MCHOYO YEYOTE YULE PIA NI MWIZI

Na Mwinjilisti John Chinyuli.

Huwezi kuwa mchoyo(mnyimi,mbinafsi) bila kuwa mwizi(mzurumaji au tapeli)
maana moyoni mwa mtu mchoyo lazima kumejaa ubinafsi,umimi,kujijali wewe tu,ushibe wewe tu na wengine watajiju....! utanielewa tu tuendelee
kumbe basi uchoyo ni tabia ya ubinafsi ambayo ndani yake imebeba roho ya wizi

Moyoni mwa mtu mchoyo hamna chembe ya upendo maana yeye ni mbinafsi kilichotawala maisha yake ni uonezi,kugandamiza wengine,ulafi ,Kwahiyo mtu mchoyo(mbinafsi) hapendi kuona wengine wafanikiwe ila ni yeye tu kwahiyo yuko tayari hata kuwaibia,kuwagandamiza,kuwadhulumu nadhani sasa ushaanza kunielewa kuwa mchoyo yoyote Yule ni mwizi pia japo ni ngumu kuamini ukweli huu lakini ndivyo ilivyo ichunguze jamii ya watu unao ishi nao utagundua hiki ninacho kwambia,
Basi ikitokea mchoyo ametoa kitu ni ili asifiwe/aonekane/ajulikane kuwa yeye ndio yeye anavyo au kuna mazingira Fulani anayaandaa ili apate anachokihitaji huko mbele,na si tu anatoa kitu ili mladi tu ametoa/amesaidia na asubiri Mungu mwenyewe atamlimpa/atambariki kwa wakati na majira yake vile Mungu apendavyo,mtu mchoyo hayuko hivi!
Jambo hili ndicho kitu kinachosumbua ndani ya jamii yetu na nchi yetu watu wengi/viongozi wengi ni wachoyo na kupelekea maisha yao kutawaliwa na hizo roho zingine za wizi kuwamiliki automatically na hata kutenda kazi ndani ya maisha yao,
Halafu ukumbukwe ukizoea kuwatendea wengine jeuri,Jiandae na wewe siku kutendewa jeuri maana apandacho mtu ndicho atakacho vuna!
Mungu atusaidie sana watanzania hatutaki kufuata utaratibu wa Mungu kuwa katika kutoa ndipo tupokee ila tunataka kulazimisha mambo matokeo yake ndio hapo tunaingia kumtumikishwa na shetani

Pia ikumbukwe kabisa shetani ni mshezi sana akimkamata mtu kwenye mtego Fulani huo huo mtego huwa unafungua na mlango wa jambo jingine ndio maana mwaka jana nikakueleza pia lile jambo la walevi wote ni wezi japo ni ngumu kukubaliana na ukweli huu kutokana na walevi wengi wanahadhi Fulani katika jamii na kuonekana watu wenye heshima zao sana lakini ukweli utaendelea kubaki pale pale walevi wote ni wezi na wachoyo wote ni wezi,
Kumtumikia shetani hakufai maana mtu akimtukia anaendelea kuharibikia kwenda mbele maana akianza kufanya dhambi Fulani inafungua na mlango wa kuanza kufanya uharifu(dhambi) nyingine tena na matokeo yake maisha ya huyu mtu yanamenzwa na ushetani na kuishia kwenye uharibifu
Ni heli kumgeukia Mungu leo maana kwa Yesu inalipa,Amua leo kuwa mtu mwema,uishi maisha ya kumpendeza Mungu uache uchafu wa tabia,na hata tabia hizo unazoziita ni dhambi ndogo ndogo,kumbuka dhambi ni dhambi tu na dhambi ndogo ndogo ndizo zilizomaliza wengi na kuwaingiza wengine kwenye maisha ya majuto yasiyo isha,Niishie hapa kwa leo,Mungu aendelee kukukarabati uwe mtu mwema sana ndugu yangu na ufanikiwe sana
RUDISHA WATU KWA YESU KAMPENI 2015 (16)
chinyulimwinjilisti@gmail.com

Comments