SAA MOJA YA KULETA MAGEUZI KWA MWANADAMU.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu..
Karibu tupate maarifa ya uzima.
Saa moja tu inaweza kuleta mageuzi makubwa maishani mwako.
Saa moja tu inaweza kuyafuta majaribu ya shetani maishani mwako yaliyokutesa kwa mika 10.
Saa yako moja MUNGU anaitaka ili aitumie kwa mambo ya kukuletea faida kubwa na wakati huo huo saa yako moja shetani naye anaitaka ili akuangamize.
Marko 14:37 '' Akaja akawakuta wamelala usingizi, akamwambia Petro, Je! Simoni, umelala? Hukuweza kukesha SAA MOJA? ''
-saa moja yako ni muhimu sana.
-Saa moja yako kwa ajili ya maombi kila siku ni muhimu sana maana inaweza kuleta majibu kwenye hitaji lako.
-Saa moja ya kuombewa  inaweza kukufanya usiishi na mapepo tena tena wala laana za wanadamu.
-Saa moja ya kukatazwa kumwabudu Mariam inaweza kukufanya jina lako likaandikwa kwenye kitabu cha uzima kama tu ukitubu na kutokurudia tena.
-Saa moja ya kufundishwa kwamba usiabudu visanamu vilivyowekwa makanisani  inaweza ikakufanya ukaandikwa jina lako kwenye kitabu cha uzima. Ndugu pita njia ile nyembamba ambayo ndiyo ya uzima wa milele.
-Saa moja ya dua ni muhimu sana kwako kama tu unamsihi MUNGU katika KRISTO pekee. Dua maana yake ni maombi ya kusihi na unyenyekevu mkubwa kwa BWANA.
-Ni hasara kuu kama unaitumia saa yako moja kwa shetani.

-Saa yako unaitumia kwa ajili ya nini?
Kama ambavyo hakuna ajuaye saa ya kurudi kwa BWANA YESU ndivyo wengi watajifurahisha kwenye dhambi wakidhani watatubu baadaye kumbe baada ya kifo pia ni hukumu. itumie vizuri saa yako. Mathayo 24:36 '' Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila BABA  peke yake.''
Kumbe kuna SAA ILE ya siku ya mwisho. je utakuwa wapi ndugu?  Sio saa moja tu ndiyo ya kumtukuza MUNGU bali kila saa moja yako mche MUNGU.
Unaweza kujiuliza kwamba '' Kwanini hawa walitumia muda mfupi kumtukuza MUNGU na MUNGU akatenda muujiza?''
Mfano hai ni kwamba 
MUNGU hukaa kwenye sifa hivyo kumsifu MUNGU kwa muda wa chini ya saa moja tu kunaweza kuleta utukufu wa MUNGU(2 Nyakati 5  13-14, hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya MUNGU imejaa utukufu wa BWANA.   ''
MUNGU anahitaji saa moja yako ya kumtukuza ili ajidhihilishe kwako.
Alipo BWANA ndipo pahali salama.
-Saa moja ya kujifunza neno la MUNGU kunaweza kumfanya mtu atubu na kupata cha uzima wa milele(Warumi 10:13, kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. ).
Saa moja yako unaitumia kwa ajili ya nini?
-Lisaa limoja linaweza kufanya mageuzi makubwa maishani mwako.
-BWANA YESU anahitaji saa yako moja ili akuandike jina lako kwenye kitabu chake cha uzima kama tu utatubu.
-shetani analitafuta lisaa lako moja tu ili umkosee MUNGU.

-Kufa kwa mtu hutumia muda mfupi tu  lakini pia Kumpokea YESU na jina lako likaandikwa mbinguni tukio hilo linaweza kutumia muda mfupi tu.
Saa moja fulani ya Waisraeli waliokuwa vitani kwenye wakati mgumu ilileta majibu kutoka kwa MUNGU kwamba '' Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; BWANA awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya MUNGU.-2 Nyakati 20:15'' 
Hawa walikuwa kwenye maombi ndio maana MUNGU akasema nao. Je MUNGU aseme na wewe ambaye saa yako moja uko tu kwenye uzinzi?  Haiwezekani na kama akisema na wewe basi ni kwa kukuonya tu maana hujitambui na haujui.
-Ndugu yangu, saa yako moja ya kujifunza neno la MUNGU inaweza ikaleta mabadiliko makubwa maishani mwako na hata jina lako linaweza kubadilika kutoka kuitwa mtoto wa shetani hadi kutaitwa mtoto wa MUNGU maana UKUOKOKA.
-Ndugu yangu saa yako moja inaweza kukupa ukimwi na maisha yako yakawa mafupi lakini pia saa yako moja tu kwa ajili ya maombi inaweza kuleta uponyaji kwako kwa jina la YESU KRISTO.
 -Saa yako moja ya kuwasikiliza watumishi wa MUNGU na kulishika neno la MUNGU wanalolisema kunaweza kukufanya usiende jehanamu tena hata kama umeshatoa mimba 9. Biblia inasema 2 Nyakati 20:20 '' mwaminini BWANA, MUNGU wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. ''.
Ndugu yangu Mwamini BWANA na pia waamini watumishi wake au manabii zake kwa jina jingine.
-Ndugu yangu, Saa yako moja ya kumkiri YESU na  kutubu kwake dhambi zako zote kunaweza kukupa uzima na tena kunaweza kufuta laana zote. MUNGU wala hayuko mbali, yuko karibu sana, wala haihitaji masaa kumi ndipo MUNGU akujibu bali hata muda mfupi hata kabla ya saa moja tu MUNGU anaweza kujibu  Warumi 10:8-10 '' Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.''
Ndugu nakuomba itumie saa yako moja kwa kuokoka na kisha mche MUNGU siku zote. 
-Saa yako maoja ya maombi inaweza kumfanya MUNGU ashuke  na kuwaangamiza wachawi na waganga wote waliokusumbua, ( Mika 1:3 ,  Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka. )
-Ndugu, Je hukukesha hata saa moja kwa maombi ili kumfanya BWANA ashuke na na kukushindia?
Je saa yako moja unaitumia kwa ajili ya nini?
MUNGU anakuhitaji masaa yako na siku zote hivyo usikubali kupoteza hata saa yako moja kwa shetani.
''wala msimpe Ibilisi nafasi.-Waefeso  4:27''
shetani anatafusa nafasi kidogo tu kwako ili ahakikishe huendi mbinguni hivyo MUNGU anakushauri kwamba usimpe ibilisi nafasi. Ndugu yangu hakikisha humpe shetani hata sekunde 10 wala dakika 7 wala humpi hata saa yako moja.

 Unapojikabidhi kwa MUNGU unakuwa sio mali yako mwenywe bali unakuwa mali ya MUNGU.
-Saa moja ya kuomba sawa sawa na maandiko inaweza kukuletea mabadiliko makubwa maishani mwako.
-BWANA YESU alitaka wanafunzi wake watumie  hata saa moja tu  katika maombi ili wasiingie majaribuni. Ndugu yangu agizo hilo la BWANA YESU kwa sasa linakuhusu wewe.
-Ndugu yangu   hakikisha unakula kila siku chakula cha roho yako ambacho ni neno la MUNGU. Na hakikisha huli chakula bila kuomba yaani muombe MUNGU akupe neno la kukufungua na kukuvusha ili usiende upotevuni bali uzimani. Kama unavyoombea chakula cha kimwili basi ombea pia na chakula cha kiroho ili usijeletewa uji wakati wewe unahitaji kongoro gumu ambalo ukilila na kulitii neno hilo gumu kwako litakufanya uache uchawi na kuokoka. Tukikuhubiri tu amani na upendo wewe ambaye ni mzinzi haitakusaidia hivyo tunatakiwa tukubadilishie chakula cha uzima na sasa tukufundishe kwamba ukifa dhambini unaenda kuzimu na sio mbinguni.
Saa yako unaitumia kwa ajili ya nini?
 ''Naye YESU akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.- Yohana 12:23''
Saa ya kutukuzwa kwa BWANA YESU imefika.
Hii ni saa ya kutukuzwa kwa MUNGU wetu. BWANA YESU baada tu ya kushinda kifo na mauti alitukuzwa milele. Ni heri mtumishi mwenzangu tumia saa yako kumhubiri KRISTO.
-Saa yako moja ya kumshukuru MUNGU juu ya alichokupa ni muhimu sana maana inaweza chanzo cha baraka zko zingine nyingi.
Saa moja ya kumwimbia MUNGU kwa shukrani moyoni mwako inaweza kuwa na maana zaidi kuliko kuitumia saa yako kwa shetani kwenye disko.
-Saa yako moja ya kujazwa nguvu za ROHO MTAKATIFU kwa kuombewa ni muhimu sana kwako kuliko vyote ulivyowahi kufanya kabla hujaokoka.
-Saa yako moja ya kulitafakari neno la MUNGU ni muhimu sana kwako maana ufahamu wa kimungu utakaoupata unaweza kuwa chanzo cha ndugu zako kufunguliwa.
-Saa moja ya kulisikia neno la MUNGU kwenye mkutano wa injili  unaweza kubadilisha maisha yako.
-Saa moja ya kuwa kwenye kusudi la MUNGU kunaweza kukuletea uponyaji.
Kiwete wa mlango mzuri yeye aliitumia vizuri saa yake kuwa sehemu sahihi ambayo MUNGU alikusudia kumponya ndio maana alipona, Biblia  inasema
 Matendo 3:1-9 ''Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.  Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka. Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi. Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao. Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO  wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu MUNGU. Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.''
-Ndugu yangu saa yako moja unaitumiaje?
Ndani ya saa moja makumi ya watu wanaenda mbinguni na ndani ya saa hiyo hiyo maelfu ya watu wanaenda kuzimu.
-Itumie saa yako kwa BWANA YESU. 
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
 

Comments