MWIMBAJI WA ACACIA SINGERS AOLEWA NA MWIMBAJI WA THE HEAVENLY GATE SINGERS

Pichani ni maharusi,Daniel Simeon na Elina Rubakula katika pozi mara baada ya kuwa mwili mmoja kwa kufunga pingu za maisha.




 Hivi karibuni mwimbaji wa sauti ya kwanza wa kundi la uimbaji wa nyimbo za Injili la Acacia Singers la jijini Dar es salaam Elina Rubakula alifunga pingu za maisha na Daniel Simeon ambaye pia ni mwimbaji wa kundi la The Heavenly Gate Singers,ndoa ya wawili hao ilifungwa katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Mwenge jijini Dar es salaam ambapo wageni na marafiki wakiwemo waimbaji wa Acacia Singers walihudhuria na kushuhudia mwimbaji huyo na mumewe wakiimba kwa kuimba pamoja na kundi hilo,kanisani mwenge na ukumbini wakati wa sherehe ya wawili hao.

Comments