MWAKA MPYA: MUNGU ANATAKA UFANYE JAMBO LIFUATALO.

BWANA YESU atukuzwe.
Ni mwaka mpya hakika.
Ndugu Zangu "Ni Huruma Za BWANA Kwamba Hatuangamii, Kwa Kuwa Rehema Zake Hazikomi.- Maombolezo 3:22
Hakika ni MUNGU ndiye aliyetulinda hadi kuufikia mwaka mpya au mwaka wa nyongeza.
Jambo kubwa ni hili Mshukuru MUNGU Kwa Uzima Aliokupa Hadi Kufika Leo tena katika mwaka mwingine.
-Kuna Watu Wameondoka Dakika Kadhaa Kufika Mwaka Huu mpya. Unadhani Kwanini weweUpo Hai Leo? 
-BWANA YESU Anakupa Nafasi Ya Kuchagua Uzima Na Si Kuzimu. Anatamani Akupe Uzima Wa Milele Ila Utaupata Tu Kwa Wewe Kumpokea. 
-Huu Ni Mwaka Wa Toba. 
-Umepewa Mwaka Wa Nyongeza Ili Utubu. 
-YESU KRISTO Anakuita Leo Ili Akuokoe.
 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu. -Warumi 6:23.''
 
 Je Uliupokea Mwaka mpya Ukiwa Wapi? 

-Kuna Watu Huupokea Mwaka Wakiwa Sehemu Mbaya Kama Disko Na Kwenye Bar Au Kwenye Vilabu Vya Pombe. Watu Hawa Hushangilia Kuuona Mwaka Mpya Huku Wakiwa Na Chupa Za Bia. 
-Ndugu, Je Unajua Kwamba Kadri Unavyoupokea Mwaka Mpya Ndivyo Na Miaka Yako Ya Kuishi Duniani Inapungua? Maana Kama Unatakiwa Uishi Miaka 28 Na Leo Umeshangilia Kwa Kupokea Mwaka Wa 27 Kumbe Hujui Kwamba Umebakiza Mwaka Mmoja Ili Uondoke Duniani. Je Unafurahia Miaka Yako Ya Kuishi Kupungua?. 
-Ngoja Nikupe Siri Hii, Sisi Wateule Wa KRISTO Huwa Tunashangilia Sana Kuupokea Mwaka Wa Nyongeza Au Mpya Kwa Sababu Siku Zetu Za Kuwa Duniani Zinakaribia Kuishi Maana Duniani Sisi Ni Wapitaji Tu, Wenyeji Wetu Uko Mbinguni. Wafilipi 3:20 '' Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, BWANA YESU KRISTO; '' 
Huku Tuko Njiani Tu Kuelekea Kwetu. Kama Unatuiga Huku Hujampokea YESU Pole Sana. Maana Wewe Mtenda Dhambi Ukiondoka Hapa Kabla Hujaokoka Utaenda Kuzimu Kwenye Mateso. Mimi Nakuonya Ili Umpokee BWANA YESU. YESU anatuambia Hivi sisi ambao tunatarajia kuishi na yeye mbinguni, BWANA YESU anasema anatuambia  ''Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini MUNGU, niaminini na mimi. Nyumbani mwa BABA yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.  Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo- Yohana 14:1-3'' 
MUNGU amekupa kuuona mwaka mpya ili uamue vyema.

 unaweza kujiuliza jambo hili, Kila Mtu Amemshukuru MUNGU Kwa Kumfikisha Mwaka huu mpya. 
Kila Mtu Amemshukuru, 
- Wachawi Wamemshukuru, 
-Walioenda Kwa Waganga Mwaka uliopita  Nao Wamemshukuru -Hata Walichanjwa Chale mwaka uliopita Nao Wamemshukuru, -Wazinzi Na Walevi Nao Wamemshukuru 
-Na Hata Waongo Nao Wamemshukuru. 

Wote Hawa Wamefanya Vyema Kumshukuru MUNGU Wa Mbinguni Kwa Kuwapa Kuishi mwaka huu mpya Lakini MUNGU Amenituma Niseme Kwamba MUNGU Hajawapa mwaka mpya Ili Mwendeleze Dhambi, Bali Amewapa mwaka mpya Ili Mtubu. 
''Tubuni; Kwa Maana Ufalme Wa MUNGU Umekaribia(Mathayo 3:2), 
BWANA YESU Anamtarajia Kila Mmoja Ampokee. 
Ndugu Yangu Usipookoka mwaka huu mpya Sijui Utaokoka Lini. Binafsi Namuombea Neema Ya Wokovu Kila Mtu. Mathayo 24:37-44 Biblia inasema ''Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja BWANA wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.'' 
Heri ya mwaka mpya.

 Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

Comments