MRUHUSU YESU AINGIE NDANI YAKO

Na Mtumishi Alex Simion Makuli
Bwana YESU asifiwe. 
Katika maisha yetu hapa duniani tunaishi lakini kwa upande mwingine tukumbuke kwamba lipo tumaini jipya ndani ya KRISTO YESU, YESU KRISTO anahitaji sana mioyo yetu kuliko kitu kingine chocho, hataki hata mmoja wetu apotee bali kila mmoja afikilie toba. Niongee na wewe ambaye siku zote umeisikia sauti ya Bwana ikikusihi "KUOKOKA" halafu ukaufanya moyo wako kuwa Mugumu, bado Nafasi ipo, na YESU bado anakupenda hataki uangamie ktk Jehanamu, bado lipo tumaini jipya, Kumbuka kuokoka ni leo wala sio kesho, "Na utakapoisikia sauti ya BWANA leo usifanye moyo wako kuwa Mugumu". BIBLIA inasema "Ufunuo 3:20" TAZAMA NASIMAMA MLANGONI, NABISHA, MTU AKISIKIA SAUTI YANGU, NA KUFUNGUA MLANGO NITAINGIA KWAKE, NAMI NITAKUWA PAMOJA NAYE, NA YEYE PAMOJA NAMI. YESU KRISTO yupo mlangoni kwako leo mkubari ili aingie kwako, Na kama hujampokea YESU kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako ndio wakati sasa wa kumpokea

 Hakuna furaha kubwa kama kumwamini YESU KRISTO ktk maisha yako, ikimwamini YESU anakuwa kiumbe kipya(2KOR 5:17), hajalishi umetenda uovu kiasi gani lakini YESU akiingia ndani yako anabadilisha historia ya maisha yako na kukupa uzima. Ukimwamini YESU na kumpokea moyoni mwako hapo ndipo unapata nafasi ya kufanyika mtoto wa MUNGU(Yoh 1:12). Nashangaa sana nyakati hizi tulizonazo watu wanakataa "WOKOVU" eti kwa sababu wanazo dini zao ua madhehebu yao, YESU ni wa mhimu sana kuliko dhehebu lako. Lakin ja ajabu watu wako gizani pamoja na dini zao, Ukija kwa YESU unakuwa nuruni, BIBLIA inasema "YOH 12:46 MIMI NIMEKUJA ILI NIWE NURU YA ULIMWENGU, ILI KILA MTU ANIAMINIYE MIMI ASIKAE GIZANI". Unaweza kuwa na dhehebu lako zuri lakin ukawa gizani, lakin ukija kwa YESU unakuwa nuruni na kupata uzima wa milele

 Mtu mmoja anapomwamini YESU kunakuwa na furaha mbinguni kwa ajiri ya mtu huyo ambaye amempa YESU maisha yake. "LUKA 15:7 NAWAMBIA HIVYO HIVYO KUTAKUWA NA FURAHA MBINGUNI KWA AJILI YA MWENYE DHAMBI MMOJA ATUBUYE, KULIKO KWA AJILI YA WENYE DHAMBI TISINI NA KENDA AMBAO HAWA HAJA YA KUTUBU". Kwa hiyo unaweza kuona ni kwa jinsi gani roho ya mtu ilivyo ya thamani mbele za MUNGU.  

FAIDA ZA KUMPOKEA/KUMWAMINI YESU

(1)Unahamishwa kutoka ktk ufalme wa giza na kuingizwa ktk MUNGU[KOL 1:13].
 (2)Unasamehewa dhambi[LUKA 7:48-49, KOL 1:14]. 
(3)Unafanyika mtoto wa MUNGU[YOH 1:12]. 
(4)Unapata haki[WARUMI 5:9]. (5)Unapata nguvu ya MUNGU[1KOR 1:18].
 (6)Unakuwa kiumbe kipya[2KOR 5:17]. 

MUNGU wetu anatupenda sana hataki hata mmoja wetu apotee bali kila mmoja afikirie toba. Mpokee YESU leo upate uzima wa milele.

 Hakuna kitu kibaya kama kumkataa YESU, Maana ukimkataa YESU umeikataa mbingu/umekataa uzima wa milele. BIBLIA inasema "1YOH 5:11-12 NA HUU NDIO USHUHUDA, YA KWAMBA MUNGU ALITUPA UZIMA WA MILELE, NA UZIMA HUO UMO KATIKA MWANAE, YEYE ALIYENAYE MWANA ANAO HUO UZIMA, ASIYENAYE MWANA WA MUNGU HANA HUO UZIMA". Kama kweli unataka kuingia ktk uzima wa milele aliko KRISTO YESU lazima umwamini YESU na umruhusu aingia ndani yako. Lakini kama ukimkataa YESU kuna hukumu, YOH 3:18 Biblia inasema "AMWAMINIYE YEYE HAHUKUMIWI, ASIYEMWAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA KWA SABABU HAKULIAMINI JINA LA MWANA PEKEE WA MUNGU, NA HII NDIYO HUKUMU YA KUWA NURU IMEKUJA ULIMWENGUNI NA WATU WAKAPENDA GIZA KULIKO NURU KWA MAANA MATENDO YAO YALIKUWA MAOVU". Kwa hiyo ukisikia sauti ya YESU halafu ukaikataa Biblia inasema "UMEKWISHA HUKUMIWA" Sio "UTAHUKUMIWA", 

Unapomruhusu YESU ili aingie ndani ya moyo wako hapo ndipo jina lako huandikwa ktk kitabu cha uzima. Na wale wote ambao majina yao yameandikwa ktk kitabu cha uzima cha Mwanakoodoo ndio wenye haki ya kurithi uzima wa milele wakiwa na KRISTO YESU. UFUNUO 21:27 Biblia inasema "NA NDANI YAKE HAKITAINGIA KAMWE CHOCHOTE KILICHO KINYONGE, WALA YEYE AFANYAYE MACHUKIZO NA UONGO, BALI WALE WALIONDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA CHA MWANA-KONDOO". Kwa upande mwingine inawezekana kweli tumempokea YESU, lakini tunapaswa KUTUBU pamoja na KUISHI MAISHA MATAKATIFU ili siku ile ya mwisho tusije tukawa watu wa kukataliwa. "1YOH 1:8-9 TUKISEMA KWAMBA HATUNA DHAMBI TWAJIDANGANYA WENYEWE WALA KWELI HAIMO MWETU. TUKIZIUNGAMA DHAMBI ZETU, YEYE NI MWAMINIFU WA HAKI HATA ATUONDOLEE DHAMBI ZETU NA KUTUSAFISHB NA UDHALIMU WOTE". MUNGU atusaidie sana ili tuweze kufikia ile ahadi ya uzima wa milele. "YESU ANAOKOA", 
Barikiwa sana!. 
By Alex Simion Makuli

Comments