TABIA YA WANA WA MUNGU.


MTUMISHI; JANETH VICTOR (HUDUMA YA EFATHA-MWANZA).

Bwana YESU asifiwe..
Wana wa MUNGU wana tabia zifuatazo:


1. Mwana wa MUNGU huongozwa na Roho mtakatifu. (yohana 14:16-17), kwa hiyo hawafanyi maamuzi au jambo lolote bila kumuuliza Roho mtakatifu.


2. Wana heshimu matakatifu ya MUNGU, hivyo tabia zao humpendeza MUNGU.


3. Wana wa MUNGU huwa na hekima, (1Wafalme 3:12) na kwa sababu ya hekima huwa wana kiasi, si walafi au wanao penda kufanya mambo kupita kiasi.


4. Wana wa MUNGU wana Upendo. (wanazingatia amri kuu ya upendo).


5. Wana wa MUNGU ni wepesi wa kusikia, (Waraka wa Yakobo 1:19-23) kwa sababu hiyo, ni wepesi kutendea kazi kile wanacho sikia.


6. Wana mahali pao pa kukutana na MUNGU wao. (mahali pa kuabudia) siyo wazururaji kiroho yaani leo kanisa hili kesho kwingine!!


7. Wana wa MUNGU ni wale walio ushinda ulimwengu na tamaa zake. (1Timotheo 1:12-16).


8. Wana wa MUNGU ni waombaji (Yeremia 29:11-13) wanajua kutembea katika maagizo "kesheni mkiomba".


9. Hufanya mambo kwa faida, hawana mizaha, hawana jambo la kupoteza maana hutenda sawa sawa na maagizo (Zaburi 1:1-2).


10. Wana wa MUNGU siyo wa kulaumiwa. (1Timotheo 3:1-2).

Comments