MUNGU ANAHITAJI UJANA WAKO(2)

Bwana Yesu asifiwe
CAM00027
Na: Mwl Lubeleje Daudi
Nakukaribisha tena katika mwendelezo wa somo la “Mungu anahitaji ujana wako”. Katika sehemu ya pili ya somo hili tutaona kuwa Mungu ameandaa mpango/kusudi kwa kijana ambaye ni potential (rasilimali) muhimu katika ufalme wa Mungu. Kusudi la Bwana kwa kijana ni atumike katika utumishi/huduma mbalimbali kwenye ufalme wa Mungu.
Hebu tuone katika 1 SAMWELI 3: 1 na maandiko yanasema “Basi mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli…..”. Neno “akamtumikia Bwana” inaonyesha kuwa samweli hakuwa amekaa tu nyumbani tu Bwana bure bali alikuwa akitumika. Nikuongeze mstari mwingine pia katika 1 Samweli 2:18 inasema “ Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana……….”. Maandiko yanaweka bayana kuwa “NAYE ALIKUWA KIJANA” akitumika mbele za Bwana. Sasa wewe kijana ambaye unasema mimi wakati bado au mimi siwezi au wakati bado huna cha kujitetea kwa Bwana kwa sababu wenzio walianza wakiwa vijana kama wewe. Nataka nikumegee siri ya utumishi wa Samweli ambayo pia mimi na wewe kama vijana tunaweza kuwa wa kuleta faida katika ufalme wa Mungu. Siri hiyo kubwa ni;
“HAKULIACHA NENO LAKE (MUNGU) LOLOTE LIANGUKE CHINI” (1 SAMWELI 3:19”
Ngoja nikwambie wengi tumeacha kutumika kwa sababu tumeacha Neno la Bwana lianguke chini. Katika zaburi 119:9 maandiko yanasema “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lako”. Vijana wanaotii wakilifuata neno la Mungu hawawezi acha neno la Bwana lianguke chini katika maisha yao bali watalishika. Neno la Mungu kwa kijana ndiyo msingi wa Utumishi wao. Kijana anapaswa kumtumikia Mungu huku msingi wakeukijengwa katika neno la Mungu. Hebu jiulize mara ngapi umekuwa wa kuacha neno la Bwana lianguke tu chini?.
Wewe ni thamani na Mungu anataka ujana wako kwamba uwe kwa faida na siyo hasara. Wewe ndiyo Mwalimu wa Neno la Mungu, Mwinjilisti n.k. Usifukie huduma Mungu amekupa. Neno la Mungu lisafishe njia yako leo katika kumtumikia Mungu.
Na: Mwl Lubeleje D (Vijana na Utumishi)
0764771298

Comments