bali wa walio hai. Hivyo mwapotea sana. ''
-YESU alikuwa anazungumzia maandiko matakatifu  ambayo yanatoka katika vitabu vya Musa  ndani ya Biblia.

8.     YESU alisema ahadi zote na unabii kutoka katika Biblia sharti zitimie: Yohana 10:35 '' Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la MUNGU; (na maandiko hayawezi kutanguka); ''
MUNGU akubariki sana na naamini umejifunza uhakika wa Biblia yote.
-Soma Biblia kila siku ili ujifunze kusudi la MUNGU juu ya maisha yao.
-Soma Biblia ili ukue kiroho.
-Soma Biblia ili upate mamlaka zaidi ya kimungu.
-Soma Biblia ili adui akuogope.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.


Comments