BWANA YESU atukuze ndugu.
Karibu tujifunze habari njema za ufalme wa MUNGU.
''BWANA Alinitokea Zamani, Akisema, Naam, Nimekupenda Kwa Upendo Wa Milele, Ndio Maana Nimekuvuta Kwa Fadhili Zangu-Yeremia 31:3.''
Ndugu zangu MUNGU ametupenda tangu kabla hatujazaliwa, ndio maana hata akaruhusu tutoke salama kwenye matumbo ya mama zetu na tuishi kwenye dunia aliyoiumba yeye.
Ni miaka mingi bado MUNGU anaendelea na upendo wake kwetu ndio maana tuko salama. Mababu zetu tangu zamani walimkosea MUNGU, walifanya maovu ambayo hata sisi tumeyarithi kutoka kwako. Lakini MUNGU bado akatupenda kwa kuandaa ukombozi kwetu.
MUNGU Anatupenda Sana.
Na Kwa Kuonyesha Upendo Huo MUNGU Alimtoa BWANA YESU Ili Atuokoe(Yohana 3:16, Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. ).
KRISTO Alikufa Tulipokuwa Tungali Wenye Dhambi(Warumi 5:8-11, Bali MUNGU aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa KRISTO alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na MUNGU kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika MUNGU kwa BWANA wetu YESU KRISTO, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho. ).
- MUNGU Ameonyesha Upendo Wake Mkuu Sana Kwetu Wanadamu.
WAJIBU WETU WANADAMU NI:
2. Ni Kutubu(Matendo 3:19, Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; )
3. Ni Kuenenda Kwa Roho Huku Huzitazamii Tamaa Za Mwili(Warumi 8:5, Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. )
4. Tuzae Matunda (Yohana 15:16, Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni. ) -Matunda Ni Watu Tutakaowaleta Kwa YESU. Enendeni Ulimwenguni Kuwashuhudia Watu Habari Za Uzima, Agizo Hilo Ni La Wote Waliookolewa(Marko 16:15-16, Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. ).
Ndugu Je Unajua Kwamba YESU Anakupenda Upeo? Je Unajua Maana Ya Kupendwa Upeo? Biblia Katika Yohana 13:1 Inasema Kwamba YESU Alitupenda Upeo. Yohana 13:1 '' Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, YESU, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa BABA, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. ''
Ndugu Husika Na Upendo Wa MUNGU.
''Tubuni; Kwa Maana Ufalme Wa MUNGU Umekaribia(Mathayo 3:2).''
Toba ya kweli ni muhimu sana.
-Toba inaweza ikasababisha upate uzima wa miele.
-Toba inaweza kukufanya ukubaliwe na MUNGU hata kama siku za nyuma ulifanya mabaya kiasi gani.
-Toba humfanya MUNGU ashughurike na wewe hata kama ulifanya mabaya sana.
-Toba hukupatanisha na MUNGU.
-Toba hukufanya ukubaliwe na MUNGU.
-Toba itakufanya uwe ''heri'' badala ya ''ole''
BWANA YESU Yuaja Ili Kumlipa Kila Mtu Kama Kazi Yake Ilivyo(Ufunuo 22:12, Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. ).
Kama hukutubu ni hasara maana YESU akija atawalipa kila mwanadamu sawasawa na matendo yake. Wema wataenda uzima wa milele na wabaya watenda dhambi wataenda motoni.
Kwa leo naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

1. Ni Kuupokea Upendo Huo Kwa Kumpokea YESU (Yohana 1:12-13,Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. )

Comments