NINI CHA KUFANYA PINDI UMEOMBA MAOMBI KWA MUDA MREFU NA HUJIBIWI.

Na Emmanuel Kamalamo.
Bwana Yesu asifiwe!
Najua hakuna mtu ambaye hajapitia maombi ya namna hii, na baadha ya watu wameweza kurudi nyumba na hata kimuacha Kristo sababu wameomba muda mrefu bila majibu yoyote kupoke.
Na unaweza ukatafuta tatizo nini lakini usipate jibu, au ukasema labda nina DHAMBI inayozuhia maombi yangu maana maandiko yanasema..."TWAJUA MUNGU HAWASIKII WENYE DHAMBI; BALI MTU AKIWA NI MCHA MUNGU, NA KUYAFANYA MAPENZI YAKE HUMSIKIA HUYO" Yohana 9:31.
Isaya 59:1-2 "Tazana, mkono wa BWANA haukupunguka, hata asiweze kuokoa; wala sikio like si zito, hata lisiweze kusikia. Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu , na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia"

Ni kweli hivi ni vizuhizi vya kutojujibiwa maombi. Lakini si kila maombi yasiyo jibiwa yamezuhiwa na dhambi la asha! Bali kuna namna hayajibiwa kuna sababu ya kutokujubiwa. Unaweza ukatubu dhambi zote na za wajukuu na ukawa safi mbele za Bwana lakini bado anga limekaa kimya. Sasa nini cha kufanya katika hali ya namna hiyo?.
JAMBO LA MUHIMU.
~GEUZA MAOMBI YAKO NA MUULIZE MUNGU KWA NINI UNAOMBA HUJIBIWI.
Mungu anaposemea..TUHOJIANE ELEZA MAMBO YAKO UPATE KUPEWA HAKI YAKO" maana yake ni nafasi amekupa ya maswali muulizane pale unapoona hupati haki yako na umeomba kwa muda mrefu.
Habakuki 1:2 "Ee BWABA, nilie mpaka lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa." Wasomaji wa biblia wanajua maombi ya Nabii Habakuki alikuwa akiomba Mungu auondoe UOVU NA UHARIBIFU ulio katika nchi, na aliomba kwa muda mrefu lakini Mungu alikaa kimya, hatujui ni muda gani aliomba lakini anaposema.."NILIE MPAKA LINI" maana kalia muda mrefu hakuna majibu Mungu anamtazama tu.
Habakuki alipoona MAOMBI hayajibiwi aligeuza mfumo wa maombi, hakuomba maombi yaleyale bali alirudi kumuuliza Mungu kwa nini hunijibu, walihojiana na Mungu.
Habakuki 2:1"Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyomjibu katika habari ya kulalamika kwangu"

Nini Mungu alimwambia Habakuki aliporudi kuuliza kwa nini hajibiwi, Ukisoma sura ya Mungu alimjibu Habakuki akamwambia..."MAANA NJOZI HII BADO NI KWA WAKATI ULIOAMRIWA....IJAPOKAWIA INGOJEE: KWA KUWA HAINA BUDI KUJA, HAITAKAWI" Habakuki 2:1-3
Kwa majibu ya Mungu tunagundua Habakuki alikuwa anaomba nje ya "MPANGO WA MUNGU/ MAPENZI YA MUNGU" ndiyo maana Mungu alikuwa kimya.

Inawezeka na wewe umeombea hitaji lako kwa muda mrefu na huoni majibu, umetubu DHAMBI, umevunja na LAANA umewekewa mikono na watumishi mbalimbali lakini hujibiwi....oh! Geuza maombi yako muulize Mungu kwa kuhojiana ili akwambie. Inawezekana una taka PESA ZA MTAJI na hupati si kwamba Mungu hana pesa maana pesa na dhahabu ni Mali yake na alifanyika MASIKINI ili sisi tuwe MATAJIRI ni kweli...Ukimuuliza anaweza kukwambia sijakupa pesa maana zitakuvuruga mwanangu nasubiri UKOMAE nikikupa utaniacha. Na ukishajua jibu la namna utajipanga sawasawa kiimani, lakini huku unajua kwa nini hupewi pesa kuliko kuomba na hujibiwi.
Unataka KUOA/KUOLEWA katika kipindi kisicho mpango wa Mungu au mke si wako au mume si wako, uwe na uhakika Mungu atakaa kimya. Usipouliza "KWA NINI MUNGU HUNIJIBU" huwezi kuuja Mungu kapanga nini kwako, lakini ukijua kwamba utaolewa baada ya miaka 10 lakini sasa nakuandaa kwa utumishi utakuwa na NGUVU ya kusonga mbele.
Nakwambia mambo ambayo nimepitia, miaka 6 naomba sijibwi, nakuja kuambiwa sababu ya kutokujibiwa nilichokuwa naomba nitendewe hakikuwa mpango wa Mungu.
Kwa mantiki hiyo jifunze kurudi kwa Mungu kumuuliza usilalamike, Habakuki angeendelea kulalamika na kutokurudi kumuuliza Mungu sijui mwisho wake angefanyaje.
Mungu anaweza kukwambia unalomba unamba kwa tamaa zako. Yakobo 4:1-3.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA LEO BAADA YA KUFA HUKUMU. Waebrania 9:27.
MUNGU AKUBARIKI.
.

Comments