MTU WA MUNGU NA MTU WA MUNGU HASA

Na Godfrey Miyonjo.

“Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe WATU WAKE HASA” ZABURI 135:4.
BWANA YESU asifiwe.
Ninakusalimu kupitia jina lipitalo majina yote, JINA LA YESU.
Mpendwa kati ya mambo ambayo huwachanganya watu wengi ni hili, kushindwa kujua tofauti iliyopo kati ya “WATU WA MUNGU” na “WATU WA MUNGU HASA”.
Wengi husema sisi sote ni wa Mungu mmoja (watoto wa baba mmoja) hivyo tusihukumiane (tusikosoane/tusiambizane ukweli) kuhusiana na imani zetu hasa pale tunapoonekana tupo kinyume na neno la Mungu.
Huu ni unyama kwa mujibu wa neno la Mungu, kwa maana imeandikwa:
“kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama” MITHALI 12:1.
Ni kweli wanadamu wote ni wa Mungu lakini WOTE SIYO WA MUNGU HASA.
Wote ni WATU WA MUNGU kwasababu sote tumeumbwa na Mungu, lakini kuumbwa tu haitoshi, kuna kitu cha ziada cha kufanya kwa Mungu aliyetuumba ili kuonesha kuwa sisi ni WATU WA MUNGU HASA.
Ili uwe MTU WA MUNGU HASA lazima uwe ni mtu unayeishi kwa kufuata matakwa ya Mungu (NENO LA MUNGU).
Ukiangalia katika jamii zetu siyo watoto wote wliozaliwa katika jamii/familia flani ni warithi katika jamii/familia hiyo, kuna watu wamekataliwa na jamaa zao (wazazi, ukoo) hata wakaondolewa na kuhesabika kuwa siyo sehemu ya jamii hiyo kutokana na tabia zao mbaya.
Hata katika marafiki pia kuna baadhi ni “MARAFIKI ZETU” na wengine ni “MARAFIKI ZETU HASA” kutokana na tabia zetu na za kwao kuendana au kutokuendana. AMOSI 3:3.
Hivyo kwa Mungu pia kuna watu kutokana na matendo yao wamejiondoa/wamejifarakanisha na Mungu hata wakawa siyo WATU WA MUNGU HASA. RUMI 1:21.
Lakini Mungu ni mwingi wa rehema, hapendi kuona hata mwanadamu mmoja anapotea.
Anasema ingekuwa heri tusikiapo sauti yake (kupitia vinywa vya watumishi wake) tungetubu, na tukitubu kwa Mungu dhambi zetu hazitakumbukwa kabisa. WAEBRANIA 10:17.
Ni toba na utakatifu tu ndivyo vitakavvotufanya tuwe WATU WA MUNGU HASA.
………Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia, yashike hayo na kutubu……… UFUNUO 3:3.
MUNGU akubariki.
By Godfrey Miyonjo

Comments