NABII WA KWANZA WA MAISHA YAKO NI WEWE MWENYEWE (EZEKIELI 37:1-10)

USIACHE KUJITOLEA UNABII KWA NENO LA BWANA KILA SIKU NDANI YA ROHO MTAKATIFU
Ezekikeli alielekwa na BWANA kwenye bonde la mifua mikavu, Lakini tutambue kwamba Imani ya Ezekieli ilikuwa chini sana hakuamini kwamba ile mifupa inaweza kuishi, kama vile wewe unavyoona maisha yako kuwa ni mifupa isiyoweza kuishi,

Ezekieli alipoitazama ile mifupa hakujua kwanini Mungu alimpeleka pale ni sawa na wewe usivyojua kwamba kwanini Mungu amekupitisha hapo kwenye pito hilo, Kilichomsaidia Ezekieli alikubali kutulia na kuisikiliza sauti ya Mungu inasemajekuhusu mifupa na siyo akili yake inasemaje kuhusu mifupa, Unapofika kwenye bonde la mifupa mikavu unatakiwa kutulia kwa makini sana kumsikiliza Mungu anasemaje kuhusu Mifupa mikavu na siyo kuanza kutumia akili zako, watu wengi sana wamefia kwenye bonde la mifupa mikavu sababu hawakutaka kuisikiliza sauti ya Mungu bali walianza kutumia akili zao na elimu zao wenyewe. Sikiliza mwana wa Mungu kama unataka ufie kwenye magumu ya maisha na majaribu unaoyapitia wewe tumia akili zako tu utaona haitchukua muda mrefu utafia hapo hapo kama wengine walivyokufa kwenye bonde na kubakia mifupa, bonde la mifupa mikavu halihitaji akili ya kibinadamu hata kidogo bali lina hitaji akili ya kiungu.
Ezekieli hakutumia akili zake bali alizikabidhi akili zake kwa Mungu na yeye binafsi alijitoa kwenye kesi hiyo akamkabidhi Mungu kesi yote kwa kusema BWANA WEWE WAJUA. Hapa Ezekieli alikataa kabisa kuzipa akili zake nafasi, sasa watu wengi leo wanaishia tu kusema BWANA WEWE WAJUA lakini wakiisha kusema hivyo wanakaa kimya matokeo yake wanakfia hapo,
Sikiliza mwana wa Mungu Haitoshi tu kusema BWANA WEWE WAJUA hii haisadii lolote kwasabu hta kabla ya kusema hivyo Mungu alikuwa tyari yeye anajua sasa hii kusema wewe wajua ni jambo jema maana ni kuzikataa akili zako lakini hii peke yake haitoshi hata kidogo na ndiyo maana Mungu aiposikia Ezekieli anasema hivyo Mungu akamwambia TOA UNABII ILI MIFUPA IPATE KUISHI Sasa hapa nisikilize kwa makini mwana wa Mungu, Unajua Ezekieli aliposema BWANA WEWE WAJUA alijua ameshamaliza wajibu wake lakini Mungu alipoona Ezekieli ametulia tuli baada ya kusema hivyo Mungu akajua kama atamwacha aishie kusema hivyo basi atafia pale kwenye lile bonde kama vile wale wengine walivyofia pale hata akaikuta mifupa yao pale, kwasabu hata wao waliishia tu kusema BWANA WEWE WAJUA lakini hawakutoa unabii wowote, hii ndiyo sababu iliyompelekea Mungu kuwambia Ezekieli TOA UNABII JUU YA MIFUPA IPATE KUISHI sasa hii inamanisha kwamba mifupa ipo na kuwepo kwake siyo tatizo maana inaasubiria tu Neno litoke kwa Mungu na likiisha kutoka kwa Mungu iingie kwa mtu na likiisha kuingia kwa mtu litoke tena na upako yani mafuta ya Roho mtakatifu na kuingia kwenye mifupa na likiisha kuingia kwenye mifupa ndipo mifupa ianze kukusanyana na kuungana na kuota nyama na kuapa punzi. kwahiyo mifupa mikavu ya maisha au ndoa au elimu ipo ila inasubiria Neno la Mungu siyo neno la mtu hapana bali ni Neno la Mungu, unapoona mifupa mikavu kwenye maisha yako usitumie neno lako kwasabu hilo neno lako kamwe halina nguvu ya kuifanya ikawa hai, na watu wengi sana wamevunjika moyo baada ya kuona wameitabiria na kuitolea unabii mifupa miaka kwa miaka lakini bado mifupa iko vile vile haijikusanyi na haibadiliki, hii yote hutokana na kuitamkia mifupa maneno yao wenyewe na wala siyo Neno la Mungu, sasa unapoona mifupa kwenye maisha yako tafuta Neno linasemaje kuhusu mifupa hiyo alafu iendee hiyo mifupa uiambie kwamba wewe mifupa ya kutokufanikiwa silkiliza Neno la BWANA linasema Mpenzi na ufanikiwe kwa mambo yako yote mimi ninaenda kufanikiwa kwa maeneo yote, Itamkie mifupa Neno la Mungu na unajua Neno siyo andiko andiko ni andiko lipo kwenye karatasi lakini Neno ni lile unalolitamka wewe ndiyo maana Imeandikwa kwamba Lile neno likaribu nawe kinywani mwako>WARUMI 10:8. Hapa haijaandikwa Kitabuni no bali kinywani sasa Neno linatoka kinywani mwa mtu yani ni Ukiisha kunukuu msrari wa ushindi na kuutamka kwa imani ndani ya Roho mtakatifu hilo ndiyo neno, sasa mifupa mikavu inahuishwa kwa Neno na sasa unaitabiria hali uliyonayo kwa kutumia Neno bila kuchoka kila siku,
NGAZI TATU ZA UNABII NA HATUA ZAKE
Kutoa unabii juu ya maisha kuna hatua kubwa tatu na hatua hizi ni lazima kuzitambua na kuelewa kunahitajika nini hapa kwa kila hatua maana kila hatua inayo aina yake ya utanabii unaohitajika hivyo ni muhimu sana mtu kujua kwamba yupo kwenye ngazi ipi kati ya ngazi hizi tatu maana katika kila ngazi kunayo jinsi yake ya kutabiri hii inamaana kwamba kila mifupa inavyobadilika mtu anatakiwa kubadili aina ya unabii wa kutoa kuendana na hiyo hatua.

HATUA YA KWANZA NI UKUIKUSANYA MIFUPA
Hatua ya kwanza ya kutoa unabii ni unabii wa kuikusanya mifupa mikavu, sasa hapa weengi sana huwa wanakosea wanapotoa unabii na kuona mifupa imeanza kjikusanya na kuwa karibu tu wanajua kazi imeisha wanaacha kuendelea kutabiri matokeo yake maono yao yanaishia tu kwenye mifupa kukusanyika, hii ni mbaya sana mifupa inapokusanyika na kuwa pamoja siyo mwisho wa kutoa unabii hapo hapana bali hapo ni pakubadilisha aina ya unabii wa kuitolea mifupa na unabii huu unapobadilika ni wazi kwamba na Neno lakutolea unabii huo nalo linabadilika hatutumii neno lile lie hapana tunatafuta teena Neno lingine la Mungu na kuanza kulitumia kwa kutolea unabii mifupa ili ipate kuishi, unapoona kwamba kuna mabadiliko kidogo yamafanikio yanayoanza kujitokeza kwenye eneo ulilolitolea unabii usiache ukazania hapo ndiyo mwisho no bali endelea kutolea unabii mpaka uhakikishe mifupa inaota nyama.

NGAZI YA PILI NI MIFUPA KUOTA NYAMA
Mifupa ikiisha kuota nyaama Mtu hupaswa kubadili aina ya unabii wa kutoa, kwasabu Neno la kwanza limesababisha mifupa kuota nyama sasa kunatakiwa neno la pili litakalosababisha mifuppa kupata pumzi, kwasababu iko wazi kwamba nyama isipokuwa na pumzi inaoza kama itakaa muda mrefu na ndiyo maana maono ya wengi yameshaoza na sasa yanatoa harufu mbaya kwasabu pindi nyama ilipotokeza, wao wakaacha kutoa unabii wakaridhika kuwa na nyama isiyo na pumzi, sasa hii ni mbaya sana maana mifupa ikiisha kuota nyama na nyama hiyo ikaoza hali halisi inakuwa ni mbaya sana, kwasabu muhusika atayakimbia maono yake maana yanatia aibu kwa kutoa harufu mbaya, hata sasa kuna maono yako umeyakimbia kwasabu yamekwishakuoza, unahitajika kuaza upya kwa Neno la Bwana Mungu na akurehemu.

NGAZI YA TATU NI NYAMA KUPATA PUMZI
Ngazi ya mwisho ambaayo hiyo ndiyo hitimisho la kutoa unabii juu ya maisha yako ni kuona mafanikio yamepatikana hapa sasa ndipo unaweza kusema mifupa imekuwa jeshi kubwa sana ambalo halikuonekana kwaanza bali lilionekana baada ya mwanadamu kutoa unabii juu ya mifupa hatimaye mifupa ikajikusanya, akaendelea kutoa unabii ikaota nyama, akaendelea kutoa unabii ikapata pumzi hatimaye sasa limekuwa jeshi kubwa lakumpagainia na kumtumikia yeye

Mwana wa Mungu usitishwe na mazingira yako mabaya yakukatisha tamaa yanayokuzuunguka iwe kwenye ndoa, Masomo, Uchumi, Kibali, Biashara, Kazi nk wewe chakufanya hapo ni kuisoma sana biblia na kutafuta mistari ya maandiko ambayo inaenda kinyume na hali hiyo kisha uitamke mistari hiyo kwa kinywa chako huku umezama rohoni maana hilo ndilo Neno usiache kufanya hivyo siku kwa siku utaona mwenyewe hali hiyo itakuacha kwa ghafla fumba na kufumbua. nakumbuka Mwaka Juzi 2012 nilikuwa na mahitaji ya muhimu sana ambayo gharama yake sikuwa na uwezo nayo hata kidogo gharama yake ilikuwa ni kubwa kwangu nikawa najitolea unabii kila siku kwa kutumia Neno la BWAN nilikuwa nafanya mara tatu kwa siku Asubuhi najitolea unabii kwa lisaa limoja, na mchana najitlea unabii kwa lisaa limoja, na usiku najitolea unabii kwa lisaa limoja, ikapita miezi miwili nikaitwa na mtu niliyewahi kumhudumia zamani akapata mtoto mtu huyu ni mama anafanya kazi kwenye mashirika ya kuuza na kununua hisa aliponiita akanibariki kwa shingi Laki Nne na na nusu kwangu ilikuwa ni muujiza mkubwa kwasabu kipindi hicho nilikuwa sina hata nauli za daladala nilikuwa natembea mguu kwa mguu toka Mbagala hadi Yombo nilishatembea kutoka Yombo mpaka Kibamba kwa mguu, nivigumu kuamini lakini kwa kuwa ni kweli acha tu niseme, tulikuwa tuna lala na njaa na tumeshazoa kabisaa hiyo hali hivyokilikuwa kipindi kigumu kwangu sasa katika hali kama hiyo alafu anakuja mtu anakupa laki nne na nusu gafla gafla tu ooh siyo jambo dogo na ndani ya mwezi huohuo nikapata muujiza wa laki tatu na sitini kutoka kwa Mchungaji mmoja mwanamke wa Morogoro na hatimaye ule uhitaji wote ukapata ufumbuzi. huwa napenda kufundisha vitu ambavyo nimevipitia sana maana hivyo nina uhakika navyo maana kwa macho yangu naliviona.
Usisubiri kutolewa unabii Nabii wa kwanza wa maisha yako NIWEWE MWENYEWE tumia vema kinywa chako kujitolea unabii kwa kupitia Neno la Mungu FANYA HIVYO NAWE UTAISHI.
YANGU NI HAYOTU KWA LEO
ZIDIKUBARIKIWA.

Comments