USIFE KIROHO NA ROHO HII INAYOUA WENGI

vlcsnap-2015-01-17-13h53m38s168
Na Mwl Daudi Lubeleje

Bwana Yesu asifiwe.
Namshukuru Mungu kunipa kibali cha kufundisha somo hili la USIFE KIROHO NA ROHO HII INAYOUA WENGI, pia nakushukuru wewe kutoa muda wako kusoma somo hili maana Neno la Mungu linasema “…..tuna maneno mengi ya kunena…..; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia” Waebrania 5:11 (SUV), Unaona!! Wengi wetu ni wavivu wa kusikia. Ni Maombi yangu unapoendelea kujifunza somo hili Roho Mtakatifu akupe kuelewa na kukupitisha maeneo ambayo anataka UPONE.
UTANGULIZI:
Najua umewahi kusikia misemo hii katikati ya watoto wa Mungu “Hee! umesikia Fulani eti kanunua gari, Mara wanasema Mmmmh Fulani ana kiherehere wa kwanza kanisani hata kwa mchungaji hakosi, Nyingine utasikia wanasema Mmmmmh hivi Fulani kwa kutoa michango kisa yeye tajiri eeeh n.k”. Nyuma ya misemo hii iko roho inayoua wengi kiroho na kumwacha Bwana. Sasa tujifunze kwa kumwangalia mtume Paulo alichofanya akiwa na Timotheo alipoandika waraka kwa kanisa la wakolosai.
GUNDUA HII MAPEMA:
Neno la Mungu linasema katika Wakolosai 1:3-4 “3Twamshukuru Mungu, Baba yake Bwana wetu Yesu Kristo, siku zote tukiwaombea; 4tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote” (SUV). Ngoja nikwambie kitu hapa ambacho nataka ukione. Mtume Paulo anasema; tangu waliposikia habari kutoka kwa wakolosai ambazo zilihusu mambo makubwa mawili;
  1. Imani ya wakolosai katika Kristo Yesu
  2. Upendo waliokuwanao wakolosai kwa watakatifu wote
BAADA YA KUSIKIA, waliweza kufanya mambo makubwa mawili ambayo tunayaona katika mstari wa 3 ambayo ni;
  1. Walimshukuru Mungu
  2. Waliwaombea siku zote
Hapa ngoja niweke pozi kidogo!!. Nataka kusema na wewe mwana wa Mungu ambaye umesikia habari ya mpendwa mwenzio katika Kristo Yesu kuwa IMANI YAKE au UPENDO WAKE kuwa unakua na kuendelea vizuri, Halafu wewe badala ya kumshukuru Mungu na kumwombea kwamba Mungu azidi kumwinua zaidi unabaki kumsema vibaya na kumwonea wivu. Kwa taarifa yako iko roho nyuma yake inayotaka kukupoteza na kukuangusha kiroho, Nasema kwa jina la Yesu STUKA WEWE!!!.
Kabla sijaendelea ngoja nikuoneshe kilichomtokea Kaini baada ya hii roho mbaya, ya adui kumnyemelea na kumwonea wivu ndugu yake Habili. Twende kwenye Mwanzo 4: 3-5
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
Wapendwa wengi tupo hapa, Tunaghadhibika na nyuso zetu zinakunjamana afu tukiulizwa tunasema “Ona ameongeza gari ya pili tena, mara utakuta mwingine anasema yaani amepeleka watoto wake nje kusoma” n.k. Leo sikia Neno la Bwana kwamba “UKITENDA VYEMA HUPATA KIBALI?” (Mwanzo 4:7). Mtumishi wa Mungu usipofanya hivo Neno la Bwana linasema “Dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe,……” (Mwanzo 4:7). Ila nikutie moyo kwa neno la Bwana kuwa “Walakini yapasa uishinde” (Mwanzo 4:7).
Ukiendelea mstari wa 9 utaona Mtume Paulo anagundua mtego uliopo hapo alioweka adui unaoangusha hata watumishi wakubwa wa Mungu akisema “9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu…….”. Hebu tulia kidogo uone kilichopo hapa. Neno la Mungu linasema “kwa sababu hiyo…..” unajua ni ipi? Ukisoma kwenye Yohana 10:10 utagundua alichosema Bwana Yesu kuwa “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;………..”. Sasa daka pointi iliyopo hapo chini;
POINTI: Kwa sababu Mwivi (Adui) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu kwenye wokovu, biashara yako, familia yako au mke/mme n.k wako basi unaposikia kwa habari ya mafanikio, Baraka ,kibali, upako, huduma n.k kwa wengine usiache kuomba na kufanya dua kwa ajili yao ukimshukuru Mungu ili akuinue na wewe hapo ulipo.
Nataka nikuonyeshe jambo hili ambalo lilitokea kwa Haruni Kuhani na Miriamu watumishi wa Mungu baada ya kumsema vibaya Mtumishi wa Mungu Musa kwa pembeni afu wakitegemea Mungu atanyamaza. Twende Hesabu 12:1-2
1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke mkushi aliyekuwa amemwoa; maana alikuwa amemwoa mwanamke mkushi.2 Wakasema, je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao”.
Sasa mimi sijui wewe umemnenea nini mwanakwaya mwenzako, mchungaji wako au mwinjilisti mwenzako n.k ila nataka uone kuwa Mungu anasikia maneno yako!!!. Hii ni roho iko nyuma ina ajenda ya siri kukuangusha jitambue na kujielewa mtoto wa Mungu.
UFANYE NINI SASA?:
Nasema kuwa ni lazima kupona na kuvuka huu mtego wa shetani alioweka ili kutunasa watoto wa Mungu. Ngoja nikwambie Neno la Bwana katika 2 Wakorintho 2:11 linasema kuwa “……hatukosi kuzijua fikira zake (shetani)”. Haleluya!!! Huyu Mungu ni mwema ametupa neema ya ajabu kujua fikira za adui yetu shetani.
Mtume Paulo akimwandikia filemoni  katika ule mstari wa 6 anasema “ili kwamba ushirika wa Imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo”. Huu mstari katika biblia ya English Standard Version (ESV) unasema “and I pray that the sharing of your faith, may become effective for the full knowledge of every good thing that is in us for the sake of Christ”.  Nataka nikufunulie siri iliyopo hapa ambayo wengi tumeikosa. Tunapokuwa nyumbani mwa Bwana kama Mwili wa Kristo wote tunakuwa na Ushirika wa Imani au Sharing of faith. Ushirika wa Imani ndani ya kanisa unafanya kazi ya kuvumbua na kugundua vile vitu Mungu ameweka ndani ya mpendwa mwenzio. Kwa maana nyingine Ushirika wa Imani unafanya uweze kuacknowledge kila kitu chema kilicho ndani ya mshirika mwenzio. Hebu daka hiyo pointi hapo chini;
POINTI: Tunapofikia hali ya ushirika wa Imani ndani ya kanisa na kuweza kugundua na kuvumbua vitu vya thamani vilivyo ndani ya wenzetu katika mwili wa kristo, Ndipo tunaweza kushinda ile hali ya kuwasema vibaya, kuwaonea wivu, kuwatangaza kwa mabaya wale watu Mungu ametia kitu ndani yao iwe kibali, upako kwenye huduma n.k bali tunaweza sasa kukaa nao na wakatumegea siri ya kufanikiwa kwao.
Hivyo ni Maombi yangu kwa Mungu tuweze kuona hili na kudumisha ushirika wa Imani ndani ya kanisa. Ngoja nikuongezee mistari kadhaa inayoonyesha ushirika wa Imani kwa watakatifu ulivyo.
Romans 1:11-12 “11 For I am yearning to see you, that I may impart and share with you some spiritual gift to strengthen and establish you; 12 That is, that we may be mutually strengthened and encouraged and comforted by each other’s faith, both yours and mine.
HITIMISHO:
Mungu wa mbinguni, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo akubariki sana, najua kwa hakika Bwana amesema nawe katika somo hili na kiwango chako cha Imani kimekua. BARIKIWA NA BWANA!.
NA Mwl . DAUDI LUBELEJE
0764771298 & 0652034083
lubelejedaudi@yahoo.com

Comments