UTUMISHI NA KANISA

vlcsnap-2015-01-17-13h53m38s168
NA MWL. LUBELEJE DAUDI

UTANGULIZI:
Tukisoma katika 1 Wakorintho 3:9 Neno la Mungu linasema “Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu;…….”. na katika Warumi 8:28 Tunapata kujua kuwa “………katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao…..yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake”. Katika mistari tumesoma hapo juu tunapata pointi hii;
Sisi ni wafanya kazi pamoja na Mungu (we are God’s fellow workers au we are labourers together with God) maana Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika mambo yote (walioitwa kwa kusudi lake)
Mimi na wewe tumeitwa kwa kusudi la Mungu. Katika Waefeso 1:4-5 Mtume Paulo anawaambia wapendwa walioko efeso kuwa Mungu alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo.
Mungu anapofanya kazi na sisi hutupa maelekezo (instructions, directions) ya namna ya kufanya kazi. Tunaweza kusema kwa namna nyingine kuwa Hutufundisha na Kutuonyesha mahali pa kupita palipo sahihi kwetu. Angalia katika Zaburi 32:8 na Isaya 9:6 inasema;
Zaburi 32:8 “Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama”.
Isaya 9:6 “……..Naye ataitwa jina lake, mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu.……”
Tunapofanya kazi na Mungu hatujiongozi wenyewe katika namna ya kufanya kazi, Bali katika kila hatua ya kazi husika tunamtegemea Mungu atuonyeshe namna ya kufanya kazi kwa hatua hata kufika mwisho. Iwe Mungu amekuita kuwa Mchungaji, Mwalimu, unapofanya kazi na Mungu katika eneo hilo tegemea KUONGOZWA NA MUNGU MWENYEWE.
Pointi: Ni hatari kujipa maelekezo mwenyewe unapofanya kazi ya Mungu maana umeitwa hujajiita mwenyewe
Ipo mifano kadhaa kwenye biblia ya watumishi wa Mungu mbalimbali waliofanya kazi na Mungu wakipokea maelekezo katika kazi hizo; Mfano Musa (soma kwenye kutoka 3), Yeremia (soma yeremia 1:7), Paulo n.k.
Napenda kusema kuwa Tutegemee kuona Mungu anatupa kazi za kufanya mfano; Mzigo wa kuomba, kuhubiri injili n.k.
SWALI: Je Mwitikio wangu na wako (Response) kwa Mungu unapopewa kazi (Assignment) ya kufanya ukoje?.
NGAZI NNE ZA KUITIKA KWA MUNGU UPEWAPO KAZI YA KUFANYA
Zipo ngazi nne ambazo mtu huitika anapopewa kazi (huduma) na Mungu ya kufanya
Pointi; “Kuitika kwako kwa Mungu (response) huonyesha Kiwango cha utii wako kwa Mungu na namna unamvyomuweka Mungu katika nafasi gani katika maisha yako’
Ngazi hizi nne zimeainishwa kama ifuatavyo;
  1. NAENDA BWANA; ASIENDE
Tukisoma katika Mathayo 21:28-30 tunapata maelezo yafuatayo;
28 Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu. 29 Akajibu akasema, naenda Bwana; asiende.
Huyu mtu alimwambia mwana wa kwanza “Mwanangu leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu”. Unaweza kujiuliza kwanini asingesema mwanae aende kesho akafanye kazi kwenye shamba la mizabibu, au unaweza kujiuliza hivi kwanini asingeenda kwa mtoto wa pili?.
Kuna kitu cha ajabu binafsi huwa najifunza kuwa Mungu anapotuchagua kufanya kazi au huduma Fulani huwa lipo kusudi lake kamili juu yetu. Ukisoma katika Yeremia 1:5 unaona Mungu anasema;
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa (nalikutenga); Nimekuweka kuwa nabii (mwalimu, mchungaji, mwinjlisti, n.k) wa mataifa”
Jambo la kusikitisha ni kuwa wengi wetu tunajibu kama huyu mtoto wa huyu mtu tukisema NAENDA BWANA lakini ni wazi kuwa hatuendi wala kufanya kile tulichokubali tutafanya. Ni kweli kuwa ‘Hiki ni kiwango kinachoonyesha tabia ya kutokutii na kudharau Neno la Bwana.
Tusome baadhi ya mistari hapa chini
Mithali 13:13 Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu
Luka 19:13,15, 20-24 13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake. 20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako,ambalo nililiweka akiba katika leso.21 kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda; 23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake? 24 Akawaambia, waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.
Anayekaa katika ngazi hii yupo katika hatari ya kufanya dhambi kwa kusudi ukisoma katika waebrania 10:26 maana Unamwambia Mungu kuwa nitafanya kazi uliyonipa halafu hufanyi kwa kusudi.
Pointi; Kwa mtoto wa Mungu hutakiwi kukaa kwenye kiwango hiki
SOMO LITAENDELEA KWA MAWASILIANO 0764771298

Comments