MFALME WA WAFALME NI MUNGU MWENYE NGUVU.

BWANA YESU asifiwe.
Karibu tena tule chakula cha uzima wa roho zetu.
Mathayo 5:10 ''Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana UFALME wa mbinguni ni wao  ''
Na Peter M Mabula
BWANA YESU ndiye MFALME wa wafalme tena BWANA YESU ndiye BWANA wa mabwana. Danieli 7:13-14 ''Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo MZEE wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na UFALME wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.''

Haleluya maana yake msifuni BWANA YESU aliye MFALME wa wafalme wote.
Mfalme anatokana  ufalme.
Ufalme maana yake ni utawala.
Ufalme una mamlaka.'Kumb 10:17 ''  Kwa maana BWANA, MUNGU wenu, yeye ndiye MUNGU wa miungu, na BWANA wa mabwana, MUNGU mkuu, mwenye kuogofya, asiyependelea nyuso za watu, wala hakubali rushwa. ''

Kuna falme za aina 3.
-Kuna ufalme wa MUNGU.
-Ufalme wa kibinadamu.
-Ufalme wa shetani.

Ufalme wa kibinadamu ni ufalme ambao hauwezi kusimama peke yake maana ufalme huu lazima utegemee UFALME wa MUNGU au utegemee ufalme wa shetani.
Kama viongozi wa ufalme huu wa kibinadamu watamcha MUNGU aliye hai basi  watakuwa chini ya UFALME wa MUNGU na hakika watakuwa wanafanya vyema lakini ufalme huu wa kibinadamu ukijitenga na MUNGU hakika ni makosa makubwa ( 1 Samweli 13:13, Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya BAWANA, MUNGU wako, aliyokuamuru; kwa maana BWANA angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya Israeli milele) 
Ufalme wa kibinadamu ukiwa chini ya shetani maana yake viongozi wa ufalme huo wa kibinadamu wako chini ya majini, waganga wa kienyeji, wanajimu, uchawi na wakuu wa giza kutoka kuzimu.
Ufalme wa shetani huongozwa na shetani na ni ufalme ambao siku ya mwisho utaangamizwa wote kuanzia kiongozi mkuu wa ufalme hadi mfuasi wa mwisho ambaye ni mwadamu.Ufunuo 17:14 ''Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni BWANA wa Mabwana, na MFALME wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.''
Nimezungumzia kwa sehemu tu kuhusu falme hizi lakini jambo kubwa nataka tuujue ufalme wa MUNGU ambao ni Ufalme wenye nguvu  na hakika ukiwa upande wa ufalme wa MUNGU uko upande wenye nguvu maana falme zingine zote hazitadumu 2 Wafalme 19:15''  akasema, Ee BWANA, MUNGU wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe MUNGU wa falme zote za dunia; wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi. '' 
 falme za wanadamu wafalme wao watakufa au watastafu au kufukuzwa kazi  na ufalme utakuwa umeishia hapo, wafalme hawa wa ufalme wa kibinadamu sio lazima waitwa wafalme maana hata rais ni mfalme kwenye nchi, waziri ni mfalme kwenye wizara, mkuu wa wilaya ni mfalme kwenye wilaya, mameneja ni wafalme kwenye vitengo vyao, wakuu wa idara au taasisi mbalimbali ni wafalme kwenye idara zao, hata baba kwenye faimilia ni mfalme kwenye familia yake hivyo ukitegemea ufalme wa kibinadamu hakika utakuja umia tu siku moja maana ufalme huo au utawala huo una mwisho. Ukitembea kwa kujidai kwa sababu baba yako ni mbunge ipo siku nafasi ya ubunge atakuwa hana tena hivyo ufalme kuisha. Kama wewe huwa unaenda ofisini kwa baba yako na kuingia tu bila hata kupita hodi ipo siku nafasi hiyo itachukuliwa na wengine na wewe ukiwa na shida ofisi hiyo unaweza ukatuma maombi kwa miezi 6 ili tu kupata nafasi ya kuonana na mkuu huyo, jambo la kujua hapo ni kwamba ufalme umebadilika. Kutoka 1:8-11 '''   Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.'''
Ufalme ulipobadilika mateso yalianza.

Hata ufalme wa shetani una mwisho maana hata shetani mwenyewe unayemtegemea kwa kukupa pesa za muda mfupi naye atakwenda jehanamu.
Ndugu zangu ufalme sahihi wa kuhakikisha unakutawala ni ufalme wa MUNGU tu. Zaburi 10:16 ''  BWANA ndiye Mfalme milele na milele; Mataifa wamepotea kutoka nchi yake. ''
Ufalme wa MUNGU ndio ufalme mkuu na ufalme wa milele. Ufalme wa MUNGU unasifa nyingi sana. ni ufalme wenye nguvu. Ufalme huu una MFALME wa milele kama ufalme wenyewe ulivyo wa milele.Ufunuo 19:16 ''Naye(YESU) ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.''
BWANA YESU ndiye mfalme wa ufalme wa MUNGU.
Jina la MFALME wa ufalme wa MUNGU  ni YESU KRISTO.
YESU KRISTO ni MFALME wa wafalme
MFALME wa wafalme maana yake ni kwamba hakuna mfalme aliye juu yake. hakuna mfalme asiyepiga goti kwa MFALME wa wafalme, Hakuna mfalme asiyepiga saruti kwa MFALME wa wafalme.
1 Timotheo  3:14-16 ''   kwamba uilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hata kufunuliwa kwake BWANA wetu YESU KRISTO; ambako yeye kwa majira yake atakudhihirisha, yeye aliyehimidiwa, Mwenye uweza peke yake, MFALME wa wafalme, BWANA wa mabwana; ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina. ''
-Jina hili la MFALME wa wafalme BWANA YESU haitwi duniani tu bali hata mbinguni.Ufunuo 5:8-10 ''Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.''

Ndugu, kwanini unajitenga na MFALME wa wafalme?
Wafalme unaowategemea wote hawana nguvu zozote kwa MFALME wa wafalme.
BWANA YESU alipokuja duniani alisema tuombe kwamba ''UFALME WA MUNGU NA UJE''  Mathayo 6:9 ''...  BABA yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, ''.
inaposemwa kwamba Ufalme wa MUNGU uje maana yake haukuwemo, haukuwepo katika mioyo yetu, haukumwepo katika maisha yetu. Ufalme huu haukuwepo kwetu tu ila ni ufalme ambao upo tangu milele na utadumu milele.
Ndugu yangu, ita ufalme wa MUNGU kwenye familia yako, kwenye ukoo wako na kwenye kazi yako.
Ufalme wa MUNGU ni ufalme wa haki na uzima wa milele.
Mwite MFALME wa wafalme YESU KRISTO mwenye mamlaka yote na ukuu wote.
YESU ni MUNGU mwenye nguvu. Daniel 2:47 ''Mfalme akajibu, akamwambia Danielii, Hakika MUNGU wenu ndiye MUNGU wa miungu, na BWANA wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. ''  
Kataa kuwa kwenye ufalme mwingine wowote bali hakikisha uko kwenye ufalme wa MUNGU na hakikisha unaongozwa na kulindwa na MFALME wa wafalme.
Mathayo 6:33'' Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.   ''
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments